Wizi wa masega kwenye magari

Kiongozi Miongoni

Senior Member
Feb 6, 2021
197
255
Wasalaam wana wa Jehova.

Kuna tatizo linaendelea kuwa sugu katika jamii yetu. Kuna kitu kinaitwa masega kwenye exhaust ya magari na hiki kitu kina kazi maalumu katika mfumo wa gari, sijui kazi yake kubwa ni nini kwa maana mimi siyo mtaalam wa mambo ya magari.

Last week gari yangu ilikuwa inapoteza nguvu na kutoa mlio mkubwa inapokuwa inatembea, niliamua kupeleka kwa fundi mmoja hapa mjini ninapoishi. Baada ya kufanya ukaguzi wa gari, fundi aliniambia kuwa gari tiyari imeibiwa masega.

Nilimuuliza fundi je yanaonekana kuibiwa lini, fundi akasema inaonekana yameibiwa kitambo na akaniambia kuwa wezi wa masega ni wengi na wayaiba kwa haraka sana.

Basi nikamwambia anitafutie masega mapya niweke, yule fundi alikataa kunitafutia masega kwa madai kwamba nisijaribu kuweka masega mapya maana nitagombana na watu, kwamba nikishaweka masega mapya ntakuwa simwamini mtu yoyote kumpa gari na kwamba hata nikipeleka gari garage itabidi kikae kwa sababu ntakuwa na wasi wasi kuwa yataibiwa tena.

Fundi anasema magari mengi yameibiwa masega ila wamiliki hawajui kwa sababu magari yao hayajasumbua.

Sasa najiuliza masega yanatumika kufanyia kazi gani na kwa nini yamekuwa ni deal kubwa kiasi hiki?.

Je, serikali haioni umuhimu wa kulifuatilia suala hili?

Wasalaam.
 
 
Ukisoma kwa makini utagundua kwamba, huyo fundi wako hajagundua tatizo la gari lako na wala hayo masega hayajatolewa. Achana na huyo fundi utafute fundi mwingine makini halafu, leta mrejesho....
Pia unaweza kuelezea vizuri tatizo la gari lako upate ushauri wa wapi pa kuanzia...
Mfano: Kupoteza nguvu na mlio mbaya kuna weza kuwa umetumia mafuta machafu kwa muda hivyo inaweza kuwa gari haichomi au hayapiti vizuri kwenye mfumo hivyo unatakiwa usafishe tank na plug....
Lakini pia yaweza kuwa gari inahitaji kusafishwa diff na kuweka oil mpya ya diff hasa kama ni gari ya zamani) nk nk
Hiyo ya masega weka mwishoni kabisa....
 
Yanaitwa mafla kwa kilo moja wanauza hadi sh 50,000 inategemea na Aina ya gari industry yake Ni biashara ya chuma chakavu Kuna copper, alluminium hata betri za gari Ni vitu vinavyowaingizia Sana pesa wajanja wachache wa hapa mjini..tatizo uuzaji wake unaprotocal Kali Sana la sivyo jiandae kupigwa na madalali
 
Back
Top Bottom