Wizi nyumbani kwangu Mbezi Beach

Wizi nyumbani kwangu Mbezi Beach

Hii ni kwa wadau wa tasnia ya filamu

Usiku wa kuamkia leo wezi wamepachua kitasa cha mlango mkubwa wa kuingilia nyumbani kwangu na kufanikiwa kuingia ndani.

Wameiba vitu vingi vyenye thamani. Lakini kimoja ambacho kinahusiana na tasnia ya filamu ni computer aina ya Apple iMac 20-inch model, toleo la 2008. Computer aina hii hutumika sana na watayarishaji wa filamu.

Kwa hiyo, yeyote atakayeona au kusikia iMac inauzwa awasiliane nami kupitia +255-762-949577.

Nitakuwa tayari kulipa kiasi watakachotaka kurudisha mali hizo. Hawa ni vibaka wa mtaani. Asanteni.

Pole sana. Mungu atakupa nyingine.
 
Pole sana. Mungu atakupa nyingine.

Usimdanganye huyo bwana...
Cha msingi mwambie apambane ili apate pesa ya kununua vingine.
huyo Mungu angekuwa anatoa vitu basi angejitoa mwenyewe ili watu wazidi kumuamini na kuwa na hofu ya uwepo wake.
 
Poleni sana, mimi nina namba za Polisi Jamii huwa nikisikia hata kama ni Paka huwa nashtuka fasta ila siku ya kuibiwa huijui, Poleni sana, tujifunze labda pia kuvikatia BIMA vifaa vyetu japo uchumi wetu ndio huo unabana sana

Sinza Polisi jamii wao wakikukamata wanakupeleka chocho kisha wanakupukutisha na kukupiga vitasa kisha wanasepa...ukienda Mabatini au Urafiki utachoka hayo majibu yao...
 
Niliibiwa pia Oct mwaka jana flat screen, sony Brevia, laptop 3, na simu ( iphone), xbox na game zake. Maeneo ya Kilongawima....kuna wezi sana kule. Nina hasira sana na wezi nina bastola waje tena waona

Nina uhakika safari hii wakija watakusafisha tena kisha wataaiiba hata hiyo Bastola yako na wewe utakapoamka saa 4 asubuhi hutokuwa na wa kumlaumu...
Cha msingi chunguza kwa nini wanaoibiwa wooote wanaripoti huwa wanalala fofofoooo je ni nini kinafanyika mpaka mnapoteza fahamu?

Kununua Bastola na kufuga mbwa ni sawa na kuchimba mtaro ili maji yapite, lakini kufuatilia kwa nini mnalala mnapoibiwa ni kuziba maji pale yanapotoka...

Period
 
Pole sana mkuu, mi waliniliza mwaka jana mchana kweupe nikiwa namtumikia muajiri... hadi leo bado naugulia! Mungu yupo, 40 yao itafika tu ...

Mungu angekuwepo 40 ya hao mabingwa ingekuwa siku ile walipokuja kukusafishia Ghetto.

Lakini Mungu huyo aliewaona na kuwaacha wakwibe kwako kisha we still unampa chapuo ati iko 40 yao mi nakuona hauko timamu kichwani...

Sorry kama nimeandika kitu kitakukwaza...
 
Niliibiwa pia Oct mwaka jana flat screen, sony Brevia, laptop 3, na simu ( iphone), xbox na game zake. Maeneo ya Kilongawima....kuna wezi sana kule. Nina hasira sana na wezi nina bastola waje tena waona

Pole Mkuu! Nadhani wakija tena wataondoka na hiyo Basitola.
 
Poleni sana wakuu wangu. Ndiyo maana hakika wakikamatwa ni kiberiti tu.
 
I know,sisi wenyewe tulilala km tumekufa tumekuja kushtuka sa 1 na huwa tunaamka sa 11.hadi bedroom kwetu walifungua madirisha kwa nje wakavuta cm na vingine,laptop ilikua sitting room,yaani ukiona walivyovuruga!inaonekana walipania haswaa.kumbe kwa jirani yangu waliiba vitu kibao vya thamani wakamuachia na zigo la mavi sebuleni

Sasa hapo kwa jirani yako ndipo walitakiwa waingie chaka kwa wazee wa kazi na huo mzigo walioachiwa hapo sebleni, yaani vitu wangevipata kiulaiiiini...

Lakini kwa kuwa uzungu umewajaa hayo ndio matokeo.
 
Mungu angekuwepo 40 ya hao mabingwa ingekuwa siku ile walipokuja kukusafishia Ghetto.

Lakini Mungu huyo aliewaona na kuwaacha wakwibe kwako kisha we still unampa chapuo ati iko 40 yao mi nakuona hauko timamu kichwani...

Sorry kama nimeandika kitu kitakukwaza...

acha kufundisha watu uwoga . Kwangu juzi nimetandika wezi risasi tena ni baada ya mbwa kunishtua nikawawai . Mbwa anasaidia sana kukushtua mapema .
 
watu wanalalama tu ooh walipokuja nyumba nzima tukalala fofofoooo...
Wengine wanalalamika eti ooh Mbwa tunao na ni wakali kweli, lakini siku hiyo walibonyea na hawakufua dafu...

