Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa Msikitini...


Nunua i pad weka msahafu wako kwenye i pad. Ama hujui i pad ni nini?
 
Mtazunguka mbuyu wee wakati aliyepanda mbegu ya haya yote yupo na anafahamika! Na mbaya zaidi yupo kimya tu kama vile haoini na hasikii
 
Hata kama mama wa 'Bedui' alijibu kwa ujeuri juu kitendo cha yule mtoto amabacho si cha kiungwana, ilitakiwa yeye mwenye kosa ndiye ahukumiwe kwa kosa lake BINAFSI. Iweje kosa la watu wawili liwahusishe watu wengine wasiohusika? Usijaribu kuhalalisha uovu uliofanywa na hao Waislamu kwa sababu ambazo hazina mashiko. Tafadhali soma kwa makini ujumbe wa Mjengwa ambaye pia ni Mwislamu utapata kitu cha kukusaidia . Punguza jaziba na Mungu atakusaidia.Amen
 
Sasa nani ataweza kunishawishi niondoe dhana yangu kwamba uislamu ni NGO iliyojengeka kwenye misingi ya vurugu? Kila mahali duniani utasikia vurugu za waislam dhidi ya dini zingine. Maggid keshasema Boss wa Uislam hakuwa na pupa, labda alisahau kuwaambia watu wake wafanyeje likitokea tena hilo, au aliwaambia lakini kwa kuwa msahafu umeandikwa kwa lugha wasiyoijua wengi hawasomi, na wanaosoma wamekariri hawajui maana yake, wanaojua wanawatumia wafuasi wao kukamilisha malengo tofauti na Mtume wao. Mtume atawakana siku ya siku, maana hinaonyesha hakubaliani na vurugu. Maana yake wanaofanya vurugu ni wahuni tu na wala hawana dini mioyoni mwao. Kisasi ni cha Mungu na wala binadamu hawezi kumsaidia Mungu sababu Mungu huyo anao uwezo wa kufanya chochote apendavyo.
 
Ndugu umenena sahihi,ila suala la msingi sio umri wa yule mtoto bali ni kuvumiliana,hata angefanya mtu above 18 years.Nimehudhuria mara nyingi mihadhara ya waislam huwa wanachoma biblia na wakristo wakiwa around bila reaction yeyote,na huu ndo uvumilivu wa aina tunaohitaji.Swali fupi,kwanini hiyo hasira haikuelekezwa kwa yule mama aliyesema hayo ni makaratasi tu? kwanini ielekezwe kwenye makanisa? individual issue handled as community issue? is that right.elimu dunia duni.
 
Kaka Maggid umenena kitu kizuri sana waislamu wajaribu kupitia hi kitu natumaini watafaidika sana na somo litawaingia ikiwezekana hata misikiti humo wapelekee hili neno ulilolinena hapa tena uanze na Ponda!
 
A very educated Muslim indeed. Thank you Maggid! May the God of us all bless you today and the days to come!

 

ulikuwepo katika hilo eneo ukasikia hiyo kauli? au umesikia tu na unashuhudia kama uliyekuwepo katika tukio huyo mama akijibu utasemaje? na je ukiambiwa na mwingine haikuwa hivyo! maana issue hii kila mtu anasema alivyosikia, wengi si mashuhuda. ushabiki sio mzuri, kama unapenda haki basi usi-bias
 
Kwahiyo maswahaba huwa hawana subra!

Wewe nawe!! watu wanazungumza ya maana unaleta jokes zisizochekesha!! nyie ndio siku zoite mnapenda kushabikia udini-faida mtakayoipata ni ndogo sana ukilinganisha na hasara zake!!!

-Majid, nakushukuru kwa kuthibitisha kwamba Uislamu ni dini ya amani, tofauti na inavyoonyeshwa na baadhi yetu waislamu
 
TUngekuwa na Waislamu japo 10 ya Mjengwa hapa Tanzania, hakika nchi ingekuwa ya maana sana. Huyu ana akili. Si hawa wanaoleta vurugu. Swali kwa Mjengwa: Yule aliyekojolea Kuran kafikishwa mahakamani, je, yule aliyempelekea Kuran mbona kaachwa?

MJENGWA SIO Muislam. Huyu ni kafiri wa kutupwa. Hana mke. Ameweka hawara wa kizungu. Hawezi kujiita muislamu.
 
Nimependa maoni ya mwandishi, ni ukweli usiopingika kuwa dini zetu si kichaka cha kutenda maovu bali matendo mema, kuvumiliana, amani, upendo na utulivu na kumcha Mungu hivyo kikundi kinachofanya mambo yanayoharibu uhuru wa kuabudu wa mwingine huyo anafanya matendo ya kishetani nasi tuwaogope watu wanaoleta udini kama ukoma. Je kuna yeyote mwenye hakika kuwa dini yake ndio dini ya mwenyezi Mungu? Kitakachomwokoa mtu ni imani yake na matendo mema na si dini yake hivyo tuendelee kuvumiliana na kushirikiana maana chuki haitusaidii kwani wote ni waTz. Mungu ibariki Tz, Mungu tubariki waTz.
 

