Ya Magufuli na Dr. Tulia ni mpango wa CCM dhidi ya Lowassa

Robert PR

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2014
Posts
591
Reaction score
57
MAGUFULI ANAMTAKA NANI?
Katika mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, agenda kubwa imekua mawazo ya Rais Magufuli ni yapi?
1. Je Magufuli anamtaka kijana Abdulla Mwinyi mbunge wa Afrika Mashariki?

2. Je, Rais Magufuli anamtaka Job Ndugai?

3. Je, Rais anamtaka Dkt. Tulia Ackson, aliyekua naibu mwanasheria mkuu wa serikali?
Nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana katika utendaji wa serikali na Bunge. Inahitaji mtu ambaye ni mtulivu, mwenye hekima na busara katika kuendesha mambo.
Rais Magufuli anahitaji Spika ambaye hatakua mkorofi wala mpenda sifa kupitiliza. Bali Spika mwenye kufuata weledi na kanuni katika kuongoza bunge.
Rais Magufuli hahitaji mamluki wala kibaraka wa waliokua wasaka Urais. Anahitaji mtu msafi asiye na madoa wala kashfa.
Rais Magufuli hahitaji watu walewale katika serikali na safu ya mihimili ya serikali. Hawa watamsumbua na kuleta ujuaji mwingi.

Rais Magufuli ni mtu wa kazi tu. Anahitaji weledi na sio ubabaishaji.
Spika atatoka upande wa Tanzania bara, kwakua Zanzibar tayari wanalo baraza la wawakilishi. Hivyo ukimtoa Abdulla Mwinyi, wanabaki Job Ndugai mtaalamu wa wanyamapori na Dkt Tulia Ackson mwanasheria msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Ukiniuliza Magufuli anamtaka nani? Nitakuuliza unadhani mtu anaweza kuacha nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali ili abahatishe uspika? Unadhani kafanya kwa bahati mbaya?
Nani alitarajia kuwa Magufuli angekua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jibu ni hakuna, basi tumtazame vizuri Dr. Tulia Ackson. Hapo ndipo jicho la wenye kuona mbali lilipo.
Twende na Dr. Tulia.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Dkt Magufuli uwa hana timu. Yeye ufanya kazi na yoyote yule ambae ni msafi kwa maana hana ufisadi na wizi.Hivyo katika hao watatu atafanya kazi na yeyote yule. Makundi na timu sio hulka ya Dkt Magufuli.

Lakini tufanye stori iwe fupi, spika ni Job Ndungai. Wabunge wengi wa CCM wanamkubali Job Ndungai.

Kisa cha kumkubali hiki hapa:

Pamoja na kwamba kwa sasa hakuna spika, ila aliyekuwa naibu wa spika (ambae ni Job Ndungai) ushirikiana na katibu wa Bunge kufanya maandalizi ya wabunge wapya mjengoni. Ndungai kaifanya hii kazi usiku na mchana tangu Novemba 6 huko. Kwa ufupi, tayari ana kura nyingi za wabunge wa CCM.

Hivyo basi, msipoteze muda kufanya mjadala kuhusu hili la uspika. Ni Ndungai tu. Labda mjadala uhamie kwa nani atakuwa waziri mkuu wa JMT.

#NdungaiForSpeaker
 
Kama.watapigiwa.kura na.jamaa.zetu baai tutarajie.kilio.kwa.dada
.....
 
Msitufanye nyumbu kiasi hicho, tukumbushane kidogo: ni nani vile alisimamia zoezi la kugawiana nyumba za serikali na akafikia hata kumgawia hawara yake?
Iko siku atakuja kujibu!

Weka ushahidi wa tuhuma zako hapa. Kati ya vitu ambavyo vilinichekesha kwenye huu uchaguzi mkuu ni pale ambao niliona mgombea wa chama tawala anakemea ufisadi na kuonyesha kuuchukia hadi kusema akishinda urais ataanzisha Mahakama za majizi na mafisadi...lakini upande wa pili wa wapinzani....tangu kampeni zianze hadi zinamalizika...neno ufisadi, rushwa na wizi hayakutajwa kabisaaaaa. Hii ilinichekesha sana. Only in Tanzania upinzani unaogopa kutaja neno 'ufisadi'.
 
Chenge, Tibaijuka, Ngeleja wameshinda kwa kutaja ufisadi? ni nani amekudanganya kwamba Watanzania ufisadi ni ajenda yao? nchi imejaa majizi kuanzia mfagiaji mpaka Rais.
 
MAGUFULI ANAMTAKA NANI?
Katika mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, agenda kubwa imekua mawazo ya Rais Magufuli ni yapi?
1. Je Magufuli anamtaka kijana Abdulla Mwinyi mbunge wa Afrika Mashariki?

