kadri nilivyoangalia michezo mingi ya WC mwaka huu nimegundua kuwa mbinu za kisayansi kwenye mchezo wa mpira wa miguu zimfikia saturation level. Yaani kila timu inazijua; ndiyo maana timu za Marekani, New Zealand, na zile za Balkan zimefanya vizuri kuliko zilivyotegemewa na kuzikuta timu za kutisha kama Ufaranza, Italy, Uingereza na Ujerumani zikihaha. Ingawa timu za Afrika zimefungwa na kuondolewa kwenye raundi hii ya kwanza tu, ukweli ni kuwa hakuna timu ya Afrika iliyofungwa kirahis vile. Mabao yote yalikuwa yanapatikana ama kwa bahatibahati au kwa makosa madogo madogo ya walinzi, wala siyo kwa ubora wa wafungaji.
Kinachotakiwa katika muongo ujao ni kuwapata tena wachezaji wenye kuchanganya sayansi ya mchezo huo na mbinu zao binafsi ili kuwapita wapinzani bila kikwazo. Wafungaji mabao wa aina ya Pele na Okocha ndio watakaotakiwa tena katika siku za mbele.