Wizara zinazofutwa hadharani

Wizara zinazofutwa hadharani

Nchi hii ilikuwa imeoza, Kikwete hakuwa mbaya hata kidogo, sema washauri wake ndo walikuwa wabaya, mpk tulikuwa na wazir asiyekuwa na wizara maalmu.
 
Kupunguza wizara 15 siyo mchezo. Wanaouliza pesa za elimu zitatoka wapi hawakuyajuwa haya. Nadhani tutaheshimiana tuu. Eti kuna watumishi walikuwa hawauhesabu mshahara wanakula posho tuu. Maguuuuuu! Bado Tanesco.[/QUOTtowE]

Mkuu hapo tanesco hawezi kufanya kitu zaidi labda aende wizarani na sio tanesco, tanesco hatoweza kupunguza chochote labda amtimue mtu na kumuweka mwingine lakini sio kupunguza kitu. Tatizo unaloliona tanesco si la tanesco mzizi wa tatizo ni wizarani, tanesco ni kama watolewa kafara tu au wabebeshwa mizigo ya lawama tu
 
sasa hapo atakuwa ameongeza ajira au amepunguza ajira? watu wengi wanashindwa kufikiri na nini maana ya kuongeza ajira
 
Nchi hii ilikuwa imeoza, Kikwete hakuwa mbaya hata kidogo, sema washauri wake ndo walikuwa wabaya, mpk tulikuwa na wazir asiyekuwa na wizara maalmu.

ndugu, SIYO WASHAURI, bali WALIOMSAIDIA (toka 1995 hadi 2005), kuwa Raisi na Mrajisi wa vyeo...
 
Wizara ya Michezo iwe peke yake iwe kama wizara ya fedha, wizara ya maji yaani michezo iwe na wizara ya pekee isichanganywe na vitu vingine kabsa. Hii itasaidia michezo kukua kwa kasi kubwa.

Achanganye tu... Michezo si priority ya kwanza kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chochote hapa nchini.
Afu michezo wala hata haiajiri watu wengi sana kilivyo ukilinganisha na sekta kama ya sanaa.
 
Ivi kwanini magufuli hafuti sherehe za Christimas? hizi sherehe ata kwenye kitabu cha biblia haziko ata wakiristo wenyewe hawana fatwa yeyote kuhusu kuzaliwa yesu ni mambo ya kupanga tu.

Zile sherehe watu wanazalishana nje, maradhi na kushikana shiakana kule kanisani bure hazina tija yeyote, watu wanalewa sana wanapiga mziki wanahemkwa kule makanisani fedha nyinzi zinapotea bila faida yeyote.
 
Watendaji waliokuwa waajiriwa wa wizara hizo itakuwaje??? Najaribu tu kupiga picha ya kitakachojiri. Mfano mtu aliye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo...sijui atapelekwa Idara ya Habari Maelezo, ama BMT ama Idara ya Utamaduni huko Halmashauri??? Wale wa Mazingira pale kwa Makamu wa Rais nao vipi????

Japo kuna tija katika kuzipunguza ila kwa watumishi walioko katika hizo Wizara nadhani matumbo joto.

Mkuu ni mawaziri tu ndo hawatakuwepo, wafanyakazi hawapunguzwi
 
Acheni ujinga huu Mwanasiasa waAFRICA usimuapie badae akivurunda mtaona aibu wee shukuru kama anafanya yale tunayotaka lkn kusema mambo kama hayo ni Ujinga

Na ni kweli.

NAkumbuka Kikwete aipoanza mwanzoni watu walisema ni CHAGUO LA MUNGU; baadaye alipovurunda wale wale waliosema CHAGUO LA MUNGU wakabadilika na kusema ni CHAGUO LA JIRANI YAKE MUNGU.
Hhahahahahahahahahahahah!!!!!!

Yatubidi kufanya subira na hakuna sababu ya kumkweza kwani anafanya kazi tuliyomtuma ndio maana tulipoteza siku nzima kupanga foleni ya kuandikisha na siku nzima kupanga foleni ya kupiga kura.
 
Actually hapo watakaopungua ni Mawaziri na Manaibu waziri. Hao watumishi wengine watabaki hapo kama sekta fulani au watapangiwa kazi nyingine, na salary kama kawaida

Hivi unajua sababu ya kupunguza "baraza la mawaziri"??!!!
Hao wafanyakazi watapangiwa majukumu mengine. . . .. . . .
 
Mi nafikiri itakuwa kama ilivyofanya wizara ya viwinda biashara na masoko kipindi hicho, baadae ikawa ikawa ni wizara ya viwanda na biashara, ile masoko ikawa idara na watendaji wake wanaendelea kama kawaida.
Hata hii itakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom