Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,454
- 872,087
Kuna hiki kitu WIZI, wizi ni kujitwalia kwa njia ya kificho kisicho chako kwa njia ya kukimiliki kukitumia au kukiuza ili upate chochote au ufaidike.
Kuna aina nyingi za wizi lakini leo nimechagua wizi huu wa aina hii ambao nimeuita wizi kichaa au wizi majnuni, ni wizi usio na faida yeyote kwa mwizi mwenyewe, ni wizi wa vitu vidogovidogo mno, ni wizi unaofanywa na watu wenye kipato na kazi zao nzuri tu.
Member mmoja hapa jamvini alikuja na post ya kuomba msaada, yeye ni mwizi wa chupi za wanawake anaotembea nao, akishaziiba hana kazi nazo tena anazirundika tu uvunguni mwa kitanda chake.
Tunao wengi wa jinsi hiyo kwenye Jamii yetu na hata hapa jamvini tunao, wezi wa vijiko na uma na glass kwenye sherehe, wezi wa tishu stick na mapambo, wezi wa scent balls kwenye vyoo..
Ukiwaangalia wote ni watu wasio na dhiki yoyote!
Mtu anaingia bar anaagiza chakula cha gharama tu akimaliza kula analetewa toothpick na napkin/tissue .... Kichekesho anachukua stick kadhaa na tissue kadhaa tena kwa kificho unakuta kwenye gari kajaza toothpick na tissue nyingi tu, kalamu za ofisi, pini, kalamu za kuazima benki TRA au kwenye ofisi za umma wao wanabeba tu.
Huu ni ugonjwa, ni aina fulani ya uchizi au wendawazimu unahitaji tiba ya kitabibu...Ukimuona mtu wa hivyo msaidie usimcheke wala kumlaumu, ana tatizo.