Wizi wa ATM: Wanne wakamatwa Mbeya

Wizi wa ATM: Wanne wakamatwa Mbeya

Kwanini NMB!? juzi juzi tu ilikua mwanza leo huku tena sema ndio hakuna benki nyingine iliyo sambaa kama NMB.
 
Mimi sifanyi kazi CRDB na wala sio msemaji wao.....! Lakini haiwezekani kuiibia CRDB kwa aina hii ya wizi wa ATM, technolojia inayotumika na bank hii, wezi wanachemka!

All in all, haiwezekani kufanya aina hii ya wizi bila kuwa na ushirikiano na wafanyakazi wa bank husika wa kitengo cha IT. Hivyo basi kuwakamata hao wezi ni hatua ya kwanza, lakini pia kugundua wanao shirikiana nao ndani ya bank ni kubwa zaidi........! Ukichukua namba za simu za hao wezi, na ukachunguza mawasiliano yao kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita, huwezi kukosa namba za wafanyakazi wa IT wa NMB.

nina brother wangu mwezi uliopita kaibiwa milioni mbili pale crdb moshi mjini.
 
Hata CRDB wanapigwa kwny ATM sana tu mkuu,sema huwa ishu inakuwa siri sn,mteja ukiibiwa,ukienda kulalamikawanakuita wanakurudishia chako kimya kimya,
wana avoid sana ishu isiende kwenye media itashusha company's reputation.

Uko sahihi....
Niligundua upungufu kwenye akaunti yangu, nikaandika barua....walirejesha zile hela ndani ya robo saa....na wakaomba niiondoe ile barua!
Hela zilitolewa dirishani...(akaunti hairuhusu matumizi ya ATM)
 
Mimi sifanyi kazi CRDB na wala sio msemaji wao.....! Lakini haiwezekani kuiibia CRDB kwa aina hii ya wizi wa ATM, technolojia inayotumika na bank hii, wezi wanachemka!

All in all, haiwezekani kufanya aina hii ya wizi bila kuwa na ushirikiano na wafanyakazi wa bank husika wa kitengo cha IT. Hivyo basi kuwakamata hao wezi ni hatua ya kwanza, lakini pia kugundua wanao shirikiana nao ndani ya bank ni kubwa zaidi........! Ukichukua namba za simu za hao wezi, na ukachunguza mawasiliano yao kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita, huwezi kukosa namba za wafanyakazi wa IT wa NMB.

usijidanganye my friend wala asikudanganye mtu kwamba hawaibiwi kwa njia ya atm,card pekee ambayo wezi wa atm wameshindwa kupata taarifa ni za chip & pin.hakuna benki hata moja tanzania wanaotumia hiyo technolojia kadi za crdb ni chip and pin lkn haiko active so wanaibiwa sana .skimming ni challenge kila mahali duniani.
 
Hata CRDB wanapigwa kwny ATM sana tu mkuu,sema huwa ishu inakuwa siri sn,mteja ukiibiwa,ukienda kulalamikawanakuita wanakurudishia chako kimya kimya,
wana avoid sana ishu isiende kwenye media itashusha company's reputation.

Ni kweli, wateja kadhaa wa CRDB wameshaibiwa tena sana tu. Mimi nipo Mbeya watu wangu wa karibu kadhaa wameibiwa ila kama ulivyosema walikwenda kwa Meneja wa Tawi, akawataka kuwasilisha taarifa zao kwa maandishi na baadaye kurudishiwa fedha zao. Tena mmoja fedha zake zilionekana kutolewa kupitia benki moja ya Msumbiji.
 
Well well!
Ni upotoshaji tu wa vyombo vya habari walio kamatwa tukuyu leo sio wezi, ila ni wakopeshaji amb ao ukopesha wafanyakazi na wao kuweka dhamana Kadi zao za benki na kukabidhi na password kuwa mshahara ukiingia kachukue chako, na hii wa walio ishi mawilayani ipo sana.

