Wizi Wa Laptops

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,036
Kwema jamanii washika dau? Hivi mnajua kwamba sasa Dar ni hatari sana kwa wale wanaotembea wamening'iniza laptop zao mabegani? Ndugu yangu kuna watu wako standby kuipora na kukimbia nayo. Najua unajiuliza luwa inakuaje???

Sikiliza, ukiwa unatembea barabarani hasa kwennye njia za watembea kwa miguu ambazo Dar magari yanazitumia pia, jihadhari sana na magari yanakuja nyuma yako, hawa jamaa huja kwa mwendo mdogo sana na akisha kukaribia mmoja wao anaivuta laptop yako toka begani mwako na gari kutokomea kusikojulikana.

Naongea kitu ambacho nimekushuhudia kwa macho mara mbili na mimi nikiwa nimekoswa koswa bara bara ya mwenge- ubungo kati ya junction ya mlimani city na mwenge. Jamaa walikuja na kupora laptop kwa mtembea kwa miguu, na siku nyingine vivyo hivyo.
Kwa kifupi, kuweni makini, asanteni
 
Ndugu yangu Elli nashukuru kwa kuwataarifu wajumbe.

Kusemakweli huo ni ukweli mtupu, maana yapata mwezi mmoja sasa mdogo wangu yalimkuta pale Ikulu kuelekea kituo cha Kivukoni toka wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Laptop yake ilivutwa na mkanda wa lile bedi ulimnasa shingoni, alianguka akapiga kichwa kwenye tairi kabla ya kuburuzwa umbali mrefu kiasi kisha akapoteza fahamu, Chakushukuru ni kwamba hakupoteza maisha.

La muhimu
Wale Mabrazamen na Masista du, wanaopenda ujiko kwa kujidai wamebeba laptop huku ndani ya begi kukiwa na makaratasi tu tena yasiyo na ishu nawaombeni sana muwe makini. Mtakuja poteza maisha bure wakati laptop hamnazo. Hii ni ishu serious wazee kuweni makini.
 
usemayo ni kweli ndugu yangu haya mabegi yanayofanana na ya kubebea laptop yamekuwa kishawishi watu wakifikiria wamebeba laptop kumbe amejibebea zao mitumba. Kweli unaweza kukabwa kwa kudhaniwa kuwa umebeba laptop.

Kwa wale wanaojua hili wameanza kuacha kubebe laptop kwenye mabegii ya laptop wametafuta njia mbadala ya kuzibebea kama mabegi ya ma-dent n.k.
 
Ndugu yangu Elli nashukuru kwa kuwataarifu wajumbe.

Kusemakweli huo ni ukweli mtupu, maana yapata mwezi mmoja sasa mdogo wangu yalimkuta pale Ikulu kuelekea kituo cha Kivukoni toka wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Laptop yake ilivutwa na mkanda wa lile bedi ulimnasa shingoni, alianguka akapiga kichwa kwenye tairi kabla ya kuburuzwa umbali mrefu kiasi kisha akapoteza fahamu, Chakushukuru ni kwamba hakupoteza maisha.

Kama kweli ilitokea sehemu hiyo basi inabidi uende polisi ambao watawasiliana na ikulu na kuweza kuwashika washenzi hao. Kwani kuna kamera 24/7 pale. Fanya hima usiogope peleka issue hiyo mbele kwani wangemuua huyo ndugu yako. Kama Kamera za ikulu zilinasa tukio hilo basi mwenye gari itabidi aeleze ni nani alikuwa na gari hilo siku hiyo.

Mimi ilinitokea na nilichukua hatua ingawa inakuwa vigumu kuwatia hatiani kwa kukosa ushahidi. Inakuwa ghafla sana lakini kwa hili la ikulu mtafanikiwa tu. Tusilee tabia hii kwa kuogopa usumbufu ni ya hatari sana itakuja kuua mtu. Polisi hawachukui hatua ya kuweka mitego na kumaliza kadhia hii. Sisi tuchukue hatua wenyewe.
NB: nilishawahi eleza kilichonitokea katika posti moja hapa

Nyati
 
Back
Top Bottom