Ya Kikwete yanafurahisha

Ya Kikwete yanafurahisha

Kipindi cha kikwete kilikuwa cha wananchi kutafuta mitaji na kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatatoa ajira kwa wananchi mijini na vijijini.
Watu wengi waliweza kulima, kufuga na kujenga kwa urahisi tofauti na sasa ambapo kupata mtaji ni jambo gumu sana. Taifa ni lazima liwe na mahali pakuanzia. Shule, hospitali, vyuo, viwanda, bank, petrol station, vyombo vya habari, mabwa ya samaki na mashamba vilijengwa na kuajiri watu wengi sana.

Migogoro ya ardhi ilizuka kwakuwa kila MTU alitaka kulima, kufuga na kujenga. Haya yalikuwa mapinduzi makubwa sana kwa Taifa hili, asitokee MTU kumdhihaki JK.
mtizamo wako kwasie tulie kuwa tunafuata taratibu mambo hayakua rahisi kwetu. hata kodi za fremu majumba hazikua halisi. narudia tena wizi ulikua ndio ujanja
 
Alijitahidi sana, hakuwa na roho ya kisasi wala kutaka watu waishi kama mashetani. Kosa kubwa ni aliyetuletea badala yake
 
mtizamo wako kwasie tulie kuwa tunafuata taratibu mambo hayakua rahisi kwetu. hata kodi za fremu majumba hazikua halisi. narudia tena wizi ulikua ndio ujanja
Narudia tena, kipindi cha kikwete kilikuwa kipindi cha watanzania kutafuta mitaji ya uwekezaji. Kipindi cha Nyerere watanzania wengi kama sio wooote walikuwa masikini sana kuweza kuwekeza chochote kokote. Hata wazungu pia walikuwa na kipindi cha mpito cha wazungu kutafuta mitaji ya kuwekeza kwa njia ambazo sasa hivi hazikubaliki tena. Mfano, walitumia watumwa, kufanyisha kazi watu kwa masaa mengi hata watoto na kuvamia na kutawala mataifa mengine kama makoloni yao na kupora lasirimali zao.

Ukiwauliza Waganda watakwambia wao waliinuka kibiashara baada ya kuwafukuza wahindi wote na kupora mali zao. Kule Kenya wao hawakuwafukuza wakoloni waliowekeza Kenya na wazawa wachache walipora na kumiliki ardhi. Hapa kwetu wawekezaji walikuwa watanzania wenye asili ya Asia tu, wenyeji hatukua na mitaji hata ya kufugia kuku.

Hivyo, Watanzania wengi waliweza kupata mitaji kwa njia mbalimbali kipindi cha JK. Uwekezaji huo wa kipindi cha JK ndio vyanzo vya kodi katika awamu hii ya tano. Bila JK kuachia watu kutajirika na kuwekeza leo hii awamu ya tano isingekuwa na pahala pa kukusanya kodi. Mfano, Kodi ya majumba inayokusanywa awamu ya 5 ni nyumba zilizojengwa na watumishi wa serikali waliopata fedha kwa kuhudhuria mikutano, washa na makongamano na kupewa posho. Kodi za magari zinazotozwa na askari barabarani zinatokana na magari mengi yaliyonunuliwa na utoaji holela wa leseni za udereva wakati wa JK hivyo kusababisha madereva kufanya makosa mengi barabarani.
 
Trip za majuu kibao. Kuzid kupungua kwa tembo na wanyama wengine mbugani. Wazungu kujichotea zahabu kupitia mikataba na usimamiz feki. Watumishi wa uma kwenda majuu kuhuzuria semina wakati hiyo semina ingeweza fanyikia bagamoyo. .
 
Trip za majuu kibao. Kuzid kupungua kwa tembo na wanyama wengine mbugani. Wazungu kujichotea zahabu kupitia mikataba na usimamiz feki. Watumishi wa uma kwenda majuu kuhuzuria semina wakati hiyo semina ingeweza fanyikia bagamoyo. .
Umedanganywa. Exposure ni mtaji muhimu sana. Unapotoka nje ya nchi unafahamu mengi sana na kupata ujasiri wa Ku "think globally and act locally" yaani unaona nje wanafanya nini na kurudi nyumbani kuyatekeleza uliyoyaona nje.

Kwetu watu wengi wanakalia vigoda, sisi kwetu pekee ndio tulikuwa na viti vya mbao vya kukunya, mimi nilidhani kuwa sisi ndio wenye viti bora duniani lakini nilipokwenda sekondari nilikuta makochi nyumbani kwa mkuu Wa shule nikayashangaa.
 
Umedanganywa. Exposure ni mtaji muhimu sana. Unapotoka nje ya nchi unafahamu mengi sana na kupata ujasiri wa Ku "think globally and act locally" yaani unaona nje wanafanya nini na kurudi nyumbani kuyatekeleza uliyoyaona nje.

