Wote tuseme Ajali sasa basi, zinatosha

Wote tuseme Ajali sasa basi, zinatosha

Mara nyingi sipendi kuwalaumu madereva ila katika hili kwa vyovyote dereva wa bas hakuchukua tahadhar ya kutosha . Kwa mtazamo wangu ajali hii ilikuwa hailwepeki lakin dereva angeweza kupunguza madhara yaliyotokea. Jambo jingine magar yanayotumika tanzania mengi hayana hadh ya kubeba abiria kabisa nina amin gari ile ingekuwa Yutong au Zoutong new model madhara yasingekuwa haya lazima ajali ingezuilika. Ni kweli kuna shimo lakin kumbuka dereva analijua shimo hilo anapita kila siku. Pia kwa mtazamo wangu naona kama alikuwa na speed kubwa sana hiyo ingemsaidia dereva kuepuka kugongana uso kwa uso japo ajali igetokea madhara yangepungua kwa hiyo nadhani pia huyu dereva alikuwa na matatizo ya akili kidogo(punic) . Ushaur wangu kwa madereva wenzangu unapokimbiza gar jaribu kuwaza hiv ikitokea dharura ndani ya mita hamsin naweza kusimama au kuepuka? Kabla ya kujijibu swali hilo angalia uwezo wa gar lako. Kwa wale wanaoendesha bus za kichina inawezekana vip kwa wale wa scania na nissan? Kwa malor mwenye Man ,iveco au howo anaweza mwenye scania jitafakari. Sipingi mwendo mkal ila lazima dereva ujue unachofanya. Pamoja na mashimo msimamo wangu dereva alifanya uzembe asingeepuka ajal kama lor lilimfata lakin madhara yangepungua sanaaa.
 
tuanze kwa kuangalia chanzo cha hizo ajali kisha turekebishe....na hii dhana ya kwamba mwendo kasi ndio chanzo cha ajali em tuiangalie kwa jicho la tofauti....maana kama ni hvyo kwanini hayo magari yanakuja kutoka kiwandani yakiwa na uwezo wa hzo spidi kama zinaua??
 
Njia mojawapo ni kuimarisha usafiri wa reli. Treni moja ina uwezo wa kuvuta mabehewa 40 au zaidi hiyo ni sawa na malori 40 au mabasi 80 kwani behewa moja lina uwezo wa kuchukua zaidi ya abiria 80. Abiria awe na uchaguzi akipanda treni atakuwa na uhakika 99% atafika salama, aamue mwenyewe kupanda basi (ikiwa anaona ana haraka). Kwa sasa abiria hana uchaguzi kwa mfano DSM - Arusha vinginevyo apande ndege na ni watz wangapi wana uwezo huo? Wa Tz wengi watapanda treni kwani bei ni rahisi na hata kusafirisha mizigo ikiwa urasimu utaondolewa. Kumbuka Ajali nyingi zinatokea kwa mabasi yanayokwenda safari ndefu.
 
Tatizo jingine wanasiasa wanapendelea ujenzi na sio matengenezo ya barabara. Hii ni kwasababu ujenzi (road development) unasaidia kupata kura wakati wa uchaguzi. Matengenezo (road maintenance) haitiliwi mkazo kwakuwa haileti kura nyingi.

Sasa nchi yetu imekuwa ikifungua barabara mpya na kusahau matengenezo ya zile za zamani hata kama muhimu. Matokeo ndiyo haya
 
Ushauri wako Tafadhali.

Unajua mkuu Namtumba, rushwa imetufikisha mahali pabaya kabisa. Mimi sioni lingine isipokuwa rushwa na kukosa kuwajibika kila mtu ktk jukumu lake. Kabla sijaendelea Namtumba, nikuulize swali, unaweza kuniambia yule Nahodha wa ile Meli iliyoua watu karibu Elfu kule Nungwi yuko wapi?..maana waliopona walisema alichukuliwa na wafanyakazi wakatoweka nae. Sasa wahusika walimtafuta kumfikisha panapohusika?...hilo mi sijui, wana Jamvi wanaoelewa humu wanaweza kutudadavulia.Narudia kusema, RUSHWA na sheria kutupiwa kapuni ndio chanzo cha yote haya. Ntatoa mfano wa kwanini nasema Rushwa ndio inatuangamiza. Mwaka juzi nilipokuwa Tanzania, nilikuwa natoka Airport na rafiki yangu mmoja wa usalama barabarani, siku hiyo alikuwa day off. Kama unavyojua Nyerere road foleni. Sasa Daladala wakawa wanatanua hovyo hovyo,nikamuuliza yule Askari; Hivi hawa jamaa( watu wa Daladala ) hamna namna ya kukomesha hii tabia yao?...yule rafiki yangu alinijibu kuwa dawa waliipata, lkn hata nguvu yake ilipoishia hajui. Aliniambia walipewa maagizo kutoka juu, wakamate kila Daladala inayotanua, halafu dereva apelekwe moja kwa moja Mahakamani. Wakatekeleza. Ilikuwa kila anayefikishwa Mahakamani anapigwa miezi 3, no fine. Rafiki yangu aliniambia Dsm kwa muda ilikuwa na adabu ya udereva maana taarifa zilisambaa kwa hiyo kila mtu akawa makini barabarani . Mfano huu dhahiri unaonesha kila mtu akiwajibika ktk majukumu yake na rushwa ikapewa kisogo ( Ingawa ngumu kwa mahali TZ ilipofikia) naamini kila mtu atakuwa na adabu barabarani. Hata haya matuta tunayowekewa barabarani, ni uvivu wa watu kufanya kazi. Badala ya kuwa na sheria kali tunawapunguza speed madereva kwa kuwawekea matuta. Ughaibuni huku (Japan) juzi juzi Dereva wa basi la long trip, kapigwa miaka 13 jela baada kusababisha ajali kutokana na usingizi.Mkuu Namtumba, sijawahi kuona matuta huku kwa wenzetu, barabara kama ulimi, safi, lakini kila mtu ana adabu barabarani, kwanini?...kwa sababu kila mtu anawajibika kwenye jukumu lake. Ukipanda Highway(Express way) speed mwisho 100, ukizidisha unashtukia unapigwa mkono, point kwenye leseni unakatwa na pesa unalipa. Sisi tunaumia na rushwa na kukosa kuwajibika. Vinginevyo kila mtu angekuwa na adabu barabarani.
 
Madereva wa Malori, watembee usiku tu. Labda kwanzia saa 12 Jion mpka 12asbh.
Muda ukmfikia yupo njian.ana paki lori pmbn asbr mpaka jioni..6pm
 
Bado hazitoshi kwasababu nyengine ziko ktk nje ua uwezo wetu
 
Madereva ndio tatizo. hata kama barabara mbaya dereva ndio wa kuchukua tahadhari.
 
Hatuna raha na safari kwa kweli, yaani mtu unakaa kwenye gari roho juu juu kama mabawa ya ndege khaa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom