Wizi wa Pesa za Kodi Dar es Salaam aiport | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa Pesa za Kodi Dar es Salaam aiport

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KVM, Aug 2, 2012.

 1. K

  KVM JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Juma lililopita nilisafiri kupitia JNIA. Kitu cha kwanza baada ya kucheck-in pamoja na mizigo yangu nililakiwa na kijana (Security personnel) akaniuliza kama tiketi yangu ilinunuliwa mwezi huu (July 2012) au kabla. Nilimwuliza, kulikoni? Akanieleza kama nilinunua kabla ya July 2012 basi ni lazima nilipie kiasi cha $10 kwani kodi imepanda kutoka $20 hadi $40. Nikamweleza yule kijana kuwa tkt yangu ilinunuliwa June 2012 na hilo ongezeko silipi.

  Nilipofika kwenye meza ya kupata boarding pass walinipa boarding pass yangu halafu yule dada akaniambia nimwone mtu wa kodi. Nilikwenda kwa yule dada na kumweleza kuwa mimi sitembei na pesa na kama anataka pesa yangu basi achukue kutoka kwenye credit card yangu. Akanywea, nikaondoka zangu. Wakati wote nikiwa kwenye mstari nilikuwa naangalia kinachoendelea pale kwenye desk la "kodi". Watu walikuwa wanatoa pesa lakini lakini hakuna risiti iliyokuwa inatolewa kwa pesa iliyopokelewa bali kugonga mhuri kwenye boarding pass. Huu ni wizi wa waziwazi. Cha kusikitisha ni kuwa wengi waliokuwa wanatoa pesa walikuwa ni Watanzania kwani wageni, hasa wazungu walikuwa wanaogopwa.

  Licha ya tukio hili la jana pale JNIA kuna uswahili na ulaghai kwelikweli. Security personnel wa pale kazi yao ni kubughudhi wasafiri. Mara kadhaa wameniambia kuwa wanauza Kadi za Chanjo, n.k.
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Uwanja wa ndege wa Dsm ni sawa tu na stesheni ya basi huko kwa wenzetu.

  Kwanza kuna wajamaa pale wasumbufu sana ukirudi safari wanawahi mabegi yako wanajifanya wanakubebea halafu wanataka hela. Hii kitu sijaiona Airport ya nchi nyingine yeyote zaidi ya Dsm. Mheshimiwa Mwakyembe hebu nenda pale kasafishe wale wahuni waondoke wanakera sana.
   
 3. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Halafu JK anasema serikali haina hela ya kuwalipa walimu, kwa uzembe.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hawa sea urchins na leeches wanaokaa pale wana njaa sijawahi kuona.

  Kuna mmoja, baada ya kuninyanyasa sana kuhusu uzito wa mizigo akaniambia hilo swala la ongezeko la $10, nikampa Tsh 20,000, and she had the nerve to ask to keep the change bila aibu.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa...hiyo cha mtoto. Mimi kuna mmoja bila hata soni aliniambia 'kaka niachie basi hiyo saa na mi nitokelezee'. Nikamwambia 'unacheza wewe'.
   
 6. K

  KVM JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  I hope they gave you the official Exchequer Receipt Voucher, not simply a stamp on your boadring pass!

  Kwa kweli njaa ya wale watu wa airport inanikera sana. Mara nyingi wanawalenga watu weusi. Nadhani watu wa kuwaeleza matatizo haya ni Swissport. Mara kadhaa nimewasiliana na Gaudence Temu ambaye ni Meneja Mkuu wa MD kwenye maswala mengine kama kupotelewa na mizigo alikuwa ni mtu wa msaada sana.
   
 7. mito

  mito JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,619
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  aisee wanatia aibu sana, mi kila nikipita pale (hata kama sina kosa lolote) wananiambiaga 'kaka tuachie hata ya chai hali mbaya'

  kuna security guard aliwahi kunifuata hadi kule boarding lounge ananibembeleza eti nimwachie madafu niliyobakiza, yaani kero sana aisee!
   