Pana nini hapa?
 
acha kufundisha watu uwoga . Kwangu juzi nimetandika wezi risasi tena ni baada ya mbwa kunishtua nikawawai . Mbwa anasaidia sana kukushtua mapema .

Bucho hongera sana ''bravo''...
Ila ninachokwambia mimi nielewe, hawa watu wanavyolalama it means kuna kitu kipo ndani yake.
tujadili hili swala kwa mapana zaidi, kwa nini watu wanalala wanapoibiwa?
 
Hawa jamaa naskia hupuliza dawa maana hata. walingia kwangu wala hawakuvunja na mpaka leo cjui walingiaje...na cjui kwa nin cktj hyo ckush2ka. Na c kawaida mim kuamka sa 4 asubuh mim huwa nakawaida kuamka mapema alfajiri.ila cku ya 2kio nlilakb fofofoo.

Aiseeh mbona unaandika kama form four ya ndalichako ?!
 
Naunga hoja mkono Gang Chomba

Nina uhakika safari hii wakija watakusafisha tena kisha wataaiiba hata hiyo Bastola yako na wewe utakapoamka saa 4 asubuhi hutokuwa na wa kumlaumu...
Cha msingi chunguza kwa nini wanaoibiwa wooote wanaripoti huwa wanalala fofofoooo je ni nini kinafanyika mpaka mnapoteza fahamu?

Kununua Bastola na kufuga mbwa ni sawa na kuchimba mtaro ili maji yapite, lakini kufuatilia kwa nini mnalala mnapoibiwa ni kuziba maji pale yanapotoka...

Period
 
Last edited by a moderator:
Sasa kali ni hii:
Mwizi aliingia kwenye nyumba halafu moja kwa moja akajificha juu ya dari. Sasa watu wakienda kazini anateremka chumba cha mzee kupitia chooni, ana sachi tena cash tu, kisha anarudi juu !
Zoezi kama la siku tatu hivi !
Mzee akampandishia mkewe kuwa anamsachi. Mke wacha aje juu ! Nyumba ikawa taf'rani, siku ya tatu mshikaji akateremka juu ya dari akamkuta house girl anatayarisha msomi wa mchana. Akamdhibiti kwa vibao kisha akapiga simu boda boda ikaja faster, jamaa akasepa kama na 5mn !
 
watu wanalalama tu ooh walipokuja nyumba nzima tukalala fofofoooo...
Wengine wanalalamika eti ooh Mbwa tunao na ni wakali kweli, lakini siku hiyo walibonyea na hawakufua dafu...

Pana nini hapa?

Sio kulalama mkuu,hata mi kabla haijanitokea nilikua siamini unaibiwaje usisikie,ila juzi ndo nikaamini.hata mbwa hatukumsikia wakati mtaa mzima wanajua huyu mbwa ni noma.na asbh tumemkuta mzima so hatujui walifanyaje hadi wakaruka ukuta wakaingia ndani wakapanda ghorofani wakasachi walivyoweza.inanitisha kwa upande mwingine kuwa wanaweza wakafanya kitu kibaya zaidi ya hicho,God forbid!
 
Ilikuwa naandka while naendesha gari.....sorry kama nmekukwaza
 
Sio kulalama mkuu,hata mi kabla haijanitokea nilikua siamini unaibiwaje usisikie,ila juzi ndo nikaamini.hata mbwa hatukumsikia wakati mtaa mzima wanajua huyu mbwa ni noma.na asbh tumemkuta mzima so hatujui walifanyaje hadi wakaruka ukuta wakaingia ndani wakapanda ghorofani wakasachi walivyoweza.inanitisha kwa upande mwingine kuwa wanaweza wakafanya kitu kibaya zaidi ya hicho,God forbid!

Sasa tulia kisha fanya uchunguzi yakinifu, inakuwaje jamaa wanaweza mtoka Mbwa, kisha wakapanda gorofani na kubeba walichofanikiwa?

Kwa Mbwa inabidi nikusaidie tu coz utasumbuka bila kupata jibu.
Hao wezi huwa wanajipaka mafuta ya Chatu ambayo yanapatikana tumboni.
Mafuta hayo ya chatu ni kiboko kwa Mbwa, hata awe mkali viipi akisikia harufu yake tu lazima atulie.
Mafuta hayo yanapatikana kwa gharama nafuu katika maduka ya kuuza dawa za asili.

Hilo swala la kulala fofofo sasa ndio nakuachia ulifanyie wewe kazi kisha utuletee jibu.

All in all hao mafala watawaibia nyinyi tu, mie kwangu hawathubutu kufika...

Gang Chomba.
 
Nna hasira nao sana!ntaua mtu nasema
mkuu yaani hawa watu walishaniumiza vibaya mno!! Machungu niliyo nayo siwezi simulia hapa!! Hata nikikuta wanauwa mwizi hapo siwezi kumwonea huruma hata kama ni ndugu yangu!!!
 
Back
Top Bottom