Wizi nyumbani kwangu Mbezi Beach

Wizi nyumbani kwangu Mbezi Beach

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
710
Hii ni kwa wadau wa tasnia ya filamu

Usiku wa kuamkia leo wezi wamepachua kitasa cha mlango mkubwa wa kuingilia nyumbani kwangu na kufanikiwa kuingia ndani.

Wameiba vitu vingi vyenye thamani. Lakini kimoja ambacho kinahusiana na tasnia ya filamu ni computer aina ya Apple iMac 20-inch model, toleo la 2008. Computer aina hii hutumika sana na watayarishaji wa filamu.

Kwa hiyo, yeyote atakayeona au kusikia iMac inauzwa awasiliane nami kupitia +255-762-949577.

Nitakuwa tayari kulipa kiasi watakachotaka kurudisha mali hizo. Hawa ni vibaka wa mtaani. Asanteni.
 
Jamani mi pia nimeibiwa usiku wa kuamkia juzi,naishi mbezi beach pia.wameingia ndani wakachukua laptop,cm na vitu vingine kadhaa!kumbe na majirani kibao wa mtaani kwangu walishaibiwa ila mi sikuwa nafahamu.nimejiuliza wameingiaje na nna mbwa mkali balaa na ckumskia akibweka.bado naugulia machungu ya kuibiwa sijarecover bado
 
Pole sana wadau kwa mikasa hiyo. Mungu atawalipa
 
Poleni sana, mimi nina namba za Polisi Jamii huwa nikisikia hata kama ni Paka huwa nashtuka fasta ila siku ya kuibiwa huijui, Poleni sana, tujifunze labda pia kuvikatia BIMA vifaa vyetu japo uchumi wetu ndio huo unabana sana
 
Mtaji wa maskini, na hizi divi .0 laki mbili na sitini tutalia sana, poleni wakuu
 
Kwa hiyo wezi wako watakuwa ni wadau wa tasinia ya filam?
 
na wezi wa siku hizi hawakuachi hivihivi...
Lazima wakutafune...mbona hamjaripoti hilo? Au limewavutia?
 
Hii ni kwa wadau wa tasnia ya filamu

Usiku wa kuamkia leo wezi wamepachua kitasa cha mlango mkubwa wa kuingilia nyumbani kwangu na kufanikiwa kuingia ndani.

Wameiba vitu vingi vyenye thamani. Lakini kimoja ambacho kinahusiana na tasnia ya filamu ni computer aina ya Apple iMac 20-inch model, toleo la 2008. Computer aina hii hutumika sana na watayarishaji wa filamu.

Kwa hiyo, yeyote atakayeona au kusikia iMac inauzwa awasiliane nami kupitia +255-762-949577.

Nitakuwa tayari kulipa kiasi watakachotaka kurudisha mali hizo. Hawa ni vibaka wa mtaani. Asanteni.
Dah!pole mkuu.
Mie nikisaidia upatikanaji wake sitarajii kukucharge chochote,maana mie pia ni mdau wa filamu.
 
na wezi wa siku hizi hawakuachi hivihivi...
Lazima wakutafune...mbona hamjaripoti hilo? Au limewavutia?

........Daaah ! Mkuu unawajua nini ? .....hata kama wamewananihinoo, bado hicho kitu hawakukiiba ndo maana hawajataja (yaani hakihamishiki)
 
........Daaah ! Mkuu unawajua nini ? .....hata kama wamewananihinoo, bado hicho kitu hawakukiiba ndo maana hawajataja (yaani hakihamishiki)

Hah hah haaaah hivi kwa nini Benki wasihitaji asset kama hizo?
Wao wanang'ang'ania mashamba na Nyumba tu wakati kuna asset nyiingi tu hazihamishiki...
 
Hawa jamaa naskia hupuliza dawa maana hata. walingia kwangu wala hawakuvunja na mpaka leo cjui walingiaje...na cjui kwa nin cktj hyo ckush2ka. Na c kawaida mim kuamka sa 4 asubuh mim huwa nakawaida kuamka mapema alfajiri.ila cku ya 2kio nlilakb fofofoo.
 
Niliibiwa pia Oct mwaka jana flat screen, sony Brevia, laptop 3, na simu ( iphone), xbox na game zake. Maeneo ya Kilongawima....kuna wezi sana kule. Nina hasira sana na wezi nina bastola waje tena waona
 
Kwa hiyo wezi wako watakuwa ni wadau wa tasinia ya filam?

Nimeelekeza kwanza hoja hii kwenye tasnia ya filam kwa sababu kifaa kilichoibiwa kinatumika zaidi kwenye tasnia hii.
 
Pole sana mkuu, mi waliniliza mwaka jana mchana kweupe nikiwa namtumikia muajiri... hadi leo bado naugulia! Mungu yupo, 40 yao itafika tu ...
 
poleni sana mwizi ni mtu mbaya sana siku zote anakuombea mafanikio ili aje akuibie
 
Pole sana Kiongozi!
Huku Arusha juzi jamaa waliingia hivohivo ndani kwa jamaa yangu, wakabeba vitu kibao, wakataka kuondoka na screen kubwa LCD, walipoona inawazingua wakainyanyua na kuibwaga chini, ikawa vipandevipande, wakaondoka!
 
Hawa jamaa naskia hupuliza dawa maana hata. walingia kwangu wala hawakuvunja na mpaka leo cjui walingiaje...na cjui kwa nin cktj hyo ckush2ka. Na c kawaida mim kuamka sa 4 asubuh mim huwa nakawaida kuamka mapema alfajiri.ila cku ya 2kio nlilakb fofofoo.
I know,sisi wenyewe tulilala km tumekufa tumekuja kushtuka sa 1 na huwa tunaamka sa 11.hadi bedroom kwetu walifungua madirisha kwa nje wakavuta cm na vingine,laptop ilikua sitting room,yaani ukiona walivyovuruga!inaonekana walipania haswaa.kumbe kwa jirani yangu waliiba vitu kibao vya thamani wakamuachia na zigo la mavi sebuleni
 
Back
Top Bottom