Mimi sijaona ugumu wowote ule. Ugumu upo bongo bana. Wakazi wengi wa kawaida wanahangaika sana hasa Dar. Asubuhi kukicha wanagombania madaladala ili wawahi vibaruani.
Na jioni hadithi ni ile ile. Ni kugombania usafiri wa kurudi nyumbani. Kwa kweli huwa sielewi kwa nini watu hugombania kuingia kwenye daladala. Hivi kwani wakijipanga mstari waingie kwa ustaarabu kitaharibika nini?
Madhila yanaendelea wakirudi nyumbani. Mara umeme hakuna, maji nayo ya kuvizia. Yaani kero tupu.
Hapo sijazungumzia mbu na nzi, mavumbi wala matope. Uchafu mitaani, makelele kwenye makazi, madanguro bubu kila kona, mibaa ndiyo usiseme kabisa.
Huduma za sekta karibu zote ni mbovu kupita maelezo. Si hospitali, si ofisi za serikali, si mahakama, mashuleni ndiyo balaa. Ukienda benki mara ukute mtandao uko chini. Kama ukibahatika kuukuta upo hewani huduma utakayopata ni zaidi ya mbovu.
Urasimu uliokithiri ni puke fest! Hela zako mwenyewe lakini ukitaka kutoa zaidi ya kiasi fulani lazima ujieleze kama uko kituo cha polisi.
Ngoja niachie hapo maana hata sijui hili linchi linafuata mfumo gani wa kiuchumi.....yaani ni lipo lipo tu.