Kwetu watu wengi wanakalia vigoda, sisi kwetu pekee ndio tulikuwa na viti vya mbao vya kukunya, mimi nilidhani kuwa sisi ndio wenye viti bora duniani lakini nilipokwenda sekondari nilikuta makochi nyumbani kwa mkuu Wa shule nikayashangaa.

Exposure bila kujipanga ya nini? Mkienda huko wanaishia kufanya shopping,/ manunuzi na kushangaa shangaa tu. Hakuna hata moja wanalolileta kuboresha mahala pao pa kazi. Sasa si mgesomea hapa hapa?

Kufuja Hela tu
 
Namkumbuka kwa kujenga shule za kata + UDOM
UDOM sawa lakin mwasisi wa shule za kata ni Mkapa (akitekeleza matakwa ya IMF) na kwahiyo ndie anastahili heshima hiyo!

Hata hivyo, linapokuja shule za kata namheshimu sana JK kwa jinsi alivyohangaika kuhakikisha zinapata walimu wa kutosha!

Kwa upande wa walimu wa sanaa alifanikiwa sana lakini alikuja kukwama kwenye walimu wa sayansi ingawaje nako alihangaika sana lakini mazingira yalimkwamisha!

I believe, angekaa kwa miaka 5 zaidi; hata changamoto ya walimu wa sayansi angeitatua!!

JPM sasa... ingawaje ni ex-teacher lakini wala haonekani kujali suala la kuhakikisha shule za kata zinakuwa na walimu wa kutosga; hususani walimu wa sayansi!
 
Huyu hapa!
tapatalk_1505794429014.jpeg
 
Tatizo la village elder ni kua anataka kila kitu awe nacho yeye na aabudiwe mfano logic ya kupunguza mishahara iwiane na wengine bado yoote ni kuona watu wengine wanaliowa 40,000,000 kwa mwezi roho inamuuma sana yani
village elder
 
Kweli Kabisa, Ila Leo Hata Yeye Anajuta Mno, Akitazama Uchumi Alivyopambana Kuukuza Leo Unaporomoshwa Kwa Kasi Ya 4G Na Bwana Faru, Roho Inamuuma Sana, Anaona Ni Bora Ata Angemaliza Tofauti Yake Na Blaza Edo Mamvi Akamwachia Nchi Hii Miaka Mitatu Tungekuwa Mbali Mno. Ila Ndugu Yenu Anafurahia Tu Kariakoo Kudoda, Mabenki Kufungwa, Biashara Kufungwa, Mahoteli Anayafunga Tu Huku Anachelea, Fedha Inashuka Thamani Anataka Aprint Mpya Yan Duh. Kagame Katuloga Sisi
wia on ze raiti trak
 
Mimi ninamkubuka sana Rais mstahafu Mh. Jakaya kwa mambo mazuri kumi (10) yafuatayo:

1. Ustawi wa demokrasia
2. Barabara nyingi
3. Madaraja marefu yaliyoshindikana kule Kigamboni, Msata na Malagalasy
4. Jakaya Kikwete Hospitali ya Moyo
5. Mwendo kasi
6. Nyumba za wanajeshi
7. Gesi ya Mtwara
8. Upanuaji wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
9. Ndoto ya ujenzi wa flyovers Dar es Salaam.
10. Vikoba

Je, wewe unamkumbuka kwa mazuri yapi?
Mlisema kwa kejeli na dharau kubwa kwamba alikuwa dhaifu.Mnaweweseka nini saaa ,
 
1. Uungwana
2. Being charismatic
3. Utaalum wa kiswahili na matumizi ya tafsida ( yaani anakupiga dongo taaratib bila matusi makali makali)
4. Huduma za kibingwa za afya na mafunzo ya kibingwa
5. Umeme vijijini
6. Shule za kata
7. Stimulus package (aaaaaaaaaaah, daaah hapa mzee alitupiga, wanufaika moja kwa moja sikujua vigezo vyao. Maadamu mwangwi wa stimulation ulifika pengi kwa mzunguko basi rahaaaaaaa).
8. Mabillionyiiiii ya JK
9. Kilimo kwanza
10. Kuruhusu kashifa kubwa kubwa zichunguzwe na kujadiliwa... EPA, escrow, Richmond n.k
 
This is JPM time, Hapa Kazi Tu..!! Tuko busy na kazi
Enzi za JPM unafanya kazi na hela hupati. Waliojiajiri ndio wanateseka kabisa, TRA imewafilisi kwa Kofi. Wafanyabiashara wamefunga maduka. Taabu juu ya taabu.
Le probreme sur le probleme
 
Tanzania tuitoeni ccm madarakani hata term moja tu, watakapo rudi watakuwa wamejifunza mengi sana.
Hii ya kusema Jakaya sijui Magu tuna potea.
Tukiweza kuitoa CCM madarakani tutatengeneza upinzani wa kweli Tanzania
 
Back
Top Bottom