Baba Mkali
JF-Expert Member
- Feb 9, 2011
- 810
- 808
Nilikuwa nakuja kupost kuhusu hili tangazo,kumbe linawakera wengi. Nimesikitishwa sana na kituo kama ITV kuruhusu tangazo kama hili kurushwa hewani. Halina maadili hata kidogo, ni aibu umekaa na mama yako kisha linawekwa tangazo hilo, mbaya zaidi ni kuwa huwa ni katika taarifa ya habari ya saa mbili ambapo huwezi kuacha kuangalia. ITV naamini ina wahariri makini, nawaomba waliondoe haraka kwani wanajishushia hadhi.