Wote tuseme Ajali sasa basi, zinatosha

Wote tuseme Ajali sasa basi, zinatosha

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,939
Reaction score
600
Ifike mahali jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani kianzishe utaratibu wakusindikiza mabasi yote ya abiria kwa kupokezana kama ile staili ya mwenge wa Uhuru. Askari wa DSM wasindikize hadi pwani. Pwani wasindikize hadi Moro, tanga etc. Kutoka hapo wapokee wengine kama ni iringa, Dodoma, singida na kwingineko. Kama kuna garama zozote kwa askari zilipwe na wenye mabasi, serikali isigaramie chochote zaidi yakujitolea askari wake. Askari hawa watawamonitor madereva kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho. Naamini hii itasaidia kupunguza ajali.
 
Unaambiwa tatizo ni mashimo ya barabarani. Nayo hayo unataka kila basi limbebe Magufuri?
 
Hata wakisindikiza itafika mahali watazoeana gar ya askar na bus watakua wanafanya Ligi nana fike kabla ya mwenzie Moro msavu au Pia watazoeana wataanza kupeana buku buku anasindikiza mpka kibamba manina chezea Bongo
 
Hata wakisindikiza itafika mahali watazoeana gar ya askar na bus watakua wanafanya Ligi nana fike kabla ya mwenzie Moro msavu au Pia watazoeana wataanza kupeana buku buku anasindikiza mpka kibamba manina chezea Bongo
Unashauri tufanye nini?
 
Ajali imetokea ndio.tunaambiwa gr lilikuwa linaenda kwa mwendo kas ujinga tu uzenbe unawahusu hata abiria
 
Kuna barabara (vipande) ambazo kwa kweli ni mbaya na hazifai hata kupitishia magogo achilia mbali abiria.
Barabara ya kutoka Kibaha hadi njia panda ya Chalinze maarufu kama eneo la Ruvu! utashangaa kuwa ni vipi wanaruhusu iendelee kutumika!

Kuna eneo la kutoka Mikumi hadi unaiacha Kitonga.Hili eneo ni miongoni mwa maeneo yaliyogharimu sana maisha ya watu ila seeikali ipo kama gogo!!

Kuna eneo la Mafinga.Kwanza ni msituni pili barabara ina mashimo sana na inateleza sana.Hili eneo mtu unashangaa ni vipi linaendelea kutumika.

Kuna Kilima cha Wami, Kilima cha kutokea Mbarali kuelekea Uyole na Eneo la Songea napo ni majanga matupu! Barabara ni mbovu sana!!
Serikali inapaswa ilazimishwe kuyafanyia kazi maeneo yote hatarishi maana ni mengi sana!! Wawe na mpango wa dharura kukarabati haya maeneo!
 
Kule Songea wakati fulani walikua na utaratibu kama huu wa kusindikiza mabasi Songea Njombe, Njombe Songea.

Bahati Mbaya ilitokea ajali akafa askari msindikizaji peke yake, maana alikua anakaa kiti cha staff pale mbele.

Toka hapo wakasitisha huo utaratibu.

Lakini kwa ajali ya hiyo Basi sio sababu ya mbio, yeye alisimama kwenye site yake mwenye lori ndio akayumba na kumfuata hukohuko.

Barabara ya Mafinga Mbeya inamashimo mengi ya hapa na pale, alivyopita Pinda walimwagia vumbi tu alivyoondoka mashimo yakarudi vilevile.

Serikali nayo inahusika kwa namna nyingine.
 
Ushauri wako Tafadhali.
Marekebisho ya barabara mara kwa mara. Madereva wa mabasi waache viroba na bangi. Fain na adhabu za waendesha vyombo vya abiria iwe mara mbili ya madereva wa kawaida. Kama leseni za ni exeptional basi na adhabu ziwe vilevile
 
Wa kusema ni nani, watua wemekufa 47 Kahama nchi kimya, Wakafa 43 Iringa nchi kimya, Mbung mmoja akifa eti nchi ikatetemeka? Albino wanakwata na kuuwawa Kimya! Kweli Kweli Kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Marekebisho ya barabara mara kwa mara. Madereva wa mabasi waache viroba na bangi. Fain na adhabu za waendesha vyombo vya abiria iwe mara mbili ya madereva wa kawaida. Kama leseni za ni exeptional basi na adhabu ziwe vilevile
OK, traffic wamekuelewa.
Lakini naomba niongezee neno moja hapo kwenye faini. Unaonaje kama huyu traffic msindikizaji akawa anakeep records za nakosa yote tangu mwanzo wa safari hadi mwisho na baada yahapo anamwandikia faini zake zote hata zikiwa 50 kwa safari yote. Hii intafanya dereva awe makini 100%.
 
business as usual hili litapita tu



ccm wamechoka na organ zote ziko hoi
 
Unaambiwa tatizo ni mashimo ya barabarani. Nayo hayo unataka kila basi limbebe Magufuri?
Kwa mawazo ya mleta mada ni wazi kama wengi wanafikiri hivi bado tutaendelea kuteketea na ajali.
Hebu angalia BBC wamejithidi kuilezea hii habari kwenye ukurasa wao mbele kabisa na wamefafanua vizuri kile kinachodhaniwa kuwa ni chanzo cha ajali.
Wanaoijua hiyo sehemu wanasema hilo shimo sio la jana wala juzi bali ni la muda mrefu na madereva wengi wameshalkipigia kelele lakini kama ilivyo kwa Tanzania mamlaka husika inasubiri wafe walau watu 40 kama hivi alafu ndipo chochote kifanyike.
Ni matumaini yangu kuwa zinapopotea roho zaidi ya 40 basi walau mtu mmoja.
Tanzania bus crash leaves dozens dead in Iringa

