Ya Ruto na Odinga Kuwagharimu Mbowe/Dr Slaa/Shibuda

Ya Ruto na Odinga Kuwagharimu Mbowe/Dr Slaa/Shibuda

matasha

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
378
Reaction score
400
Napenda kueleza kuwa mimi ni mfuatiliaji sana wa siasa za Kenya. Namshangaa Odinga kulalamika kuwa amedhulumiwa kwenye uchaguzi, anabishana na ukweli. Ukweli ni kwamba siku alipogombana na Ruto ndipo siku alipopoteza urais. Ruto ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kule bonde la ufa ambalo linakaribia wapiga kura asilimia 30. Huwezi kupoteza rift valley ukawa rais kenya. Odinga alishindwa kumvumilia Ruto ambaye ni a very controversial politician.

Hali hii ya kushindwa kuwavumilia wanasiasa 'controversial" ndani ya chadema itakigharimu sana chama kama ilivyoigharimu ODM. Nimesomo mahali eti chadema bado wanakazania kumfukuza Shibuda. Nina ushahidi pamoja na kwamba hardliners watanipuuza kuwa Shibuda ana ushawishi sana usukumani ambayo inawapiga kura wengi. Hii inatokana na ujasiri wake wa kuwatetea wakulima wa pamba na wafugaji kwa muda mrefu. Lakini Shibuda anazifahamu sana fitna za kisiasa hasa za usukumani. Waulize CCM wanamfahamu, maana hata pamoja na kumfanyia visa vingi, alishinda Maswa kwa kishindo na kupata pia madiwani wengi. Ni ukweli pia kuwa baada ya Chadema kukosana na Shibuda ushawishi wa Chadema kwa Wasukuma umepungua, nina ushahidi, fuatilia hata uchaguzi wa madiwani uliopita.

Ushauri. Shibuda ni mtu "controversial" lakini muhimu. Gharama ya kumvumilia ni ndogo kuliko kumfukuza. Ukimfukuza leo kwanza ataenda mahakamani na ataendelea kuwa mbunge lakini pia atalitumia jukwaa vibaya litakiumiza sana chama. Mimi naamini, kiongozi mzuri ni yule ambaye anaweza pia kuwaongoza watu wanaotofautiana nae kimawazo na pia watu controversial. Namshauri Mh Mbowe ajaribu kukaa na Shibuda na amuulize anataka nini. Nimeshawahi kukaa nae mara nyingi, anacholalamikia ni kwamba chama kimemtenga. Mchawi mpe mwanao, ningekuwa mimi Mbowe ningemteuwa kuwa waziri kivuli wa kilimo na mifugo. Acha akawatetee wasukuma wenzake lakini chama kijengeke kuliko kuhangaika nae. Hata nilikuwa na Mbunge mwenzake wa Maswa Magharibi siku moja anakiri Shibuda anaushawishi mkubwa. Naomba mkumbuke maneno yangu, Chadema will never be the same without Shibuda, Zitto et al. Chama kijenge uvumilivu ambapo CCM ndipo walipoizidi Chadema. Wao wanauvumilivu hata kwa wale wanaoitukana CCM. Nadhani tunakubali, akina Mwampamba na Shonza kelele zao si kwamba hazina madhara, tungekaa nao tangia mwanzo mambo yangemalizwa vizuri.

Mwisho namshauri Rais wangu Dr Slaa ambaye nampenda sana, ajifunze kutofautisha mamlaka ya dola na uongozi wa siasa. Ukiwa rais wa nchi unakuwa na mamlaka ya dola, unaweza kumfukuza mtu yeyote wakati wowote. Ila kwenye siasa hili haliwezekani, ni lazima kuwavumilia watu, kikubwa kutana nao, wasikilize shida zao, washauri na kuwa nao karibu. Siasa ni hiari, mamlaka ya dola hayahitaji kuwa na watu wenye hiari.

Long live Chadema!
 
Pamoja na kwamba sikubaliani na wewe asilimia 100%, kuna ukweli ndani yake. Badala ya Chadema kupambana na wale watu wenye mitazamo tofauti au maslahi tofauti, ni vizuri kuangalia namna ya kuwa accomodate. Lengo ni kushika dola, mambo mengine tuweke pembeni. Ukishashika dola ndipo sasa unaweza kukunjua makucha!
 
Shibuda ana kura ngapi katika uchaguzi? Kitu unachosahau ni kwamba siasa za Kenya zimetawaliwa na ukabila. Ruto aliweza kuvutia kura zote za Kalenjin kwa upande wa Kenyatta. Je, Shibuda anaweza kuvutia kura zote za Wasukuma? Jibu ni hapana.
 
Anatengwa kwasababu ni muongeaji mno..kuna mambo ambayo ni "inside" issues huwezi kumwambia kila mtu, busara ndogo tu huwa inahitajika, huhitaji kuwa rocket scientist kujua kuwa you don't share inside info with the "other side".. Sometimes the most trivial info could be very compromising..!! Sasa huwezi kuweka close mtu anaye-behave kwa namna hiyo!! Hao Shonza na wenzake are simply pathetic!!!!! Lakini yote uliyoshauri kwa ujumla wake yanaleta maana!
 
