X-girlfriend anavuruga ndoa yangu

X-girlfriend anavuruga ndoa yangu

Tatizo kubwa ni kwamba tunaishi mtaa mmoja.

Alipata bwana mpya akaniacha kwa matusi na kejeli. Nami nikapata mpenzi alipojua akaanza kumlisha maneno mpenzi wangu kwamba mimi sifai ndo sababu aliniacha. Mpenzi wangu aliponieleza iliniuma ila nikajitetea kwamba anichunguze kama aliyoambiwa ni kweli au la.

Tuliendelea tukawa wachumba, na mwishowe tukafunga ndoa. Lakini huyu x bado hajaridhika,akikutana mtaani na mke wangu anampa mabango,mara atakuacha,mara hafai.

Alipoona mbinu hazijafaulu anaanza kumweleza kuwa eti ninamtaka kimapenzi. Ajabu ni kwamba huyu x naye ana bwana wake.
Hili limemyumbisha mke wangu sana.

Ninajuta kujenga mtaa huu alipo huyu x, mpaka natamani niuze nyumba tuhamie eneo tofauti. Lakini shughuli zangu ziko hapa.

Wakuu hii hali iliwahi kukukuta,ulifanyaje?
Uzuri ushasema hata mke wako alikuw a anajua kuwa ni x-wako, kwa hiyo cha msingi zbeni masikio endeleeni mbele na ndoa yenu ya x-wako yafanyeni kelele za mbwa koko tu zisiwayumbishe
 
Yaani unasema unataka uhame nyumba uliyojenga mwenyewe kwa pesa zako kisa vijimaneno vya dear ex, na unakuta ni kabinti flani hivii kimbaumbau hakafiki hata 50 Kgs.!

Niqqah' are you serious.??

Amin, Amin.! Nawaambia, kwa mtindo huu wa maisha, wanaume mtaendelea kuteswa sana na jinsia Ke,
Duuuh...haya bhan
 
Kunawl watu wana vipaji vya kuvumilia ujinga
 
Wanaume wa musoma tutaendelea kubaki na ushujaa wetu na hakuna watakaotuweza kwa ushujaa.unashindwa kumfuata bwana wake na kumchana ukweli upumbavu wa mke wake? Ww mwanaume wa wapi
 
Tatizo kubwa ni kwamba tunaishi mtaa mmoja.

Alipata bwana mpya akaniacha kwa matusi na kejeli. Nami nikapata mpenzi alipojua akaanza kumlisha maneno mpenzi wangu kwamba mimi sifai ndo sababu aliniacha. Mpenzi wangu aliponieleza iliniuma ila nikajitetea kwamba anichunguze kama aliyoambiwa ni kweli au la.

Tuliendelea tukawa wachumba, na mwishowe tukafunga ndoa. Lakini huyu x bado hajaridhika,akikutana mtaani na mke wangu anampa mabango,mara atakuacha,mara hafai.

Alipoona mbinu hazijafaulu anaanza kumweleza kuwa eti ninamtaka kimapenzi. Ajabu ni kwamba huyu x naye ana bwana wake.
Hili limemyumbisha mke wangu sana.

Ninajuta kujenga mtaa huu alipo huyu x, mpaka natamani niuze nyumba tuhamie eneo tofauti. Lakini shughuli zangu ziko hapa.

Wakuu hii hali iliwahi kukukuta,ulifanyaje?
we mwambie humjui, mkane
 
Sikia leta namba ya huyo Ex wako...hana kazi za kufanya nitampa hatokaa akusumbue tena
 
Inaonekana uyo demu ambae umemuacha anaonekana huko alipoenda hafuraii mapenzi anaonekana anateseka na kuisoma no balabala sasa wewe siku akizingua mtie vitasa
 
mkuu mbona kutatua hili tatizo ni rahisi sanaa? unaweza mfuata mme wake ukaongea nae kiuana ume yakaisha pia unaweza mkalisha mke wako na kumwambia asijempa nafasi ya kumsikiliza kwa lolote maana inaelekea wanakaa wanapiga stori ama anamsikiliza ujinga wake.

kuhama nyumba kisa x ni udhaifu ulopitiliza
 
Uko too soft sana kijana

Muite mbele ya mkeo mchane live

Otherwise Ni chai maharage
 
Kwani matokeo ya ule uchunguzi ulimwambia mkeo akuchunguze yalionyesha nini?

Maana ulimwambia naye akuchunguze ili ajilidgishe na hayo maneno,sasa mwambie akupe matokeo ya uchunguzi wake.kama yapo vibaya basi muombe radhi na weka mpango wa utekelezaji wa kuyarekebisha mapungufu.

Vingine vyote ulivyouliza hapa ni kelele tuuu
 
Back
Top Bottom