John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taarifa iliyotolewa na mtandao wa Tanzania Times, tarehe 3 Machi, 2022 ikieleza kuonekana kwa faru mweusi katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.
Wizara imeeleza kuwa taarifa hiyo ambayo inaendelea kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii siyo sahihi na wanaomba ipuuzwe. Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo.
Aidha, Wizara imesisitiza kuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya wanyampori hapa nchini ikiwemo utoaji wa takwimu na taarifa za wanyamapori kwa umma ni Wizara ya Maliasili na Utalii na si vinginevyo.