Sabau hatokei kaskazini ndio maana wanamtenga na pia wanahisi mbio za urais atawapita
 
Acha unafiki long live chedema kitu gani? Chadema kama chama haziwezi kuvumilia mamluki, na siasa za Kenya inaonekana huzijui vizuri
 
Gharama na nguvu zinazotumiwa na mbowe na slaa dhidi ya wanaotafutiana nao kimsimamo ni kubwa mno na ndipo wanajikuta wanawapa tenda za kiusalama watu wasiokuwa na mbinu za kiusalama ( lwakatare, ludovi na hata ben saa nane).

Viongozi hawa watambue imani ambayo masikini wa tanzania walikuwa nayo kwa CHADEMA, leo propaganda hii ya ugaidi na tuhuma za mauaji itaendelea kuwafukuza wapiga kura wanawake ambao siku zote CCM inawaaminisha kuwa vyama vya upinzani ni vya kigaidi, watatumia hii kujistfy mambo haya.

Aidha nashauri viongozi hawa waepuke shutuma zinaletwa kuhusu maisha yao binafsi hasa tuhuma kuwa wenza wao ( rasmi au sio rasmi) wana kauli kubwa sana kuhusu chama, kwenye suala la lwakatare mtapewa taarifa nini namaanisha hapa.
 
SIDHANI unafutatilia SIASA za KENYA KI HAKI... Kati YA RUTO na MUSYOKA mwenye Wapiga kura wengi ni MUSYOKA na ODINGA aliyoosha an OLIVE BRANCH kwa MUSYOKA; Ukiangalia pia KENYATTA alikuwa na NAJIB BALALA wa PWANI lakini ODINGA alishinda MOMBASA; LAMU Maeneo yote ya Waislamu PWANI; NORTH - TURKANA, Some Parts of Rift Valley... Yeye Ukiangalia alipata kura sehemu zote za KENYA ukilinganisha na KENYATTA...

Sasa nadhani tunataka RAIS wa watu wote sio wa KABILA MOJA tu au wa ENEO MOJA TU... Sasa kama wewe UNAONGELEA MASWA na SHIBUDA -- Maswa ni Wasukuma... Mwanza Mjini ni Wasukuma... ILEMELA ni Wasukuma Maenelo hayo CHADEMA imeshinda... Sasa hatuangalii ENEO tunaangalia NCHI NZIMA SISI SIO KENYA...

Kama wewe Unawaza KENYA... na MAKABILA MAKUBWA KUGOMBEA URAIS... Mawazo yako ni FINYU na ni wa kuogopa kama UKOMA... there is no COORELATION @ all... SIASA zetu ni tofauti kabisa na za KENYA... wao ni siasa za URITHI

Kwahiyo tafadhali sana toa hayo Mawazo kwenye AKILI YAKO!!!

Inaonyesha JINSI SISI WATANZANIA sasa hivi tusivyojua SIASA...
 
Kwa upande wa Zitto nakubaliana na wewe kabisa....

Ila kwa upande wa Shibuda labda huko kwao Shinyanga....Ukizungumzia wasukuma unazungumzia Mwanza na Shinyanga na Tabora kwa mbali....Shinyanga ina wasukuma wabishi maarufu kama wanyantuzu na huku kuna wabunge kutoka CHADEMA,CCM na UDP...
Mwanza kuna wabunge wa CHADEMA na CCM...
TABORA ni ngome ya CCM...

Nachotaka kuzungumza hapa ni kuwa wasukuma wa Mwanza hawapendi majigambo na maneno ya taarabu ambayo hutumiwa sana na Shibuda....walishangaa hata Shibuda alivyopokelewa CHADEMA.

NB: Anaweza kuwa na mvuto Shinyanga...lakini akawa anakiua chama,kufikia 2015 atimize lengo lake halafu atimke..
When advantage outweighs disadvantage,that is good but the viceversa is bad!
 
Ushauri wako ni mzuri japo siasa za ruto ama uwezo na ushawishi wa ruto kamwe huwez kumlinganisha na shibuda na shibuda hakuna naye mfukuza chama atajifukuza mwenyewe, kwani alishazoeleka kwa matendo yake na tabia zake huwez kuwapinga wenzako hadharani kwa misimamo isyo na maslahi kwa wananchi, kwa mfano ni nini cha maana ambacho alishakipendekeza shibuda kwa maslahi ya wana kanda ya ziwa kisha akapingwa na viongozi wa chadema?

Yeye amepinga mala ngapi hadhalani mawazo ya wanachadema wenzake tena hoja enye maslahi kwa taifa?tunapofkiri kuwa shibuda anaonewa lazma pia tutambue nini wajibu wake kama mbunge wa chadema?
 
