SoC01 Wizi wa Fedha za Umma: Mapendekezo ya Hatua za Kuchukua

Stories of Change - 2021 Competition

Uchumi wa Mifugo

JF-Expert Member
May 20, 2021
345
575
Tanzania ni moja kati ya nchi masikini Duniani kwenye kundi hilo tupo na Burundi, Sudan Kusini, Niger, Msumbiji pamoja na nchi nyingine nyingi. Nchi hizi masikini Duniani zina sifa zinazofanana ambazo ni kama vile kuwa na vita, njaa, ufisadi, miundombinu mibovu, huduma mbaya za afya,elimu duni na kutawaliwa kimabavu.Tanzania hatuna vita wala njaa lakini tuna ufisadi.

Kwa miaka mingi wananchi na vyombo vya habari wamekuwa wakipiga kelele kuhusu wizi wa fedha za umma na imekuwa kawaida karibu kila siku vyombo vya habari nchini kutangaza kuhusu wizi wa fedha za umma au wizi wa mali za umma ikiwa ni pamoja na miradi ya serikali kufanyika chini ya kiwango au kutokufanyika kabisa kutokana na fedha za umma kutafunwa na watu wachache kwa manufaa yao na mbaya zaidi zinatafunwa na maafisa wa Serikali au viongozi wa umma.

Jambo hili linaonekana limekosa dawa mujarabu. Fedha hizi zinazopotea zingeweza kwenda kujenga shule, vituo vya afya,kujenga barabara, kujenga miundombinu ya maji na matumizi mengine mazuri kwa manufaa ya Watanzania wote.

Nini kifanyike?

Njia zifuatazo zinaweza kumaliza tatizo hilo au kupunguza wizi wa fedha za umma nchini.

Utangazaji wa Zabuni

Ubadhirifu wa Fedha za Umma unaanzia kwenye utangazaji wa zabuni hapa ndipo watu wanakotengeneza ulaji wa kupata asilimia 10, mkandarasi asiye na uwezo lakini anayeweza kutoa asilimia 10 atapewa kazi, matokeo yake kazi haitakamilika au itafanyika kwa kiwango duni kwa sababu mkandarasi atataka kufidia asilimia 10 yake aliyoitoa kwa kuhonga wajumbe wa kamati ya zabuni na watendaji wengine wa serikali.

Serikali inatakiwa ihakikishe wajumbe wa kamati za zabuni za serikali kuu na serikali za mitaa zina wajumbe wenye uwezo na wazoefu kwenye miradi wanayotaka kuingia zabuni,pia kila kamati iwe na afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye kazi yake itakuwa kuhakikisha mchakato wote wa zabuni unafanyika kwa kufuata utaratibu na kwa kuzingatia vigezo kwa kupata mkandarasi mwenye uwezo wa kazi.

Uwazi

Kati ya vitu vinavyosababisha miradi ya umma isifanikiwe au ifanyike kwa viwango duni ni usiri unaogubika mradi mzima, miradi haishirikishi wananchi wala viongozi wao. Kinachotakiwa serikali itumie tovuti yake na mitandao ya kijamii iweke miradi yote inayotekelezwa na ambayo ipo njiani kuanzishwa au ambayo imekamilika.

Mfano: Mradi wa Maji uliopo Namatuhi, Songea mwananchi wa Ukara - Ukerewe aweze kuufahamu, afahamu jina la mradi, madhumuni ya mradi, jina la mkandarasi na jinsi alivyopatikana, sifa za mkandarasi, gharama za mradi, tarehe ya kuanza na tarehe ya kuisha na vitu vingine muhimu.

Mara nyingi miradi kama maji, barabara, ujenzi wa zahanati au vituo vya afya imekua ikifanyika kwenye maeneo ya wananchi lakini si wananchi wala viongozi wao wanakuwa wanaifahamu hiyo miradi, wanakuwa hawaifahamu kwa kina wanaona barabara inajengwa lakini hawajui kama itakuwa ya lami au ya changarawe.

