Wizi na udokoaji kazina una gharama kwa mwajiri?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Rafiki yangu mmoja huko Arusha ametimua karibu wafanyakazi wake wote akidai kuwa "wanamtia hasara". Nilipomuuliza kwa undani nni kinetokea sikuhitaji mifano mingi. Kilichomuudhi zaidi ni kuwa waliotakiwa kuwaangalia wa chini ndio walikuwa washiriki lakini wakati anawatimua ndio waliobembeleza zaidi!
 
Angalie upya maslahi ya hao wafanyakazi wake mkuu...wanafanya hivyo kwa kipato cha ziada labda mshiko mdogo
 
Husomeki kama umeanza kusimulia kuanzia mwanzo ama mwisho kuja mwanzo
 
Mwanakijiji leo umetuandikia kitu gani? mbona husomeki? au umeibiwa Password yako kama Nape?
 
Kwa Tanzania hili ni tatizo ni kubwa sana, limekuwa kama sehemu ya utamaduni wetu.Nilisoma wiki iliyopita Eng Stella Manyanya akiwa anawasihi wanyakazi kuachana na hiyo tabia baada ya kupata malalamiko kutoka kwenye baadhi ya makampuni ya kujenga barabara.

Kwa mwajiri wizi na udokoaji una madhara makubwa sana,unapunguza ufanisi wa kampuni na wafanyakazi pia.Unakuta mfanyakazi kuwa na wazo la njia ya kujiongezea kipato ni kufanya kazi kwa bidii ili ajiweke kwenye nafasi nzuri ya kupandiswa cheo hatimaye mshahara kuongezeka ni kama halifikiriki
 
kwa hiyo bora awatimue wote kuliko kuishi na watu wanaokutia presha kafanya bonge la decision kwani kuanza upya sio ujinga..
Kwenye SMEs unaweza kuwa unawatimua watu au kuwafunga kila siku lakini matokeo bado ni ziro.Kuna watu wamejaribu kuafanya hivyo matokeo yake wamejifukuzisha kazi wenyewe kwa kuua biashara. Njia ni kuwa one step head, kuziba mianya yote inayoweza kuwashawishi watu kudokoa au kuiba.

Kuna kampuni moja ya kujenga barabara walikuwa wanaibiwa tairi zao za spare walizokuwa wanazi hifadhi kwenye makontena, njia ya ilibidi wawe wanakutanisha kontena mbili ile sehemu ya milango ka kutumia wichi, iliwaongezea gharama lakini walifanikiwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom