Kung'atuka kwa uelewa wangu mdogo kunachukua muelekeo wa mtu kulazimika kuacha kitu fulani bila ya hiari yake pengine mazingira yamemfanya achukue uamuzi huo. Sina uhakika kwa asilimia 100 kua Mwl alitumia neno hilo kwa mantiki hiyo possibly.
Ambacho nilikikusudia sana ni kutathmini maneno ya Mwl kwa ujumla na ukweli wake ktk wakati tulionao na sio neno mojamoja na ninadhani kua maneno ya Mwl kwa ujumla yanaeleweka no matter kung'tuka itakua na maana gani.
Naomba mchango wako sister au kama ni brother please. Thanks.
Mlikuwa mnaving'ata viti kwa mananihii?
Hilo neno ukitaka usitake asili ya maana yake ndio hiyo, linatokana na kung'ata, halafu huko kwa kina Nyerere si unajuwa meno wanayafanya nini? wee kwa kung'ata yale aking'atuka lazima ubaki na majeraha sio ya kawaida.
Ng'ata, ng'atana, ng'atuka, ng'ang'ania. Huwezi kung'atuka ikiwa hujang'ang'ania. Na ndio maana hao wazee walikuwa wanawaambia "ng'atuka" kwa kuwa hata mnapoona watu wazima nyie bado mmeng'ang'ania kung'ata kwa mananihii hivyo viti, wazee hawajakosea walipokuwa wakiwaambia hivyo.
FF mwanzoni niliona yule alokuambia usubiri umalize Menses ndo ucomment kakuonea lakini sasa naona alikuwa na haki >100%, Unaparamia maneno hata usiyojua, na Jasusi kaeleza asili na Ukweli wa neno Kung'atuka bado huelewi! Usinambia Hormone za Menses ziko kwenye Peak maana huathiri Judgement!
Kwanza nianze kwa kuwashauri ndugu wanaoshiriki ktk kutathmini neno Mwl kutotumia lugha chafu ambayo kwa njia moja sio inamdhalilisha mchangiaji bali hata watu wengine wanaoshuhudia matusi mazito kama hayo.
Daiama ninapenda kurudi kwenye topic ambayo labda nitoe historia yake kidogo. Wakati ninaangalia habari 'michuzi' Niliona kikao cha NEC na kukawa na bango ambalo limeandikwa 'Mimi ninang'atuka lakin bila CCM madhubuti nchi itayumba' Kilichonisukuma kuanzisha mjadala huu ni 'Sikufahamu CCM message ile walikua wanaambia watu au wanajikumbusha wao wenyewe'.
Ukifikiria kwa makini mazingira aliyoondokea Mwl mpaka yeye mwenyewe asitumie neno jingine akatumia kung'atuka kuna message alitaka waTanzania wenzake wailewe. La kujiuliza jee message imeeleweka?
Wadadisi wa mambo wanadai kua huwenda Mwl alikusudia kua inawezekana wengine nao wakalazimika kung'atuka baadae sio kwa kupenda lakin mazingira yakawalazimisha. Kuna wanaooona kua Mwl alipambana sana mpaka akafikia hatua ya kukatishwa tamaa kwamba asingeweza kufanikiwa au kutimiza malengo ktk uhai wake possibly! kwa sababu alikua ktk wrong time and wrong place.
Upande mwengine ni ule unaodhani kua Mwl kwa hali yoyote alichukua uamuzi wa busara wa kung'atuka ukilinganisha na mtu kama Gaddafi. Any way wewe unaonaje?
Bibie,Jasusi na wewe wote hamuelewi maana ya uasili wa maneno. Ung'atuke bila kung'ata au kung'ang'ania? Unanchekesha!
Hilo la menses nnaelewa kuwa ufahamu wenu ni mdogo sana, ngoja nikupe darsa kidogo: Kuna "practice" ambayo ilikuwa inatumika sana katika kuwaongezea wanaume afya kimwili nayo ilikuwa "recommended" na "practitioners" ambayo watu kama wewe ambao hamna uelewa hamuitumii, wenzenu "walioendelea" baada ya kuiacha kwa muda mwingi sasa wanairudisha tena kwa kasi sana na inawasaidia sana kuweka miili na akili zao sawa, nayo huitwa "blood letting" au sisi watu wa pwani huiita "chuku" kwa Kiswahili. Nakuomba ui google hiyo uielewe ni nini na utaona kuwa Mwenyeezi Mungu aliyetujaaliya sisi kuwa nayo hiyo within our system kuwa AlhamduliLlah katupendelea sana. Nenda na wewe ukafanyiwe manual nna uhakika itakusaidia.
Maana nnakuona una mashaka na Mwenyeezi Mungu alivyotuumba, usiwe na shaka kijana "kazi ya Mungu haina makosa".
Halafu huwa mnashindwa kujenga na kujibu hoja mnarukia kumvaa mtu maungoni, halafu hata huyo wa kumvaa hamtazami kama kama mnalingana nae uzito, wengine ni ma heavy weight. Mnanchekesha!
Bibie,
Mbona king'ang'anizi hivyo? Nimeshakwambia kule kwetu hatuna neno kung'ata wewe unang'ang'ania tu kwamba kung'atuka linatokana na neno kung'ata. Unajua nini? Shida yako ni kwamba unataka kumweka Mwalimu kwenye dhana ambazo umeshajenga mwenyewe kichwani na kuwalazisha wengine kuwa hii ndiyo portrait sahihi ya Mwalimu. Mambo hayaendi hivyo. Kuna yule mwenzako Barubaru naye kakazana kuleta uwongo eti enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna cheo cha President nje ya Ikulu. Na yule rais wa wanafunzi wa chuo kikuu waliogoma je? Aliitwa Kimulson. Nina hakika ulikuwepo 1966 pale wanafunzi wa chuo kikuu waliporudishwa nyumbani baada ya kugoma kupinga national service. Tukubali Mwalimu aliondoka mamlakani kwa hiari na hakukamatwa kwenye mtaro wa maji au shimo la panya kama yale yaliyowakuta viongozi wengine. Na hilo si jambo la kubezwa hata kidogo.