Miradi ya aina hii ni rahisi sana fedha za umma kupotea. Kukiwa na uwazi ni rahisi hata kwa wananchi kufuatilia na kutoa taarifa mapema pale inapoonekana kuna tatizo. Kukiwa na uwazi ni rahisi kwa wananchi, madiwani, wabunge, wenyeviti wa mitaa au vijiji, maafisa wa vyombo vya usalama kufuatilia wanapo ona kuna ubadhirifu au mradi unafanyika ndivyo sivyo.

Joseph Mbunda ni mtaalam wa masuala ya Uongozi na mtumishi mstaafu wa Serikali anasema "wasimamizi wa miradi ya maendeleo wawashirikishe wananchi wa maeneo husika ili wawe wa kwanza kutoa taarifa kunapokuwa na tatizo na pia waione ni miradi yao, kutokuwapa taarifa juu ya mradi ni kuwaweka mbali na mradi kwahiyo hata wakiona simenti au bati zinaibwa watakaa kimya"alisema Mbunda.

Viongozi wenye Sifa

Serikali ihakikishe inateua viongozi wenye sifa kwenye kushika nyadhifa mbalimbali. Kwenye kila mradi unapofanyika kuna wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa wilaya na mikoa lakini ni kawaida kusikia mradi umesimama, unasuasua, umejengwa kwa viwango duni au fedha za mradi zimeibwa.

Mfano mradi wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe mkandarasi kampuni ya Badr alighushi nyaraka na kujipatia bilioni 27 kama viongozi na watendaji wa Wilaya husika na Vyombo vya Usalama wangetimiza majukumu yao vizuri hizo fedha zisingeweza kutoka na kulipwa mkandarasi ambaye alikuwa hajamaliza kazi.

Julai 24,2021 Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango aliagiza kusimamishwa kazi aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Hamis Dambaya kwa kosa la upotevu mkubwa wa fedha za umma. Nanyumbu walijenga stendi ya mabasi iliyotumia bilioni 2.3 kiasi ambacho Dkt. Mpango alisema hakilingani na ujenzi huo. Dkt. Mpango alisema viongozi wa umma hawana budi kusimamia fedha za umma zinazo pelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Tarehe 15 Augusti 2021 Waziri Mkuu, Majaliwa K. Majaliwa alitembelea miradi iliyopo katika manispaa ya Temeke na kubaini ubadhirifu wa fedha za miradi ambapo aliiagiza TAKUKURU kumfikisha mahakamani aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi na wenzake kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa barabara ya Kijichi-Mwanamtoti yenye urefu wa kilomita 1.8 iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.4 na barabara ya Kijichi-Toangoma yenye urefu wa kilomita 3.35 iliyojengwa kwa bilioni 13.5.

“Manispaa ya Temeke waliamua kutujengea mradi huu kwa kuongeza gharama kubwa za ujenzi.Tumeona namna mlivyoharibu fedha za nchi. Hatuwezi kujenga kilomita 1.8 ya lami kwa gharama ya bilioni 5.4 na hatuwezi kuwa watumishi wa umma wa namna hii"
alisema Majaliwa.

Ili kujua kiasi cha fedha kilichopotea tuangalie ujenzi wa barabara zilizojengwa kwenye mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma ambako kumejengwa barabara za lami ngumu zenye urefu wa kilomita
51.2 zilizojengwa na kampuni ya China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya bilioni 88.2, wastani wa bilioni 1.7 kwa kilomita moja lakini Mwakabibi na wenzake walitumia bilioni 5.4 kujenga barabara ya kilomita 1.8.

Wizi mwingine wa mali ya umma uliowashangaza wengi ni ule uliotokea Kilosa ambako aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Gairo, Asajile Mwambambale alikamatwa na Polisi kwa kosa la kuiba mabati 1,100 yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri ya wilaya hiyo ambayo yalikuwa kwa matumizi ya kuezekea majengo ya umma.

Wizi wa aina hii tungeweza kuuepuka kama viongozi wangekuwa wanateuliwa kutokana na uwezo wao na si kwa sababu ya kupeana ulaji au kulipana fadhila kwa sababu imekua kawaida sasa hivi makada wa Chama cha mapinduzi kuteuliwa kushika madaraka ya wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya bila kuzingatia uwezo wao na uzoefu wao matokeo yake wanashindwa kusimamia miradi ya serikali pia wanashindwa kusimamia matumizi ya fedha za umma.