_81577824_tanzania.jpg
The injured have been transferred to hospital
Continue reading the main story Related Stories



Two lorries and a bus have collided in Tanzania's highland region of Iringa, killing 41 people, police say.
The accident happened after a lorry driver swerved to avoid a pothole, the regional commander told the BBC.
One of the lorries' containers fell on to the bus that had been heading to Dar es Salaam, crushing many passengers to death, he said.
Traffic accidents are common in Tanzania, where the state of the roads and the vehicles is often poor.
_81577994_tanzania.jpg
The crash happened next to this pot hole
President Jakaya Kikwete released a statement saying: "This gives cause for great mourning. The entire country has been shaken," the AFP news agency reports.
Iringa regional police commander Ramadhan Mungi said a further 23 passengers had been seriously injured and had been taken to Mafinga hospital.
All the bodies trapped between the lorries had been removed, he said.
The bus had been travelling from the south-western town of Mbeya to the commercial capital.
_81573079_tanzania_mbeya_iringa_464.png

 
hivi si kuna vile vibao vya kulimit speed sasa najiuliza dere akishakipita kile si nikujiachia tu,tena chanzo cha ajali nyingi ni spidi
 
Tatizo tunaona jambo moja tu, mwendo kasi lakini hatuangalii mambo mengine. Barabara ikiwa nzuri na migongo yenye upana wa kutosha inapunguza ajali. Barabara ya kutoka Chalinze kwenda Morogoro ni busy sana lakini ina ajali chache sana hasa hasa za mabasi. Ni nzuri, ni pana kuna mgongo wa kutosha ku-avoid head on collisions hata mtu akiovertake vibaya.

We need better infrastructure, hii ajali hata ingetokea kwenye spidi ya serikali i.e 80Kph bado kungekuwa na maafa tu.
 
Ifike mahali jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani kianzishe utaratibu wakusindikiza mabasi yote ya abiria kwa kupokezana kama ile staili ya mwenge wa Uhuru. Askari wa DSM wasindikize hadi pwani. Pwani wasindikize hadi Moro, tanga etc. Kutoka hapo wapokee wengine kama ni iringa, Dodoma, singida na kwingineko. Kama kuna garama zozote kwa askari zilipwe na wenye mabasi, serikali isigaramie chochote zaidi yakujitolea askari wake. Askari hawa watawamonitor madereva kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho. Naamini hii itasaidia kupunguza ajali.

Njia rahisi ni kuwa pindi inapotokea ajali... Wahusika wanaohusiana na masuala ya usalama wa huo mkoa lipotokea ajali wanatakiwa kuwajibishwa kwa kushushwa chini kicheo na kupewa adhabu nyingine stahiki kwa njia hii watakuwa makini zaidi uzembe unaosababisha ajali usitokee tena
 
wanajamvi kumekuwa na mawazo mengi ya kutafuta ufumbuzi wa ajali zinazotokea kila siku nchini kwetu. Nimekuwa kila mara nikishauri kutokana na uzoefu wangu wakusafiri kama ifuatavyo:-
1.Abiria tuwe wakwanza kumuomba dereva apunguze mwendo tunapo ona basi linakwenda mwendo kasi na iwapo dereva hakusikilizi tutowe taarifa kwa askari wa usalama barabarani ili kuchukuwa hatua za kisheria kwa madereva wa mabasi yaendayo kasi.Mimi nimekwisha fanya hivyo na nimepata msaada japo dereva na baadhi wa abiria unapofanya hivyo huwa wanakasirika.
2.Kikosi cha usalama barabarani waanze ule utaratibu wa kuondoa pointi kwa madereva wanaofanya makosa ya usalama barabarani na hili lilikuwa ndiyo dhumuni moja wapo la kuanzisha kwa hizi leseni za kielektroni za sasa, baada ya kukutwa na kosa na kulipa faini haitoshi hatua ya pili pointi zitolewe.
3.Askari wa usalama barabarani kusindikiza mabasi nakumbuka Mkoa wa Mbeya walikuwa na utaratibu huu askari anapanda basi la kwanza kuondoka, sijui kama mpango huu bado unaendelea.
4.kianzishe kitu kinaitwa Spidi ya magari ya kitaifa (National Speed Limit) mfano gari zisikimbie zaidi ya spidi120,kwa sasa spidi baada ya kuvuka eneo la mji kila dereva anaedesha spidi awezayo!ukiwa kwenye eneo la makazi ya watu au mji dereva ana amrishwa aendeshe spidi 30.
 
hivi si kuna vile vibao vya kulimit speed sasa najiuliza dere akishakipita kile si nikujiachia tu,tena chanzo cha ajali nyingi ni spidi

Mkuu ni kweli baada ya speed limit ni kujiachia hakuna ukomo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom