Wizi wa mafuta BP/Puma Sinza Kijiweni

Wizi wa mafuta BP/Puma Sinza Kijiweni

Kuna kipindi EWURA walikuwa wanafuatilia kituo kwa kituo kukagua pump na wizi kama huo,waliishia wapi? Wizi wa mafuta umekithiri sana kwenye vituo vya mafuta na kama kutakuwa na ufuatiliaji wa makini ni rahisi kuwanasa na iwapo hatua kali zitachukuliwa tatizo litakwisha.Imefikia mahali madereva wakiwa wanawekewa mafuta inabidi ushuke kwenye gari ili ukague kama unaibiwa au la,sasa haya ndio maisha gani jamini.
 
Huwa najaza mafuta Kituo cha Puma cha Airport naona wako vizuri pamoja na TOTAL Kwasokota Temeke.
 
Wana JF.

Leo asubuhi nimetoka kuweka mafuta BP/ Puma ya Sinza Kijiweni kiasi cha Lita 6.

Nimeondoka moja kwa moja kwenda posts ila cha kushangaza gari limenizimikia dar free market.

Huu si wizi huo?!

Msiokijua hicho kituo ndio hua mnaweka mafuta kibosi bosi, unaweka mafuta huku unaangalia simu, ukiambiwa tayari unalipa na kusepa. Huo ni ubwege.com na ukijaribu tu kwa kituo cha Sinza Kijiweni umeliwa vibaya sana.

Pale inatakiwa ukifika unazima kabisa gari unafungua Loki ya tank kisha unashuka kabisa mpaka kwenye tank. Mtajie kiasi unachotaka huku macho yakiwa kwenye meter reading. Hapo hutoibiwa kamwe!!
 
Hilo nalo neno chief!
 
Nimejaza mafuta vituo vingi ila suluhisho nimeliona Gapco na system ya card . Mwambie nataka mafuta ya kuanzia shs10,000 na kuendelea halafu mpe card ya gapco safari. Ukiona anakwambia mashine mbovu ujue pump wamechokonoa ila akikubali pump haijachokonolewa, kwani system yao ina link na gapco makao makuu. Kwa hiyo mwenye kituo hakubali mzigo ule kwake.
 
Sasa hii kadi ya Gapco safari sisi wengine tutaipataje?
 
Hiyo petrol station ni wezi sana, mwaka Jana niliweka mafuta ya elfu 20 gari yenye CC 1000. SIKUFIKA POSTA. EWURA KAMA KUNA MTU ANAFANYA KAZI EWURA WASHUGHULIKIWE HAO. PIA NIMESHASHUHUDIA WADAU KIBAO WAKILETA MZOZO KTK KITUO HICHO BAADA YA KUIBIWA.
 
Kweli we walikupiga. Kwa gari yako, mafuta ya hela hiyo ulitakiwa uende posta na kurudi na kwenda tena hasa kama unakaa maeneo hayo ya Sinza.
 
Vituo vyote vya mafuta lazima kuna mashine mbili ambazo zinaiba mafuta
 
Yule mmiliki anaitwa matembo amekaa sana nairobi kna wakati nlikuwa napiga mishe huko yeye alikuwepo huko kabla hajaokoka huko alikuwa ni maf. ..balaa siku hzi kamrudia mungu anakwambia, mm nikienda Victoria akiwepo ah lazima anipe lita 5 za wwese. ..jamaa ana stori ndefu sana hata ule mguu wake unaona anachechemea ni balaaa a hahahah, utajiri una stori ndefu watu kupata
Nakumbuka wabishi wakitanzania wakati ule alikuwa ni yeye na Bwana mwingine akiitwa Salewa.
 
Hawa wa Sinza kijiweni wamezidi ni balaa kubwa sana!!!.Mimi na ki stalet changu walinipiga ni siwezi weka tena kituo kile!!!!!!!!!

Hapo sinza kijiweni hta mi walishanitoa ushamba, ni kweli pale shida ipo!!!
 
Mimi nawashangaa sana vijana wengi. Hufika kwenye pampu, yu na simu, anamnyooshea huduma shs zake 10,000/- kama vile hataki. Akishajaziwa huondoka kuzunguka na baada ya muda analalamika kuwa kaibiwa. Wenzetu hutoka kwenye gari na kusimamia ujazaji. Hivyo huwezi kulala ila. Jamani thanked !!!
 
Sitetei wezi wa mafuta ila tuwe tunaangalia, unakuta mtu anaendesha gari anatumia hadi mafuta ya reserve akiweka ya 20k Km chache tu taa inawaka afu analalamika ameibiwa.
 
Puma hapa kijiweni ni wezi balaaa ukienda unakuta wameweka pump vibaya usipo kuwa nao makini wanakuingiza mjini,
Mara mbili walitaka kuniibia nikawaletea balaaa, sasa wamekalili na gari awanifanyii upuuzi

Bongo wafanyabiashara wana raha sana, yani mtu anataka kuibiwa mara mbili na bado unarudi tena?
 
Hata mimi nilipita kujaza petrol kwenye baiskeli yangu, aisee! wanichakachulia nusu lita wakati mimi nilinunua lita moja.
 
Back
Top Bottom