Kwa Tanzania hili ni tatizo ni kubwa sana, limekuwa kama sehemu ya utamaduni wetu.Nilisoma wiki iliyopita Eng Stella Manyanya akiwa anawasihi wanyakazi kuachana na hiyo tabia baada ya kupata malalamiko kutoka kwenye baadhi ya makampuni ya kujenga barabara.
Kwa mwajiri wizi na udokoaji una madhara makubwa sana,unapunguza ufanisi wa kampuni na wafanyakazi pia.Unakuta mfanyakazi kuwa na wazo la njia ya kujiongezea kipato ni kufanya kazi kwa bidii ili ajiweke kwenye nafasi nzuri ya kupandiswa cheo hatimaye mshahara kuongezeka ni kama halifikiriki