VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Jana,Mama Salma Kikwete,mke wa Rais Jakaya M.Kikwete alipanda jukwaa la kampeni hapa Chalinze kumnadi Mgombea wa CCM,Ridhiwani Kikwete. Ridhiwani ni mwana wa Rais.Mama Salma ni mke wa Rais. Mama Salma ni mama wa Ridhiwani. Kukataa alichokiomba Mama Salma ni kumkataa Rais Kikwete. Ni kujihatarisha kimaendeleo.
Wananchi wa Chalinze sasa wako kwenye mawazo mazito. Wanawaza mustakabali wao baada ya Mama Salma kupanda jukwaani na kumnadi mwanaye Ridhiwani Kikwete. "Ni kama Mama Kikwete amekuja hapa kututisha. Hakutakiwa kuja katika hali ya kawaida ya kisiasa. Viongozi wengine wa kichama walitosha kuja kumpa nguvu Ridhiwani.Nasi tutajua cha kufanya" alisema mmoja wa wakazi wa Chalinze
Ilikuwa sahihi kwa Mama Salma Kikwete kumnadi Ridhiwani Kikwete Chalinze?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Chalinze)