Mambo ya uzinzi siku hizi hayakemewi, mabinti wanapata mimba huku wanaimba kwaya, poa tu hawatengwi. Wengine wanafunga ndoa huku tayari ni wajawazito hawaulizwi kwa nini mmeanza kufanya tendo la ndoa kabla ya kufunga ndoa. Maagano ya ndoa hayafuatwi, wanandoa wanaachana haraka bila hofu ya Mungu