Uteuzi wa makada hasa kutoka CCM ambao hawana uwezo ulisababisha CCM ivunje rekodi kwa kuwa na wagombea 8000 wa nafasi ya ubunge walioomba kuwania kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Malengo yao hayakuwa ubunge au uwakilishi malengo yao ilikuwa wakubwa wawaone na wawape nafasi za ukuu wa wilaya ,ukurugenzi na za ukatibu tawala"ni kweli sisi vijana wa CCM tunapenda kuchaguliwa kuwa viongozi wa serikali kwenye wilaya au halmashauri lakini Rais ahakikishe anateua watu wenye uwezo wa uongozi na pia aangalie rekodi zao za nyuma,asiteue watu wasio na sifa ambao wakipata madaraka wanashindwa kuongoza wenzao, kusimamia maslahi ya umma na kuishia kuwa wezi wa mali za umma"alisema Juma Nassoro mkazi wa Chang'ombe Dar es salaam na kada wa umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi.

Matumizi ya Teknolojia

Serikali itumie tekinolojia kufanya malipo ya Kiserikali, ni aibu kwenye zama hizi za sayansi na tekinolojia kusikia wakala wa barabara nchini kufanya malipo mara mbili kwa kazi moja au kusikia wakaguzi wa ndani wa wizara ya fedha kujilipa mamilioni ya fedha za walipa kodi kwa kufanya kazi hewa.

Haiwezekani watu wachache wajifungie ofisini na kuamua kujilipa fedha za umma na kusiwe chombo kingine kinachoweza kudhibiti uhamishaji wa fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine.Wakala wa serikali mtandao ina wajibu mkubwa kusaidia serikali kwenye suala hili.

Ofisi ya Mkaguzi wa ndani ijitegemee na ianzie wilayani.

Ofisi ya mkaguzi wa ndani iboreshwe kwa kupatiwa watendaji wa kutosha na iwe inajitegemea kama zilivyo taasisi nyingine zilizopo wilayani kama vile TAKUKURU. Ofisi hii inatakiwa iwajibike kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu ya ndani na si vinginevyo. Hii itaongeza ufanisi na kufanya ukaguzi kwa muda muafaka na ukaguzi wa mara kwa mara au wa kushtukiza.

Mzee Christopher Mwaipopo amefanya kazi ya uhasibu serikalini kwa miaka mingi anasema "kwa kawaida mkaguzi wa ndani hawajibiki ipasavyo kwa sababu anazungukwa na watu ambao ni mabosi wake na ndiyo anatakiwa awakague na mbali ya kuwaona kama mabosi pia anawaona kama wenzake kwahiyo kunakuwa na kuoneana aibu na mambo mengine mengi mengi".

TAKUKURU iwajibike kikamilifu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini hawajibiki ipasavyo haiwezekani halmashauri ya wilaya ya Temeke inatumia fedha za umma kwa kuzidisha gharama za ujenzi wa barabara halafu wao hawagundui mpaka wapewe maelekezo na mh.Waziri mkuu ya kufanya uchunguzi na kumfikisha mkurugenzi mahakamani wakati wizi umetokea zaidi ya miezi sita iliyopita.

Hii Taasisi inatakiwa iongezewe uwezo iwe na vitendea kazi vya kutosha,iwe na watumishi wenye weledi wa kupeleleza na kufanya uchunguzi ifanye zaidi kazi ya kuzuia rushwa.

TAKUKURU haitakiwi ifanye kazi kwa kupewa maelekezo inatakiwa inuse viashiria vya rushwa kila sehemu na ijikite zaidi katika kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi .

Ni wajibu wa serikali ilinde fedha za Watanzania, Watanzania wengi wanaishi maisha ya umasikini haipendezi kila siku wasikie wizi wa fedha zao wangependa zaidi kusikia habari za miradi kukamilika na wao wanufaike na miradi hiyo.
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mh.Stephen Kagaigai amesema kuna uhitaji miradi inayotekelezwa mikoani kusimamiwa kwa ngazi ya mkoa husika badala ya Serikali kuu ili kuharakisha ukamilishaji wa miradi hiyo.