hairuhusiwi kutumia ATM card ambayo siyo yako. Hao wezi
 
Ningependa kuweka taarifa ifuatayo kuhusu huu wizi wa ATM;-

  • Kwa africa mashariki makao makuu ya huu mtandao wa wezi wa ATM upo Nairobi kenya. Kule wahusika ni Wanaijeria, wakenya na wasomali. Wana mtandao mkubwa sana, vifaa vinavyotumika vilikuwa vinatokea JAPAN, na technolojia na information za kuweka kwenye ATM card zilikuwa zinatoka TURKEY, GREECE na UK sana.
  • Kuna kifaa kimoja, kidogo kama kidole na kinatumia betrii moja tu. Hiki hupewa wafanyakazi wanaofanya huduma ya mauzo kwa kutumia hizo card, ili wapitishie kadi za wateja kwenye hicho kifaa.
  • Pili, wanakuwa wanachukua informtion za mtu kwa kuwadanganya wameshinda ili wajaze information maalumu hasa DoB na Acc No (pengine jina wanakuwa wanalijua.
  • Tatu, wanapata iformation za wateja kupitia wafanyakazi wa benki husika hasa wa IT.

Baada ya kuwa na information hizo, hutengeneza kadi (doto), ambapo kadi (kurwa) anayo mteja halali wa benki husika. Kadi doto aliyonayo mwizi hana PIN number, ambapo anaweza kufanya manunuzi kwa kadi ile sio kwenda kuchanja ukuta (using atm). Lakini, wakiamua kumfuatilia mtu fulani, na hasa mtu huyo awe anatabia ya kwenda kwenye atm fulani mara nyingi hasa usiku wanaweza kupata pin namber yake...japo kibaya zaidi watu wengi huwa wanatabia ya kuweka mwaka wao wa kuzaliwa kama PIN.

Tchnolojia yao ya kuingiza infor zako kwenye kadi doto, halafu kuitumia kadi ile kwenye ATM ya CRDB inagonga mwamba, kwani kadi zao humezwa na hazirudi....hii ni kwa taarifa nilizonazo za ukweli kabisa. Pili, ukiibiwa hela zako katika ATM ya CRDB ujue eiza ni mtu wako wa karibu anayeijua PIN yako, na mara nyingi ni wafanyakazi wa humo humo CRDB huchukua hela yako na kusingizia imechomolewa kwenye ATM, but ukikaza na kusema unataka kuonana na meneja....fasta wanakurudishia....! Wanakuambia andika barua, pengine wasiifikishe kwa huyo meneja husika.....na hata meneja akipata hiyo barua, naye yupo kwnye mchezo huo au anacheki na kujua nani kachukua, wanamrudishia mteja wao wanajua watamalizaje hili soo lao.

Andiko langu ni kuwa, technolojia ya wezi hasa wa hapa Africa Mashariki yakutumia kadi doto kuibia hela kwenye ATM, haifanyi kazi kwenye ATM za CRDB.

cc. NIGGA, Watu, ndetichia, trigger, dwight na upendom
 
Mimi sifanyi kazi CRDB na wala sio msemaji wao.....! Lakini haiwezekani kuiibia CRDB kwa aina hii ya wizi wa ATM, technolojia inayotumika na bank hii, wezi wanachemka!

All in all, haiwezekani kufanya aina hii ya wizi bila kuwa na ushirikiano na wafanyakazi wa bank husika wa kitengo cha IT. Hivyo basi kuwakamata hao wezi ni hatua ya kwanza, lakini pia kugundua wanao shirikiana nao ndani ya bank ni kubwa zaidi........! Ukichukua namba za simu za hao wezi, na ukachunguza mawasiliano yao kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita, huwezi kukosa namba za wafanyakazi wa IT wa NMB.

Mbona unachanganya mambo? CRDB mara NMB???? Which is which sasa?
 
Retreat, nadhani ww ndio umechanganya au hujaelewa mada tangu awali....ni kuwa, nawaasa wapelelezi walio wakamata wezi wa atm kuwa wasachi namba zao za simu, wataona namba za wafanyakazi wa NMB walioshirikiana na wezi.

