Wizi bandarini uliasisiwa na Mwinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi bandarini uliasisiwa na Mwinyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwikimbi, Sep 18, 2009.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  jamani wanajamii, jana na leo nilifanya ziara binafsi katika bandari ya dsm, na haswaa kujua kulikoni baada ya kuwasikia wakongo wanaopitisha mizigom yao hasa magari wakilalamika khusu wizi wa vifaa kunyofolewa kwenye magari yao, mliosikiliza bbc mlisikia aibu hii

  katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa, ulinzi pale bandarini ni very weak, yaani hamna polisi bali auxillary police ambao hawana uwezo hata wa kumshtaki mtuhumiwa, hawa mabwana wanalipwa mshahara wa juu sana around laki 6 kwa kima cha chini.lakini hawa watu wana-collude na wezi

  ilikuwaje? nimeambiwa kuwa , wakati mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani alianzisha msako katika bandari zetu na viwanja vya ndege kusaka biashara haramu, mtakumbuka kuwa aliwahi kukamata dhahabu zikitoroshwa pale airport na ikasemekana ilikuwa biashara ya mzee mwinyi na mkewe mama siti

  baada ya hapo ili kuendelea na huu ufisadi wa wakubwa, mwinyi alimuru askari wetu waondolowe kule bandarini na uwanja wa ndege na kuunda hawa wanaoitwa auxillary police kuficha ukweli

  kama jambo hili lisipoamngaliwa kwa makini wizi utakuwa maisha ya kawaida katika maeneo haya

  ikiwezekana ukwepo msukumo wa kuondoa hawa watu ili banadri zetu na viwanja vya ndege virudishiwe heshima yake
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi umewahi kusikia karibuni waingizaji madawa ya kulevya nchini wakikamatwa? Au tuseme biashara ya kupitisha madawa ya kulevya Bandarisalama imekauka?
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  nakubalina na wewe, ndo maana kinana aliweza kusafirisha zile pembe za ndovu mpaka zikaenda kukamatwa kule vietnan,

  ni vema wabunge wakafahamu hili, pale ni usanii mtupu pale bandarini
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Aliyekamata dhahabu ile airport alikuwa Mrema?..Jamani lini mtafikia kumpa sifa askari aliyeifanya kazi hiyo.. Mrema hakutoa amri wala kuanzisha kitu chochote ktk kukamata watu wenye biashara haramu. Ila ni ukweli usiopingika kwamba wakati wa Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani viwanda vyote viliibiwa parts zake na kuuzwa nchi jirani.Maradhio ya ATC, TRA, NBC na kadhalika yalianza pale na nakumbuka kuna kesi kibao za kodi na NBC toka mwaka huo zipo hadi leo hii..Ilifikia hadi magari ya Polisi yakiibiwa parts.. Kila Mtanzania alikuwa na fedha mfukoni - Ulikuwa mwaka wa neema katika kuangusha uchumi wa nchi yetu...Wizi na haramu zote zilikuwa RUKSA under his watch!
  Tunaikumbuka historia wakuu zangu..
   
 5. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  mkandara mpe mrema anachostahili hata kama hupendi.
   
 6. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Kuanzia karamagi na wote walio bandarini hasa tra ni wizi hakuna kanuni za malipo ya ushuru leo uki import gari utalipa milioni 3 kesho ki gari kama hicho lakini utalipishwa milioni 5 yaani ukimkuta afisa wa tra kagombana na mkewe huko nyumbani basi kistani na hasira zake anakumalizia wewe ili hali yeye hanufaiki na chochote kitu huku mwananchi wa kawaida unaumia ili hali mifisadi kna karamagi na wenzake wanafaidi nchi
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM hakuna asiekuwa mwizi ,etii akioza mmoja tunakubaliana kuwa wameoza wote ,kwa kilingo hicho ,CCM haifai kuwepo madarakani ,ni lazima wananchi na wapiga kura walio wengi waingie barabarani ili kuweka mambo sawa haswa kuiondoa TUME LA UCHAGUZI ,ambalo ndio mwega mmoja tu uliobakia kuipatia CCM ushindi wa "CHE".

  Kama hatukuamrisha wananchi waliowengi ambao ndio wapiga kura kuingia mabarabarani kwa misingi ya kutaka kuwepo na tume halali ambayo itasimamia kura zao ipasavyo basi tutakuwa hatuna la kufanya isipokuwa kuivumilia CCM tu.Mpaka kiyama.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  jifunzeni kuwa na heshima kwa viongozi wa taifa hasa waliostaafu,sio kuwa na tabia ya kuropoka matusi bila kuwa na ushahidi maalum,hebu na sisi waswahili tujifunze
  maana ya benefits of the doubts.......
  Mwinyi toka aondoke ni miaka mingapi imepita?????
  Nini kimemzuia mkapa na sasa kikwete kurekebisha tatizo hilo???
  Mangapi ya mwinyi yamebatlishwa?????
  Yaani wizi wa bandarini wa mwaka 2009 alaumiwe raisi aliemaliza kutawala 1995?????????hivi humu ndani
  mna matatizo ya kufikiri???????shame on u.
   