Kagaigai amesema hayo wakati akizungumza na TBC na kuongeza kuwa ujenzi wa miradi ya jengo la mama na mtoto pamoja na jengo la huduma ya dharura katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi umekuwa wa kusuasua kutokana na ucheleweshwaji wa fedha kutoka wizarani.

Kagaigai amesema kwa kipindi Cha miaka 12 sasa jengo la mama na mtoto halijakamilika na akihoji anaambiwa fedha kutoka wizarani bado hazijafika"yaani inasikitisha miaka 12 jengo bado linajengwa huku akina mama wajawazito wanaendelea kuteseka kwa kukosa huduma mbalimbali ikiwemo kliniki ya mama na mtoto"amesema Kagaigai.

Chanzo TBC online, 3 Septemba 2021.
 
Je nani wa kumfunga paka kengele?
Viongozi waliopewa dhamana wasimamie vizuri fedha za umma na vyombo vya usalama Kama TAKUKURU,Usalama wa taifa pamoja na Polisi watimize wajibu wao ile interejensia za Polisi ndio zifanye kazi kuzuia upigaji vyombo vya usalama wadhibiti wizi kabla haujatokea.
 
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameridhia kuchukuliwa hatua za kufukuzwa kazi zaidi ya watendaji wa kata 20 wa halmashauri ya wilaya ya Iramba wanaodaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha shilingi milioni 300 zilizotokana na makusanyo ya tozo na ushuru mbalimbali.

Chanzo ITV tarehe 06 septemba 2021.
 
Hawa waheshimiwa wenyewe ni wezi tu.unakuta mtu amesaini kusafiri jumapili na kazi inafanywa juma tatu.mtu ana lala dar na kuondoka alfajiri mwendo mkali na dereva wake wa serikali spidi 160 180 ili ionekane kafika.na siku ya kurudi ni hivyo hivyo.
Hasara yake,
1.Posho za selikali nne zimeibwa,
2.ajali bara barani.
3.polisi kudharaulika.
4.polisi kuonekana taka taka mbele ya madereva kwa kufanya makusudi kukiuka alama za bara barani.
5.kukosa usawa wa uendeshaji.
6.kusababisha foleni kwa kutanua tanua ovyo.
7.kutoheshimiwa kwa muda wa kuendeshwa magari ya serikali.magari yanatembea mpaka usiku.
8.Serikali ingeokoa kiasi kikubwa kama zingemlipia ofisa husika mafuta aende na gari yake badala ya posho kwa madereva na gari hii hupelekea service kuwa karibu karibu na uchakavu kwa gari la serikali.
9.Polisi kuangalia na kupisha magari yenye taa za kingora wakati sio viongozi.
10.Serikali kuonekana kama haina meno kwa hawa watendaji wanaolala ovyo na kutumia posho ya safari.
11.Vibao vya hamsini kutozingatiwa polisi wanatunishiwa na raia.kisa eti yupo serikalini.
IGP tendeni haki kwa wote tunahasira sana barabarani.
 