Soma uzi ulioletwa then, fuatilia ulipokosoa
 
Well well!
Ni upotoshaji tu wa vyombo vya habari walio kamatwa tukuyu leo sio wezi, ila ni wakopeshaji amb ao ukopesha wafanyakazi na wao kuweka dhamana Kadi zao za benki na kukabidhi na password kuwa mshahara ukiingia kachukue chako, na hii wa walio ishi mawilayani ipo sana.

uchunguzi wa kina ukifanyika ukweli utapatikana.SIO WEZI.ni wakopeshaji wanaotusaidia kutatua shida zetu.HAKUNA aliyeibiwa kadi wote walitoa kwa idhini yao wenyewe kulingana na huduma waliyohitaji,.vyombo vya habari viwemakini kutafuta ukweli wa mambo kabla ya kutangaza...kama kweli ni wezi BASI WANGESHA JITOKEZA WATU WALIOPOTELEWA CARD...
 
Samahani naiweka hii kwa kutumia simu...chanzo: Mbeya Yetu blog.....

HII NDIYO TAARIFA KAMILI YA WALIOKUTWA WAKICHUKUA HELA
KWENYE ATM YA NMB RUNGWE-

JALADA LA UCHUNGUZI.
MNAMO TAREHE 25.02.2013 MAJIRA YA SAA 20:40HRS HUKO KATIKA BENKI YA NMB TAWI LA TUKUYU LILILOPO TUKUYU MJINI WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI WILAYA YA RUNGWE WALIWAKAMATA. 1. JUMANNE S/O MAGERE, MIAKA 29, MFANYABIASHARA YA DUKA MKAZI WA MLOWO – MBOZI 2. JUMA S/O KABYELO, MIAKA 20, MJALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA, MKAZI WA MSASANI- TUKUYU 3. JOSEPH S/O PETTER, MIAKA 20, MKURYA, MKULIMA, MKAZI WA MSASANI- TUKUYU NA 4. MIRAJI S/O KETAHA,MIAKA 34,MFANYABIASHARA YA DUKA MKAZI WA MSASANI-TUKUYU WAKIWA NA KADI 150 ZA ATM ZA WATU MBALIMBALI WAKIWEMO WATUMISHI WA SERIKALI AMBAPO TAYARI WALIKUWA WAMESHATOA KIASI CHA TSHS 20,543,000/= KUTOKA KATIKA MASHINE YA ATM . BAADA YA KUHOJIWA MTUHUMIWA JUMANNE S/O MAGERE ANAKIRI KUWASHIRIKISHA WATUHUMIWA WENZAKE KUMSAIDIA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA NA KWAMBA KADI HIZO NI MALI YA WATEJA WAKE AMBAO WENGI NI WILAYA YA MBOZI WALIOKOPA VITU MBALIMBALI KATIKA DUKA LAKE ANALOUZA BIDHAA ZINAZOTUMIA UMEME ZIKIWEMO REDIO,TELEVISION PIA VYEREHANI,MAGODORO NA BAISKELI NA KUWA WATEJA WAKE NDIO WALIOMPATIA KADI HIZO PAMOJA NA NAMBA ZAO ZA SIRI [PASSWORD] ILI
AWEZE KUKATA DENI ANALOWADAI NA KUWAPATIA KIASI CHA PESA KINACHOSALIA. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA WAMEENDELEA KUHOJIWA KITUO CHA POLISI TUKUYU-RUNGWE WAKATI PIA UFUATILIAJI UKIFANYWA KWA WENYE KADI HIZO ZA ATM. UFUATILIAJI UNAFANYWA PIA KUONA KAMA KUNA UKOPESHAJI WA FEDHA TASLIMU UNAOHITAJI MALIPO NA RIBA ILI HATUA ZINAZOSTAHILI KISHERIA ZIWEZE KUFUATWA. HADI SASA UCHUNGUZI HAUJABAINI WIZI WA MOJA KWA MOJA ULIOFANYWA NA WATUHUMIWA KAMA ILIVYORIPOTIWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI WALA HAKUNA TAARIFA YA MTU KUIBIWA KWENYE AKAUNTI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI SANA NA “TRANSACTIONS” ZINAZOHUSU AKAUNTI ZAO KWA KUWA KUMEKUWA NA MALALAMIKO KADHAA YANAYOFIKISHWA VITUO VYA POLISI LAKINI YAKIFUATILIWA INABAINIKA KUWA CHANZO NI UTOAJI HOLELA WA NAMBA YA SIRI YA MWENYE AKAUNTI. Signed By, [DIWANI ATHUMANI - ACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
Back
Top Bottom