Shibuda ana kura ngapi katika uchaguzi? Kitu unachosahau ni kwamba siasa za Kenya zimetawaliwa na ukabila. Ruto aliweza kuvutia kura zote za Kalenjin kwa upande wa Kenyatta. Je, Shibuda anaweza kuvutia kura zote za Wasukuma? Jibu ni hapana.
shibuda na momose cheyo wana ushawishi sana usukumani hasa maswa na bariadi,huo ndo ukweli.
 
shibuda na momose cheyo wana ushawishi sana usukumani hasa maswa na bariadi,huo ndo ukweli.

Momose Cheyo labda kijijini mwake. Mbona hata hawajahi kupata 10% ya kura anapogombea urais? Shibuda, kwa sasa hebu nisiseme chochote. Uzuri wa Wasukuma hawako monolithic, kama walivyo wa Kalenjin, eti Moi atawaambia mpigieni kura Kenyatta na wote kama makondoo wanafuata tu.
 
Shibuda ana kura ngapi katika uchaguzi? Kitu unachosahau ni kwamba siasa za Kenya zimetawaliwa na ukabila. Ruto aliweza kuvutia kura zote za Kalenjin kwa upande wa Kenyatta. Je, Shibuda anaweza kuvutia kura zote za Wasukuma? Jibu ni hapana.

Ni kwa nini thread hizi ziletwe muda huu?Ni kwanini mtu anukuliwe kwamba ameichoka Chadema muda huu?

Fumbo watawafumbia wajinga tu ila wajanja.....!
 
shibuda na momose cheyo wana ushawishi sana usukumani hasa maswa na bariadi,huo ndo ukweli.

Hivi Kwa hii political factor,tunaweza kufanya analysis intellectually na kujiuliza asilimia ya kura alizopata Cheyo muda wote aliogombea urais kulingana na population ya wasukuma(sipendi analysis za kikabila)
 
matasha

Kwa kweli mawazo yako ni mazuri sana tena sana tu na nina hakika hilo limegundulika mapema sana na hata hivyo Shibuda naye yupo sambamba kabisa na viongozi wote wa juu na kinachoendelea kwa sasa ni mambo mazuri yatarajiwayo na Watanzania hakika!

COPY

Yericko Nyerere
Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nashawishika kusema yumkini wewe ndiye Shibuda mwenyewe unajaribu kujiokoa baada ya kuona maji yamezidi unga; Twende sawa;.



  • Yaani Shibuda afadhili mtandao wa masalia kisha tumchekee eti kwa vile ni "controversial" lakini muhimu.
  • Yaani Shibuda apingane na misimamo na sera za chama kisha tucheke nae ati kwa vile ana ushawishi mkubwa.
  • Yaani Shibuda awatukane na kuwakashfu viongozi wa CHADEMA kisha tumkumbatie kwa sababu ni influencial.
  • Yaani Viongozi wa CHADEMA wamuite Shibuda na kumbembeleza anataka nini, ili iweje?

Mkuu ni vyema ukatambua viongozi wa CHADEMA wametumia busara ya hali ya juu sana kumvumilia huyo Shibuda mpaka hapo alipofika kwa sasa. Hakuna chama chochote kiwezacho kumvumilia Shibuda kwa undumila kuwili na unafiki wake na ndo maana alitimuliwa huko magambani.

Mkuu acha kutupotosha wana JF; hakuna mwenye mpango wala nia ya kumtimua Muishiwa Shibuda; Dawa ya muishiwa Shibuda inachemka na atanywesha na wapiga kura wake ikiwa ya moto kabla haijapoa ifikapo 2015.

Shibuda kajitenga mwenyewe na siyo viongozi wa CHADEMA.
Ni dhahiri wewe si mkazi wa Shinyanga, na wasukuma huwafahamu vizuri.

Ushauri wangu kwako; ni vyema ukafanye utafiti kabla hujaingia mtandaoni na kuanza kupika na kusambaza majungu.
 
Shibuda ana kura ngapi katika uchaguzi? Kitu unachosahau ni kwamba siasa za Kenya zimetawaliwa na ukabila. Ruto aliweza kuvutia kura zote za Kalenjin kwa upande wa Kenyatta. Je, Shibuda anaweza kuvutia kura zote za Wasukuma? Jibu ni hapana.
Tanzania hatuna ukabila ila kuna watu wenye ushawishi wa kisiasa maeneo fulani ya nchi, Shibuda ana ushawishi kwa maeneo makubwa ya usukumani, hio ndio ukweli
 
Sabau hatokei kaskazini ndio maana wanamtenga na pia wanahisi mbio za urais atawapita
Si kweli, kuna watu wana nafasi kibwa na nyeti ndani ya chama ambao si wa kaskazini. Kwamba chadema ni chama cha kaskazini ni hoja dhaifu sana. Ukiambiwa uwataje watu wa kaskazini ndani ya vyombo vya maamuzi inaweza kuwataja?
 
Acha unafiki long live chedema kitu gani? Chadema kama chama haziwezi kuvumilia mamluki, na siasa za Kenya inaonekana huzijui vizuri
Hakuna chama kisicho na mamluki na dawa ya mamluki si kimfukuza na kulumbana nae bali kumnyima tu information muhimu za chama
 
Back
Top Bottom