Grand Canyon
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 547
- 1,193
Tatizo kubwa ni kwamba tunaishi mtaa mmoja.
Alipata bwana mpya akaniacha kwa matusi na kejeli. Nami nikapata mpenzi alipojua akaanza kumlisha maneno mpenzi wangu kwamba mimi sifai ndo sababu aliniacha. Mpenzi wangu aliponieleza iliniuma ila nikajitetea kwamba anichunguze kama aliyoambiwa ni kweli au la.
Tuliendelea tukawa wachumba, na mwishowe tukafunga ndoa. Lakini huyu x bado hajaridhika,akikutana mtaani na mke wangu anampa mabango,mara atakuacha,mara hafai.
Alipoona mbinu hazijafaulu anaanza kumweleza kuwa eti ninamtaka kimapenzi. Ajabu ni kwamba huyu x naye ana bwana wake.
Hili limemyumbisha mke wangu sana.
Ninajuta kujenga mtaa huu alipo huyu x, mpaka natamani niuze nyumba tuhamie eneo tofauti. Lakini shughuli zangu ziko hapa.
Wakuu hii hali iliwahi kukukuta,ulifanyaje?