 9. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo tatizo lako hapo ni kuwa Mrema ndiyo kasifiwa? It doesn't click. Kila mafanikio ya nchi asifiwaye ni Rais. Na kila wizara ifanyapo vizuri asiwaye ni Waziri; au siyo?
   
 10. K

  Kinyikani Member

  #10
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuwa fisadi bila ya kuwa CCM wala huwezi kuwa CCM bila ya kuwa Fisadi
   
 11. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  unambandika mrema ruksa, lakini unajua ruksa lina mwenyewe
  naona unajidai uwelewi kwamba TZ askari wanapewa amri na wakubwa kwamba wakamate au wasikamate vitu
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli kama taifa tunatakiwa tujipange,

  inasikitisha sana kuona tunapakaziwa sifa mbaya nje na hii inaharibu sifa na haiba ya taifa letu pia inawza kuhatarisha ukuwaji wa uchumi wetu

  wahusika wachukue hatua zinazofaa haraka inavyowezekana
   
 13. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tumuacheni mzee Mwinyi apumzike, hayo yanayotokea sasa yanauhusiano gani na mwinyi? Kumbukeni Mwinyi ameitoa wapi nchi hii, wakati anaingia madarakani hata sabuni na mkate ulikuwa kwa foleni, nchi ilikuwa hakuwa na akiba ya mafuta kabisa, n.k. Mzee wa watu alifanya kazi nzuri sana. sina maana hakukuwa na mapungufu lakini wananchi wengi walipata neema.

  Wizi wa bandarini si ulinzi tu, bali wizi mkubwa unafanyika katika documents na wanao husika ni wafanyakazi wa ngazi ya juu wa bandari, TRA na Tscan.
   
 14. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kati ya Waziri wa mambo ya ndani tuliowahi kuwapata tangu Tanzania ipate uhuru wake nadhani MREMA alijitahidi kufanya MENGI mazuri zaidi kuliko wengine wooote
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Jamani, Mzee Mwinyi ni kweli alikuwa na weakness nyingi katika utawala wake. Mzee huyu alikuwa na strenghs zake ambazo tunatakiwa kuzi-recognise na vile vile weakness zake pia ambazo tayari some tumeshazizungumza hapa.

  Strengths:
  1. Alileta mapinduzi makubwa katika uhuru wa kujieleza hasa kuanzishwa kwa vyombo mbalimbali binafsi vya habari (ITV, CTN Magazeti binafsi yalizuka kama fungi)

  2. Alijitahidi kuruhusu ukiritimba wa ujamaa ambao ulileta madhara makubwa kiuchumi kama vile kumaliza njaa ya 1980s ilikuwa watu tunapanga foleni kununua mahindi kilo mbilimbili, tulikuwa tunagombania unga wa yanga na mbaazi zisizoiva tena unanunua kwenye tarafa yako tu.

  3. Uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi, kuwa raisi wa kwanza kuonesha njia ya kufuata misingi ya katiba katika kuongoza 10 years only wakati vinongozi wengi wa Africa walikuwa wanabadili katiba ili waendelee.

  Haya ni baadhi tu, Ila ikumbukwe kuwa utawala wa mzee Mwinyi ulikuwa ni mgumu sana, ukizingatia kuwa Nyerere alikuwa amemuweka kwenye darubini masaa 24, na alikosolewa sana na Nyerere lakini yeye alitumia busara kubwa kuzima malumbano hadharani.

  Weaknesses:
  1. Aliendekeza sana urafiki na wafanya biashara hasa wenye asili ya kiasia, kiasi kwamba alifikia mpaka kwenda kufungua majumba binafsi ya wafanyabiashara hawa, mfano (SAS wa Tanga alimualika kwenda kufungua nyumba yake ya kulala). Vitendo hivi viliwafanya watu hawa ambao ni wakwepa kodi wakubwa kui-exploit system kwa sababu ya uswahiba.

  2. Inasemekana alikuwa na washauri wabovu, na aliwasikiliza ndiyo maana hata makusanyo ya kodi yallishuka mpaka Tshs 20 billion kwa mwezi, six times less than expected.

  3. Kuruhusu wafanyakazi wa umma kujilimbikizia mali zaidi ya pato lao halisi, na kusababisha kukua kwa rushwa, kufumuka kwa bei na gap kati ya tajiri na masikini kuwa kubwa kupindukia.

  Note: Kubwa ninaloliona mimi ni kitendo chake cha kuminya demokrasia hasa Zanzibar kwa kukubali kuwa CUF wasitangazwe washindi japo walichaguliwa kule Zanzibar 1995, na kuendeleza msisitizo alipoombwa na Mkapa 2005 atoe maoni yake, ambapo alikataa vile vile. Hapa Naona amedumaza demokrasia yetu mpaka leo. Alikuwa na nafasi kubwa ya kupata Nobel prize kwenye hili akalitia maji.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  makubwa haya
   
Loading...