Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,165
- 29,866
- Thread starter
- #61
UPDATEVODACOM wakiishiwa kwa tulio na simu na line zao wanaiba mchana kweupee..!
Hebu ona ujumbe nimetumiwa..
"Umetozwa Sh 100.0 TSH kwa ajili ya hadithi BABA NISAMEHE. Piga 0901767676 kuweza kusikiliza simulizi nzuri. Kujitoa tuma neno ONDOA kwenda 15460"
Hapo nipende nisipende nimekatwa shs 100 toka akaunti yangu ya m-pesa.
Halafu ukituma neno ONDOA kwenye namba waliyokupa, ujumbe hauendi maana wsmeublock, na wanaendelea kukukata pesa.
VODACOM wana wateja zaidi ya milioni 10. Hivyo kwa click moja wamekwapua bilioni moja toka kwa wateja wao.
Hata tukilalamika TCRA huwa hakuna action yoyote ya kurudisha hiyo 1b kwa wateja.
Kuna wana sheria humu, twawezaje kishitaki VODACOM kwa wizi huu?
Kulingana na mtandao na toleo la VODACOM, ina jumla ya wateja
Approximately 33.4 million
As of December 2025, Vodacom Tanzania has approximately 33.4 million total subscribers. This includes 19.0 million mobile data customers and 31.5 million M-Pesa subscribers.
Vodacom Tanzania
Wateja wa M -Pesa ni Milioni 31.5
Kwa hiyo kimsingi kwa kuwatoza Tshs 100 kila mmoja, wana kwapua kwa wakati mmoja Bilioni 3.15...!!!!
Huu ni wizi wa kutisha.