2. Je, Rais Magufuli anamtaka Job Ndugai?

3. Je, Rais anamtaka Dkt. Tulia Ackson, aliyekua naibu mwanasheria mkuu wa serikali?
Nafasi ya Spika ni nafasi nyeti sana katika utendaji wa serikali na Bunge. Inahitaji mtu ambaye ni mtulivu, mwenye hekima na busara katika kuendesha mambo.
Rais Magufuli anahitaji Spika ambaye hatakua mkorofi wala mpenda sifa kupitiliza. Bali Spika mwenye kufuata weledi na kanuni katika kuongoza bunge.
Rais Magufuli hahitaji mamluki wala kibaraka wa waliokua wasaka Urais. Anahitaji mtu msafi asiye na madoa wala kashfa.
Rais Magufuli hahitaji watu walewale katika serikali na safu ya mihimili ya serikali. Hawa watamsumbua na kuleta ujuaji mwingi.

Rais Magufuli ni mtu wa kazi tu. Anahitaji weledi na sio ubabaishaji.
Spika atatoka upande wa Tanzania bara, kwakua Zanzibar tayari wanalo baraza la wawakilishi. Hivyo ukimtoa Abdulla Mwinyi, wanabaki Job Ndugai mtaalamu wa wanyamapori na Dkt Tulia Ackson mwanasheria msomi wa chuo kikuu cha Dar es salaam.
Ukiniuliza Magufuli anamtaka nani? Nitakuuliza unadhani mtu anaweza kuacha nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa serikali ili abahatishe uspika? Unadhani kafanya kwa bahati mbaya?
Nani alitarajia kuwa Magufuli angekua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama jibu ni hakuna, basi tumtazame vizuri Dr. Tulia Ackson. Hapo ndipo jicho la wenye kuona mbali lilipo.
Twende na Dr. Tulia.
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Robert PR, Ndipo!. Hii imetulia kama Tulia!.
P.
 
Dkt Magufuli uwa hana timu. Yeye ufanya kazi na yoyote yule ambae ni msafi kwa maana hana ufisadi na wizi.Hivyo katika hao watatu atafanya kazi na yeyote yule. Makundi na timu sio hulka ya Dkt Magufuli.

Lakini tufanye stori iwe fupi, spika ni Job Ndungai. Wabunge wengi wa CCM wanamkubali Job Ndungai.

Kisa cha kumkubali hiki hapa:

Pamoja na kwamba kwa sasa hakuna spika, ila aliyekuwa naibu wa spika (ambae ni Job Ndungai) ushirikiana na katibu wa Bunge kufanya maandalizi ya wabunge wapya mjengoni. Ndungai kaifanya hii kazi usiku na mchana tangu Novemba 6 huko. Kwa ufupi, tayari ana kura nyingi za wabunge wa CCM.

Hivyo basi, msipoteze muda kufanya mjadala kuhusu hili la uspika. Ni Ndungai tu. Labda mjadala uhamie kwa nani atakuwa waziri mkuu wa JMT.

#NdungaiForSpeaker
Hivi huyo jamaa Ndugai si ndiye alimchapa fimbo kichwani mgombea mwenziwe wa ubunge wa CCM kule Kongwa hadi akazirai na kulazwa hospitali wakati wa uchaguzi uliopita?
Kwa tukio hilo peke yake, kama CCM ingekuwa chama makini kinachojali maadili hata huo ubunge angekuwa disqualified na asingeupata, lakini kwa kuwa CCM ni chama kinachoendekeza mambo ya 'ovyo' usishangae Job Ndugai akaukwaa Uspika licha ya kuwa sasa angestahili kuwa jela badala ya kuitwa Mheshimiwa Mbunge, kama serikali ya CCM ingekuwa inazingatia utawala wa sheria badala ya mtindo inaotumia wa kuwafanya wateule wachache ndani ya nchi kuwa UNTOUCHABLES na kuwa above the law.
 
Weka ushahidi wa tuhuma zako hapa. Kati ya vitu ambavyo vilinichekesha kwenye huu uchaguzi mkuu ni pale ambao niliona mgombea wa chama tawala anakemea ufisadi na kuonyesha kuuchukia hadi kusema akishinda urais ataanzisha Mahakama za majizi na mafisadi...lakini upande wa pili wa wapinzani....tangu kampeni zianze hadi zinamalizika...neno ufisadi, rushwa na wizi hayakutajwa kabisaaaaa. Hii ilinichekesha sana. Only in Tanzania upinzani unaogopa kutaja neno 'ufisadi'.

ushahidi nyumba alompa hawara pale ubungo kwani uongo?nyumba zaidi ya 20 alizojenga chato je?kebbys hotel je!!! yote tisa kivuko kipya_kibovu cha bgm posta tena kwa bei ya mara mbili ya kivuko kipya,acha ujinga huyu hafai tu ila akili za watanzania zilimpa urais kijingajinga
 
Mkuu hakuna ufisadi hapa nchini unao iweka ccm pembeni haupo kabisa, kuushughulikia ufisadi na kuutaja ni mambo mawili tofauti. Walio makini wanasubiri utekelezaji ndo wafurahi,
 
Huyu ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge la Katiba na Mshauri wa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.