Hawa waheshimiwa wenyewe ni wezi tu.unakuta mtu amesaini kusafiri jumapili na kazi inafanywa juma tatu.mtu ana lala dar na kuondoka alfajiri mwendo mkali na dereva wake wa serikali spidi 160 180 ili ionekane kafika.na siku ya kurudi ni hivyo hivyo.
Hasara yake,
1.Posho za selikali nne zimeibwa,
2.ajali bara barani.
3.polisi kudharaulika.
4.polisi kuonekana taka taka mbele ya madereva kwa kufanya makusudi kukiuka alama za bara barani.
5.kukosa usawa wa uendeshaji.
6.kusababisha foleni kwa kutanua tanua ovyo.
7.kutoheshimiwa kwa muda wa kuendeshwa magari ya serikali.magari yanatembea mpaka usiku.
8.Serikali ingeokoa kiasi kikubwa kama zingemlipia ofisa husika mafuta aende na gari yake badala ya posho kwa madereva na gari hii hupelekea service kuwa karibu karibu na uchakavu kwa gari la serikali.
9.Polisi kuangalia na kupisha magari yenye taa za kingora wakati sio viongozi.
10.Serikali kuonekana kama haina meno kwa hawa watendaji wanaolala ovyo na kutumia posho ya safari.
11.Vibao vya hamsini kutozingatiwa polisi wanatunishiwa na raia.kisa eti yupo serikalini.
IGP tendeni haki kwa wote tunahasira sana barabarani.
Kuna upigaji mkubwa kupitia posho wanazilipwa watumishi wa umma ,Kuna watumishi wanalipwa wakati mwingine hata hawasafiri akiambiwa apeleke uthibitisho wa safari anaenda stendi kununua tiketi ya elfu 2 anapeleka ofisini.
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo Asajile Mwambambale na wafanyakazi Saba wa halmashauri ya Kilosa ambao ni maafisa ugavi 4 na madereva 3 wa halmashauri hiyo waliotuhumuwa kuiba mabati 1,172 mali ya halmashauri ya wilaya Kilosa wameyarejesha mabati hayo.

Chanzo Mwananchi 7 September 2021.

Inawezekana ni wakati sasa wa kulazimisha wezi wa Mali ya umma kuzirejesha badala ya kuhangaika nao mahakamani.Na mfumo wetu wa uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka jinsi ulivyo unawezesha wezi kushinda kesi kirahisi.
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo Asajile Mwambambale na wafanyakazi Saba wa halmashauri ya Kilosa ambao ni maafisa ugavi 4 na madereva 3 wa halmashauri hiyo waliotuhumuwa kuiba mabati 1,172 mali ya halmashauri ya wilaya Kilosa wameyarejesha mabati hayo.

Chanzo Mwananchi 7 September 2021.

Inawezekana ni wakati sasa wa kulazimisha wezi wa Mali ya umma kuzirejesha badala ya kuhangaika nao mahakamani.Na mfumo wetu wa uchunguzi na uendeshaji wa mashtaka jinsi ulivyo unawezesha wezi kushinda kesi kirahisi.
Naona amesimamishwa kazi.
 
Wananchi wanalipa kodi lakini uvujaji wa mapato ni mkubwa
Screenshot_20210904-090656_1.jpg
 
Mada nzuri na yakizalendo kabisa lakini naomba tu niwakumbushe kwenye nchi zote zilizoendelea msingi mkubwa kabisa wa uchumi na maendeleo ni idara za intelligence kwenye nchi zao.

Ikumbukwe hawa ndyo washauri wakuu waserikali kwenye nyanja tofauti za kiuchumi, kijamii, namasula ya kiulinzi na usalama idara hizi zikiwa imara. na huru ndio zenye jukumu lakumshauri raisi wa nchi. niwapi kuna tatzo nini kifanyike kwa wakati husika kabla. Na baada ya madhila kufanyika.

Hawa ndyo wenyejukumu la kukusanya taarifa zote kwa maslahi ya nchi hivyo kama kuna mambo machafu yanafanyika inamaana kunatatizo mahali kwenye idara yetu

Kwakuongezea tu ndugu mwandishi inabidi serikali itazame mfumo mzima wa idara yetu. Na ufanyaji kazi wake. Ni lazima iongezewe majukumu zaidi yenye kulinda rasilimali za nchi. Hili litawezekana tu ikiwa tu sheria ya mwaka 1996 ya idara yetu itafanyiwa marekebisho na kusuka idara hii upya ilikuendana na dunia ya sasa
 
Mada nzuri sana.isipokuwa wanasiasa wanaingilia sana utendaji wa serikali kiasi ambacho hivyo vyombo vya uchunguzi kama Takukuru hata TISS wakitoa ripoti wanasiasa wanazikalia tumaana hizo kampuni ni mali zao na washirika wao.Tiss na Takukuru wanataarifa zote hizo lakini ndiyo hivyo tena.


Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom