Siemens c28 aka twanga pepeta ndo likuwa simu yangu ya mwanzo, hahaha huwezi amini ilipotea mitaa ya Posta nikiwa na sweet heart wangu ambye sasa ndo shemeji yenu tumetoka Sinza naenda chukua mpunga Standard chartered wa kula bata siku hiyo, hee si ikateleza mfukoni ikadondokea kwenye kiti mwenyewe sina habari, ndo ikawa mwisho wa Twanga yangu.
Hiyo Namba nne alikuwa nayo late bro wangu, mwenyewe alikuwa anaiweka kwenye kipochi chake anachomeka kwenye mkanda kiunoni utampenda. alipofariki nikawa naitumia, tatizo kubwa ya simu za Ericsson zina matatizo sana ya network, siku moja na shemeji yenu wakati wa uchumba, mie bado naishi na bro wangu mkubwa km kawaida yetu tukapanga tukutane pale Sinza Kamanyola hotel flani matata hivi, mzee nimewahi niko inside km dk ishirini kumbe na yeye kaja ananipigia hanipati, mie simu yangu ukiiangalia inaoneka iko vizuri tu muda unakwenda nikaanza kulaani, kumbe na yeye yupo nje ananilaani, nikatoka nje wapi simu inaonekana iko fiti, baada ya ssaa nzima si nikatoka zangu na hasira vibaya mnoo, kumbe na yeye ana hasiza zaidi ya kwangu. baada ya km nusu saa nipo migomigo si sms zikaanza kuingia ni matusi mtindo mmoja. nampigia alipopokea simu tu na lawama juu wewe ulikuwa na baamedi kwani sijui hahahahaha dah iliniletea msala hiyo simu sisahau!!