Mkuu
Huwa najiuliza kwa nini mwalimu aliwanyang'anya wamissionari shule zao na kuzifanya za serikali, kisha kila mtanzania
bila kujali dini yake wakasoma. Huwa najiuliza endapo asingefanya hivyo nadhani taifa hili lingekuwa limeangamia maana tusingewapata angalau akina mjegwa ambao wanaweza kutafakali.

Ni jambo la aibu na la kusikitisha tunapofumbia macho uhalifu kwa kisingizio cha kulinda dini. Kwanza hiyo dini niya nani? mimi naami kwamba dini zote zina wakuu wake sinaminishi mitume nazungumzia kama dini ni ya shetani mkuu wa dini hiyo ni shetani na kama ni ya Mungu Mungu ndo mkuu wa dini hiyo. Je kama dini ni ya Mungu huyo mungu anayetetewa na mwanadamu ni mungu yupi huyo.

Hicho ndicho ninachokiona kwa wakristo wanaomjua Mungu wao kwamba hana sababu ya kutetewa na mtu au binadamu. napata kigugumizi ninapo ona baadhi ya dini na hasa madhehebu ambayo yana msaidia mungu wako kujitetea huyo mungu wao kalala usingizi????. hata asijitetee, hebu tuwe wakweli tuache umamuma watu wajinga na wapumbavu tuwakemee bila kujali dini zao na tusiwaonee haya kuwapa ukweli wakati huohuo ukizingatia kuwa Usibishane na mpumbavu ukaja kuwa kama yeye.
 
Tuache mafundisho ya uogo hayata tusaidia, watoto wanajaribu mafundisho yetu je yapo sawa? kumbuka kila fundisho litajaribiwa na kizazi hiki hivyo tuwe makini na mafundisho yetu. je huyu mtoto mkristo aliitoa wapi qurani?
Mkuu hv uko dunia hii kweli..? Ina mana hujui hyo mtoto mkristo alipata wapi qurani..?
 
Waislam ubwabwa na biliani watakupinga tu Mjengwa
 
Kwa mujibu wa hadithi hii ya Mtume S.A.W inafundisha ustahimilivu bila kujali huyo Bedui alikuwa amelewa, alikuwa kichaa au vyovyote vile maana kinachosemwa ni kitendo cha kukojoa eneo takatifu bila kujua. Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar aliyasema maneno hayo siku ya tukio la Mbagala TBC alikuwa na Mkuu wa Mkoa na Kamanda Kova. Mwisho wa maneno yake akasema kuwa MAIMAMU wangelimaliza suala hilo kwa kuwaita watoto na kuwaelimisha juu ya vitabu vya MUNGU,lakini siyo kuchoma makanisa na kukusudia kuchoma kituo cha polisi. Watanzania ushabiki wa dini uliopitiliza ni mbaya sana tuwe wavumilivu na kuwafundisha vijana haki ya MUNGU WETU. Ahsante Maggid
 
Waislam tu wanapenda shari, yanayotokea Zanzibar yametkana na kukojolewa kitabu kitukutu?
 

Mkuu, ninahisi kwamba wewe ni muislamu kutokana na jinsi ulivyoandika.
Aidha unaonekana pia kwamba umebahatika kupata elimu nzuri tu. Lakini wasiwasi wangu ni kwamba elimu uliyoipata haijakuelimisha vya kutosha.

Umejaribu kutupeleka katika rejea za vitabu vya mtunzi mohamed Said, kutuaminisha mambo ya kusadikika ya kwamba ati Mwl Nyerere aliukandamiza Uislamu. Na kututaka tuamini kushindanishwa kwa dhana ati nani alipeleka kwanza MoU kwa serkali, kati ya waislamu na wakristu.

MoU ni nini?, ni sera?, hadi useme kikundi fulani kiliipeleka ya kwao kwanza kwa serikali ikakataliwa lakini ya kikundi cha pili ikakubaliwa?!!! Kama kulikuwa na MoU, lazima ilikuwa imeandaliwa kwa pamoja baina ya pande mbili zinazokubaliana kuwa na hayo maelewano.

Lakini vilevile elewa kwamba Tz, imeongozwa hadi sasa na marais wanne. Wakristu wawili na waisalamu wawili. Ina maana unataka kuwatukana waheshimiwa hao marais waislamu kwamba hawakujua kuongoza hadi wasijue kwamba ati kuna kitu kinachoitwa MoU kinachowakandamiza waislamu wenzao?

Tatizo ni kwamba badala ya kujadili hoja kwa mantiki watu wanaleta ushabiki wa kidini bila kutumia akili ipasavyo. Samahani kama nitakukwaza.
 
Wapo wachche wanaotamani hali fulani itokee nchini, lakini wapo wengi wanatamani hali fulani isitokee. Kwanini waislamu wachache wanataka kutufanya waislamu wengi hatuna akili kwa kufuata mkumbo, ambao unafaidisha watu wachache kwa malengoyangu wenyewe. Kama wanataka mapinduzi ya kidini wawapeleke Syria wakajione.. huu ni upuuzi jamani. GOMESA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…