Kuna baadhi ya watu wameshangaa kusikia akipitishwa na Kamati Kuu ya CCM kama mmoja wa wanaCCM watatu watakaopigiwa kura na wabunge wa CCM. Ni watu wachache watakuwa waliamini kama anaweza kupitishwa kwenye tatu bora hasa walipolinganisha na majina ya wanaCCM wengine waliochukua fomu.

Kile alichokifanya Dk. Tulia mpaka kufika kwenye tatu bora hakina tofauti na kile alikifanya Dk. Magufuli mpaka kufika kwenye tatu bora ya CCM katika tiketi ya Urais wa Tanzania.

Kuna uwezekano mkubwa kuna mikono ya ''kitengo'' cha CCM/Serikali katika safari ya Dk. Tulia Ackson kama ilivyokuwa katika safari ya Rais Magufuli. Watu wa ''kitengo'' kwa sasa wanataka kuhakikisha hakuna makundi ambayo ni chanzo cha kukidhoofisha chama na serikali kama ilivyokuwa katika utawala wa Rais Kikwete.

Ameenda kimya kimya kuchukua fomu za kugombea Uspika kama alivyofanya Dk. Magufuli wakati akichukua fomu za Urais.

Dk. Tulia alikataa kuongea na waandishi wa habari kabla na baada ya kuchukua fomu pamoja na waandishi wa habari kusisitiza aongee nao hata machache baada ya kuchukua fomu. Hata Dk. Magufuli alikataa kuongea na waandishi wa habari kabla na baada ya kuchukua fomu ya Urais.

Hana makundi ndani ya CCM ukilinganisha na wagombea wengine kama alivyokuwa Rais Magufuli wakati wa mchakato wa Urais.

Dk. Tulia alionekana kuwa cool, calm, and collected katika zoezi zima la mchakato wa kumpata Spika pamoja na kuwa ''CCM outsider'' ukilinganisha na wanaCCM wengine waliochukua fomu.

Kwa tell-tale signs kama hizi siwezi kushangaa kusikia amekuwa Spika wa Bunge la Tanzania.

Wahenga walisema Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama!

tulia%2Backson.jpg

Dk. Tulia Ackson akitoa maelezo kuhusu Kanuni za Bunge Maalum wakati wa bunge la Katiba Mpya.
 
Ndugai ndio spika wa bunge la 11..... Mimi ni mbunge na nakwambia huyo dada wako akishinda walahi naacha ubunge....
 
Dkt Magufuli uwa hana timu. Yeye ufanya kazi na yoyote yule ambae ni msafi kwa maana hana ufisadi na wizi.Hivyo katika hao watatu atafanya kazi na yeyote yule. Makundi na timu sio hulka ya Dkt Magufuli.

Lakini tufanye stori iwe fupi, spika ni Job Ndungai. Wabunge wengi wa CCM wanamkubali Job Ndungai.

Kisa cha kumkubali hiki hapa:

Pamoja na kwamba kwa sasa hakuna spika, ila aliyekuwa naibu wa spika (ambae ni Job Ndungai) ushirikiana na katibu wa Bunge kufanya maandalizi ya wabunge wapya mjengoni. Ndungai kaifanya hii kazi usiku na mchana tangu Novemba 6 huko. Kwa ufupi, tayari ana kura nyingi za wabunge wa CCM.

Hivyo basi, msipoteze muda kufanya mjadala kuhusu hili la uspika. Ni Ndungai tu. Labda mjadala uhamie kwa nani atakuwa waziri mkuu wa JMT.

#NdungaiForSpeaker

Uko sahihi mkuu..... Ndugai atashinda tena kwa mbali sana sana
 
Ccm ina hazina ya vichwa.chadema viti maalum tu wanatoana roho
 
Una ushahidi gani kama akili za watanzania ndiyo zilizompa kula?
 
Ndugai ndio spika wa bunge la 11..... Mimi ni mbunge na nakwambia huyo dada wako akishinda walahi naacha ubunge....
Wewe ulikuwa unatuambia maneno kama haya wakati wa mafuriko na safari ya matumaini ya Lowassa!

Mfuriko na safari ya matumaini ya Lowassa imeishia Monduli!

Kitu gani ambacho kwa sasa utatuambia tukuamini kwenye kauli zako.

By the way, Kwa nini Ndugai anapigiwa debe na watu waliokuwa kwenye TimuLowassa au Ulipo Tupo?

I begins to smell a rat!
 
ushahidi nyumba alompa hawara pale ubungo kwani uongo?nyumba zaidi ya 20 alizojenga chato je?kebbys hotel je!!! yote tisa kivuko kipya_kibovu cha bgm posta tena kwa bei ya mara mbili ya kivuko kipya,acha ujinga huyu hafai tu ila akili za watanzania zilimpa urais kijingajinga

Mkuu watanzania hawakumpa, alipewa na timu ya uchakachuaji ya kina February wakishirikiana na Tume.
 
Back
Top Bottom