X wangu kaniambia nimemroga!

X wangu kaniambia nimemroga!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,066
Huyu alikuwa mchumba wangu ambaye nilimpenda sana na tulikubaliana kuoana. Nilipatwa na matatizo njiani mwenzangu akanambia anaolewa na mtu mwingine (tulikuwa tunaishi mikoa tofauti). Niliumia sana na kutokana na hasira nikamwambia `Tutaona kama utaishi na huyo mwanaume.' Toka hapo sijawahi kuwasiliana naye tena!

Siku za karibuni alinitumia message kwamba anaomba kuongea na mimi, nikamtajia muda ambao ntakuwa free.
Muda huo akanipigia simu na kuanza kunilaumu `@nyalotsi kwanini umenifanyia hivi?'
Nikamuuliza, nimfenyaje?(huku nikiwa na mshangao)
`Umeniroga kila nikipata mimba inatoka, tafadhali sana nisamehe kama nilikukosea! Familia yangu itavurugika.'

Nilikata simu na kuanza kutafakari mambo mengi sana. Ina maana huyu dada kaniona mi mchawi? Mbona hata mizizi ya dawa za kawaida tu siifahamu? Hii laana gani tena? Baadaye nikakumbuka niliwahi kumtishia kwamba hataishi kwa amani na mumewe. Nikampigia simu na kumhakikishia kwamba siwezi kufanya kitu hiyo na wala sio muumini wa mambo hayo.
Nikamshauri pia waende na mumewe hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kiafya na wataalamu.!

Kweli duniani kuna mambo!!
 
Hivi unajua maneno yanaumba? Hivi unajua shetani anatumia maneno ya binadamu kupitishia laana zake? Inawezekana havihusiani but inawezekana pia laana uliyoapiza kwake ndio inamuathiri...
Nakushauri tu ufanye utaratibu wa kuifuta hiyo laana kwa mwenzio. .. msaidie kwa hilo
 
coincidence! it happens.
 
Anaifutaje sasa?!!! au apige mashine?!!...,lol
 
Ndio umemloga kweli kwani maneno huumba.Mkuu acha uchawi kwa jina la YESU! Vipi na kuruka na ungo unaweza? kwa maana nataka niende London.
 
Kiukweli ulimlaani japo inaweza isiwe sababu ya masahibu yake. Muambie umemsamehe kabisa kwa kukuumiza, na utubu kwa Mungu na kukiri kwa sala kuwa umemsamehe. Hii mammbo ya kuumiza nyoyo za watu can be haunting.
 
Hivi unajua maneno yanaumba? Hivi unajua shetani anatumia maneno ya binadamu kupitishia laana zake? Inawezekana havihusiani but inawezekana pia laana uliyoapiza kwake ndio inamuathiri...
Nakushauri tu ufanye utaratibu wa kuifuta hiyo laana kwa mwenzio. .. msaidie kwa hilo

Well said, ila ni wachache wanaojua hili.
 
So Maneno ni uchawi?interesting ngoja waje waumini wa weak minds msikie

Strong mind zikoje? Zisizoamini uwepo wa supernatural power (Mungu na shetani).

Haya sisi wa weak mind tunaamini kuna power kwenye kila neno litamkwalo, na ukitoa neno la baraka Roho wa Mungu hukamilisha hiyo baraka na ukitoa la laana roho ya muovu hukamilisha hiyo laana.

Ingawa kwa case hii huwezi sema kwa uhakika kama kauli ya mkuu ndio pekee imesababisha hayo. Yaweza kuwa one of the reason au hata isiwe hiyo. Hata wa strong mind (scientist) huwa hawezi sema moja kwa moja ndio maana huwa wana broad spectrum antibiotic.
 
Ulimi unaumba!!
Tuwe tunafikiri mara mbili kabla ya kuropoka,
 
pole mwaya then hata usijali kwakuwa huhusiki,ni imani yake mwenyewe ,lakini kweli maneno uumba nakumbuka kuna siku nilikuwa nimekaa na marehemu rafiki yangu kipenzi wakati tunapiga stori nikamwambia shemeji yako anaumwa sana,akacheka akanitania eti na atakufa huyo..nikamwambia thubutu utatangulia wewe utamuacha,haikupita wiki akafariki mamu wangu,na baada ya miezi kadhaa na mme nae akafata!!. nawakumbuka sana.
 
^^
Siku zote maneno kama haya ''tutaona'' si mazuri
Vinginevyo unaweza kutamka umemsamehe na aende hospitali kwa uchunguzi wa kitabibu
^^
 
yaani wewee..! jana usiku umepiga vingapi tena?!

Jana ndoto ilikuwa tofauti kidogo ila nimepata vitatu! niliota nacheza mziki wa ndombolo na mom fay akawa anakatika sana... nikashangaa nimelegea mara 3.nitafsirie ndoto hii tafadhali.
 
maneno ambayo hutakiwi kumwambia mpenzi wako mnapoachana kwa usalama wako tu
1.utaona wewe

2.nitakufundisha kitu

3.penzi langu haliwezi kupotea bure

4.huwezi kunipotezea mda lazima nikuoneshe

5.si unaniona mjinga poa subili
6.ipo siku ntalipa kisasi
 
una "natural anciety witches in your body" "mtaje jina then zungumza kwa mkazo "fulani" sasa umepona"ninakuachia na sasa upo huru zaa watoto salama
 
Back
Top Bottom