 8. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hiyo hata Mimi walishawahi nifuata mpaka juu kule kwenye boarding launge, eti niwaachie change za madafu zilizobakia... Nikawaambia Ni bora niweke kwenye zile chupa za misaada, Hebu acha kuwa omba omba... akaondoka... Tena alinianzia tangu navua mkanda kukaguliwa pale chini...
  Ule Uwanja wa ndege ni aibu tosha... Wakiwa wanakukagua mizigo utasikia Niachie basi hiyo simu au naomba hata t-shirt...ggggrrrrr
   
 9. Y

  YE JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona hiyo ndogo, mi nilikuwa namaliza mihuri ya uhamiaji kabla ya kuondoka nikaambiwa kuna afande anataka kuniona. Nikajua toba, labda kuna mtu aliweka madawa kwenye mizigo waliyonipa ya ndugu zao. Basi huyu afande na minyota kibao na kirungu akawa ananisubiri kwenye corridor, hee si kaanza kuniuliza maswali mara niachie hata dola mia.
  Hasira za ghafla zilinishika nikamwambia ajiheshimu na aniogope kama ukoma. Akanyewea akasepa. NI AIBU YA KUFA MTU PALE!
   
 10. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mie ndio wala sibishani tena ukiwa mwanamke ndio zaidi,mie nilitoaa hiyo dola 10 mwenzangu akatoa elfu 20 tukaondoka zetu wakati tkt tumekata 28jun....ah hay a nawapate wao...
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wa hapo airport ni wakushughulikia kuna siku wamechukua pen yangu yenye camera kwa kigezo eti siruhusiwi kuingia nayo ndani ya ndege ni kifaa cha kielectronic kisicho cha kawaida na nikaona ili kuepuka zogo bora niwaachie.
   
 12. Donkey

  Donkey JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 676
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 80
  Airport ya dar ni Tatizo sana, nimehawi safiri sana kwenda nje, nikirudi tu, unakuta watu wanakuja kwenye mizigo na kuuliza brother una mizigo mingi? halafu akasema tunaweza pita bila lipia kodi na utaniachia pesa kidogo , du sikuamini, last week nilikuwa napokea wageni to nje na walikuwa wanachukua visa on arrival, aibu kubwa ni kwamba walisema immigration ya Tanzania iko very poor kwani, walikusanya passport na kwenda nazo ndani, kurudi wanasoma jina la mtu kwenye passport na kutembea nazo kuuliza majina ya mtu, swali kwanini hakuna utaratibu kama ule wa kwenda kuchukua passport american embassy, jamani ni lini tutabadilika.
   
 13. C

  Cape city Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Very true..limenikuta nami on 22nd of july wakati naondoka huko tz. Nimecheck-in poa, kwenye boarding pass desk wakanikomalia airport tax $10...dah, ilibidi niwape baada ya mabishano ya kama 30min na ndege inakaribia kuruka. Nilichukia sana, ila walinipa risiti..! Airport ya ajabu sana ile, pumbavu
   
 14. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mimi waliniita nikajifanya siwasikii nikapeta Sijui wakati wa kurudi Itakuwaje? Lakini as Long nitakuwa nyumbani basi liwalo na liwe.
   
 15. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Ukifika pale usiongee kiswahili,ongea english utashangaa hawakusumbui
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  ukifika pale akianza kukusemesha usizungumze kiswahili...utaona wanakwepana halafu wanakuacha
   
 17. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180

  Ahsante mkuu kwa kunipa huu ujanja ni mzuri nitautumia!
   
 18. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 363
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  enyi wenzetu mnaosafiri manchi ya wenzetu huko, eti nao wameweka scan ya mizigo unapotoka? hapa kwetu naona ukiondoka wanscan na ukirudi hivyo hivyo, embu nitoeni ushamba
   
 19. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  siwalaumu sana kwa sababu wanakkuona wewe una hali nzuri kidogo unaweza kusympathise nao. Kiapo chao cha utii kinawafunga na hawawezi kugoma kudai nyongeza ya mishahara lakini wana hali ngumu kimaisha na bahati mbaya maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa kama ndoto kwa sasa. :A S cry:
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Aisee hii nchi kwa sanaa imepitiliza jamani.
   
Loading...