ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,370
- 4,643
Fumbo fumba kwa kapuku,wa hekima aelewa,
Hata kama ala kuku,kapuku hatoelewa,
Ukweli haupo huku,huku sote tumelewa
Ya nini kudanganyana,Ukweli tunauona
Wengi kunguru waoga,mwakimbiza bawa zenu
Hata kama mkioga,mbadili nguo zenu
Fedheha yenu na woga,msirithishe wana wenu
Ya nini kudanganyana,ukweli tunauona
Tanga kwetu napajua,ukahaba si tabia,
Mwajitia mwatujua,kwetu wazuri tabia,
Kweli mambo twayajua,ila uzuri tabia,
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona.
Wachaga twapenda pesa,nani amewadanganya
Kukosa pesa kudesa,utaishi kama panya
Sote twaitaka pesa,ila si twaisakanya
Ya nini kutidanganya,ukweli tunauona
Waswahili barazani,mnatuita wavivu
Msione mkadhani,mkatuonea wivu
Wengi tunazo vichwani,Hekima na utulivu
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
MaCCM bazazi,mambo yenu ya ajabu
Mnajitia wazazi,na mambo yenu yajabu
Mtatuia uchizi,na uo wenu ubabe
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Na mwenye Dar es Salaamu,umezidi kutuchosha
Kila ni siku ni salamu,Na sisi watusotesha
Dada Mange nafahamu,Aliwahi tuonyesha
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Sizonje usihamaki,jua cheo ni dhamana
Piga kazi tenda haki,Epuka kukamatana
Mimi sitaki ubaki,ishirini twaachana
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Na ninyi vikaragosi,msoishiwa viroja
Mmejawa na mikosi,mmeishiwa na hoja
najua nyie polisi,na kazi yenu ni moja
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Tundulisu mahututi,ahueni anapata
Usizue tashititi.Silaa atapatapa
Usigeuke maiti,chocote hutokipata
Ya nini kutudanganya,Ukweli tunauona
Unajikosha kwa ngosha,Kwa cheo kisichojina
Utabaki kujikosha,na utabaki na jina
Utarudishwa Arusha,Utabatizwa majina
Ya nini kutudanganya.ukweli tunauona
Fikirani nimechoka,kisirani kimepanda
Kiki zenu nimezichoka,wakati bei zapanda
Sifa hamjazichoka,tavuna mlichopanda
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Tamatini hitimisho,ukweli tunauona
Kupatiana vitisho,wabaya tutaonana
Msiilaumu kesho,kwa yale yenu ya jana
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Hata kama ala kuku,kapuku hatoelewa,
Ukweli haupo huku,huku sote tumelewa
Ya nini kudanganyana,Ukweli tunauona
Wengi kunguru waoga,mwakimbiza bawa zenu
Hata kama mkioga,mbadili nguo zenu
Fedheha yenu na woga,msirithishe wana wenu
Ya nini kudanganyana,ukweli tunauona
Tanga kwetu napajua,ukahaba si tabia,
Mwajitia mwatujua,kwetu wazuri tabia,
Kweli mambo twayajua,ila uzuri tabia,
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona.
Wachaga twapenda pesa,nani amewadanganya
Kukosa pesa kudesa,utaishi kama panya
Sote twaitaka pesa,ila si twaisakanya
Ya nini kutidanganya,ukweli tunauona
Waswahili barazani,mnatuita wavivu
Msione mkadhani,mkatuonea wivu
Wengi tunazo vichwani,Hekima na utulivu
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
MaCCM bazazi,mambo yenu ya ajabu
Mnajitia wazazi,na mambo yenu yajabu
Mtatuia uchizi,na uo wenu ubabe
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Na mwenye Dar es Salaamu,umezidi kutuchosha
Kila ni siku ni salamu,Na sisi watusotesha
Dada Mange nafahamu,Aliwahi tuonyesha
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Sizonje usihamaki,jua cheo ni dhamana
Piga kazi tenda haki,Epuka kukamatana
Mimi sitaki ubaki,ishirini twaachana
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Na ninyi vikaragosi,msoishiwa viroja
Mmejawa na mikosi,mmeishiwa na hoja
najua nyie polisi,na kazi yenu ni moja
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Tundulisu mahututi,ahueni anapata
Usizue tashititi.Silaa atapatapa
Usigeuke maiti,chocote hutokipata
Ya nini kutudanganya,Ukweli tunauona
Unajikosha kwa ngosha,Kwa cheo kisichojina
Utabaki kujikosha,na utabaki na jina
Utarudishwa Arusha,Utabatizwa majina
Ya nini kutudanganya.ukweli tunauona
Fikirani nimechoka,kisirani kimepanda
Kiki zenu nimezichoka,wakati bei zapanda
Sifa hamjazichoka,tavuna mlichopanda
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona
Tamatini hitimisho,ukweli tunauona
Kupatiana vitisho,wabaya tutaonana
Msiilaumu kesho,kwa yale yenu ya jana
Ya nini kutudanganya,ukweli tunauona