Ya ITV & RFA NA TANGAZO LA KULAZIMISHA NGONO...

dah jana ndo nimeliona nilikua na aunt yangu,,,sikujisikia vizuri,na yeye mwenyewe aliguna....tena wameliweka wakati wa break ya taarifa ya habar,,,,thoz medi wapo kipesa kuliko maadili so TWENDE TU

Kama Aunt yako angekupa masomo juu ya mapenz ktk muda muwafaka,usingeshanga ila kwa vile100% ya watanzania wazaz hawana muda kuwaambia watoto wao juu ya mabadiliko ya tabia ktk miili yao watu tunaoneana aibu.
 
Tangazo hili kwa kweli linakera sana na hivi waandaaji wa matangazo ya namna hii hawajui maisha ya Watanzania kuwa vyombo vya habari kama tv tunaangalia kifamilia. Tangazo hili kwa kweli linaleta aibu walifute.

Hakuna cha aibu wala nini, utitiri wa matatizo ktk ndoa unasababishwa na kubakana ktk ndoa, wanaume wakitanzania hawajuwi kubembeleza hadi mwenz wake ajisikie ila wanalazimisha sm tm hata kwa maandiko, tusinyimane... Ujinga huu tunajenga taifa lisilo na ndoa madhubuti ila malalamiko ambayo mwisho wake kuvunjika ndoa.
 
Mimi jana nilikuwa na mzazi wangu asubuhi kwenye gari,hilo tangazo lilipowekwa ilikuwa aibu tupu,mamangu alikuwa anatafuta mlango wa kutokea.Aibu tupu!!!!!!!!!!!!!

Pole mkuu I can imagine the embarassement!
 
Hakuna cha aibu wala nini, utitiri wa matatizo ktk ndoa unasababishwa na kubakana ktk ndoa, wanaume wakitanzania hawajuwi kubembeleza hadi mwenz wake ajisikie ila wanalazimisha sm tm hata kwa maandiko, tusinyimane... Ujinga huu tunajenga taifa lisilo na ndoa madhubuti ila malalamiko ambayo mwisho wake kuvunjika ndoa.

Tushavizoea vichwa kama chako,kila sehemu unajenga hoja! Shibuda nini??
 
Moja ya udhaifu wa vyombo vyetu tunavyovitegemea ndio kama hayo,Tangazo kama lile unakubali vp lilushwe hewani unatengenza kizazi cha aina gani,sielew hawa watu wanafanya kazi gani,yaani ni upuuzi mtupu.sidhani kama kuna mtu analipenda lile tangazo.
 
Ukweli ni kwamba hili tangazo linakera sana, siku ya kwanza nimeliona ni juzi kupitia ITV kibaya zaid nilikuwa na baba mkwe sebulen tunasubiri kuangalia habari, wanangu wote wapo jaman nilishtukia naamka na kuondoka hapo, sasa kasheshe wanangu wakaanza kulirudia kwa maigizo hali wanacheka nilitamani ardhi ipasuke niingie lol ........... aibu jamani. Nashukuru mungu baba mke aliwakaripia wajukuu zake mwenyewe manake nilijua nikiwaite angehisi nawaitia hilo so nilitegemea mUngu anitumie msaada wake tu.
 
hivi vitu vya misaada vina matatizo sana,maana lile tangazo ni msaada wa wamarekani,mimi ndo maana nauchukia umaskini
 
Ni kweli tangazo halijatulia sana kivile lakini kwa mtizamo wangu nadhani liko poa,kwa kuwa nao itv na rfa wanacho kitengo cha kusort kabla hawajaachia hewani tangazo.sec kubwa ujumbe unafikia walengwa ndo maana hata wewe umelisikia.kwa upande wa maadili ni issue pana kwa kuwa sisi wenyewe hatujitambui..kimtizamo,kimavazi e.g issue ya vimini kwa kina dada..vijana kuvaa kata kei..nadhani tungeanza kukemea vitu kama hivyo.huko juu ingekua rahisi kwa kuwa kuna mamlaka zenye wajibu hou.thanks!
 
Lakini jaman twende mbele turudi nyuma,hili tangazo linauwalisia wa mambo wanayo tendeana wana ndoa,so kwa vile wa tz hatupend kuambiwa kweli basi hii ni nongwa....

.
Wengi wa wale wanaojifanya watetezi wa haki za wana ndoa ni watu ambao hawana ndoa na kwa hakika ni kunguru ambao hawafugikiki ima ni kina mama au kina baba.
.
 
Tangazo hili mimi linanikera sana, nadhani ifike wakati watanzania tuwajibishane hawa TCRA kazi yao ni ipi? hao wenye Television pia hawangalii ni kipi kirushwe kwenye hadhira? hawajui kama kuna watoto wanaokua na wenye udadisi wa kujua kila waonacho ama kusikia?
 
Moja ya udhaifu wa vyombo vyetu tunavyovitegemea ndio kama hayo,Tangazo kama lile unakubali vp lilushwe hewani unatengenza kizazi cha aina gani,sielew hawa watu wanafanya kazi gani,yaani ni upuuzi mtupu.sidhani kama kuna mtu analipenda lile tangazo.

.
Ni freemasons hao. Wanakiandaa kizazi cha kitanzania kisaikolojia kabla ya kuanza kujadili suala la uhahali wa ndoa za jinsia moja.
.
 
Tunaomba mtudokezee kidogo wengne hadi sasa hatujalisikia ng hatuna fursa ya kulisikia lakin tukijua nn chaendelea nchin kwetu ni vzur ndo mana hatubanduki jamvini
 
Umaskini unatupeleka pabaya maana ayo matangazo ni kwa hisani ya wamarekani.Kwa ujumla ninakosa amani na vyombo vyetu vya habari ninapokuwa na watoto au watu ninaoheshimiana nao maana sijui nini kitakuja baada ya muda(unpredictable).
 
tangazo la kishenz kupata kutokea,alafu linawekwa wakati wa taarifa ya habari,kwakweli litawatia aibu wengi!
 
Back
Top Bottom