Ya kale dhahabu, tukumbushane

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,797
11,890
Kwa wale vijana wa zamani na wa zamani zaidi ambao bado tupo, ni vizuri kumshukuru Mungu kwa mambo mbali mbali. Hapa naomba tumshukuru Mungu kwa matukio yaliyotamba zamani zile katika kituo bora kilichojulkana kama Radio Tanzania Dare es Salaam. Ninaanza kutaja baadhi, wengine muongezee.

Kwa wale vijana wa sasa, kama una swali lolote ama unataka kujua historia fulani uliyogusiwa na babu yako ama uliwahi kuisikia katika vyanzo visivyo rasmi, unaweza kuuliza. Ninaomba wale wazee watoe ufafanuzi bora kabbisa kwa viana watakaokuwa na maswali.

1. Ngomba za mzee Moris Nyunyuso zilizopigwa kabla ya matangazo ya saa na kufuatiwa na taarifa ya habari.

2. Wimbo wa kipindi cha salam za wangonjwa. "Wakati umewadia wa salaam za wagonjwa Hospitalini, leo tunawapa pole. Ajuaye Bwana Mungu kwa Mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama...".

3. Wimbo wa mkulima " Eeh, wananchi Mkulima wa kisasa..."

4. Nyimbo za twist kama "Africa yote tunacheza twist".

5. John John mtoto mbaya, nilituma sukari akailamba.

6. Nyimbo za Patric Balisidya, kama wa Arusi ya Ndyanao na Saiba.

7. Nyimbo za Kikristo kutoka Sauti ya Ujerumani Cologne. kama Wanaokwenda kule kwenye mwezi wanatumia rocket zao; Wengine wamelala, wengine wanakesha leo kuna nini; ulioimbwa kwa rafudhi ya kimasai kabisa.

8. Nyimbo za kusifu mashirika ya umma kama TFA ni chombo chetu..

Wengine endelezeni!. Kama una ka clip ka wimbo ama tukio, tuwekee!.
 
Kwenye Hotel za enzi hizo ambazo kwa sasa zinaitwa migahawa, unakuta sehemu ya kunawia mikono ina taulo halijulikani originally lilikuja na rangi gani, siku wakisikia bwana afya anazuru maeneo hayo ndipo utaona kama lilikuwa na rangi fulani.
 
Ni bendi ipi ilipiga wimbo wa jioni njema?

Nakumbuka magari aina ya landrover yenye rangi ya khaki, mkuu wa wilaya landrover, mkuu wa mkoa landrover, waziri landrover!
Yaliheshimika nadhani kuliko V8 kwa sasa sababu yalikuwa machache, watu wengi hawakuwa na uwezo wa kuyanunua toauti na sasa.
 
Wakati ule ukitongoza msichana unaweza ukapita mwaka kabla hujampata kwasababu kuonana nae either upitepite karibu na nyumbani kwao ukimwona yuko nje umkonyeze na anaweza asije, au umwandikie barua uwape wadogo zake wampe au umvizie saa za kwenda kisimani au umvizie kanisani wakati wa kurudi, lakini siku hizi kwa kuwezeshwa na mawasiliano kama simu nusu saa ni kubwa umeshampata kila kitu hadi mchezo.
 
Nyama ya ng'ombe ilikua tamu kuliko sasa kwa sababu wanyama walikula majani halisi na si pumba.

Taalifa za kifo unaandika barua inasafilishwa na bus

Kupiga simu mpaka uende posta na usubili opareta akuunganishe,hiyo ni kwaa foreni

Gari imala na la kifahali ni LandRover 109

Magazeti makuuubwa ya Mzalendo yalishika chati

Mgambo akikukamata na boxi tu mkononi unashukiwa kua wewe ni muhujumu uchumi

Idadi ya raia wa Tanzania ilikua chache ikizidiwa hata na watu walioko mji mmoja tu wa New Delhi kule India kwa leo hii

Wali maharage ilikua chakula cha anasa na kizuri kwenye familia na ladha ya chakula cha zamani ilikua nzuri na tamu kuliko sasa

Ukivizia bus usafili toka sehemu A kwenda sehemu B itakua ni alfajili na bus linaweza likasikika linaunguruma lakini likakufikia hapo stand zaidi ya saa moja..Leyland bus

Wachawi walishika chati kuliko utandawazi

Dini ziliingia za kutoka kwa tusiowajua na kutufanya tusahau imani zetu
 
RTD waliburudisha na kuelimisha sana na kipindi cha saa 2:15 usiku cha mazungumzo baada ya habari. Ikisomwa na Suleiman hegga,salim s nkamba au selemani kumchaya. Pia kipindi cha mahoka kilibamba sana. Mahokaaaaa!
 
unaweza tongoza binti miezi kadhaa mpaka mwaka hujaambulia kitu wanawake walikuwa bidhb adimu sana
 
Jumamosi au jumapili ndio siku maalum ya ratiba ya wali. Bimkubwa anakomoa kama hujaoga.

weh! utanashati wa lkulazimishana...
 
Taarifa ya habari ilikuwa na mpangilio mzuri ikisomwa na akina Ahmed Jongo,Jacob Tesha,Abdul Ngalawa,Sara Dumba na wengineo wa aina hiyo.siku ya mechi ya simba na yanga kijiji kizima tulikusanyika kwa mwenyekiti..duh tumetoka mbali sanaa
 
Taarifa ya habari ilikuwa na mpangilio mzuri ikisomwa na akina Ahmed Jongo,Jacob Tesha,Abdul Ngalawa,Sara Dumba na wengineo wa aina hiyo.siku ya mechi ya simba na yanga kijiji kizima tulikusanyika kwa mwenyekiti..duh tumetoka mbali sanaa
 
Kwa hiyo tunakubali ya kale ni dhahabu! sasa kwa nini wasirejeshe vile vitu pendwa vya zamani kama togwa, zamani ukivaa nguo laini za kubana ziliitwa minyondo au chubana leo hii zinaitwa modo. Hivi na vitu ambavyo leo hii tunaviona si vizuri vitakuja kuwa bora au dhahabu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom