Wizara ya Nishati na Tanesco tuambieni gharama mtakazotumia kuzalisha Megawatt 2000 za Umeme kwenye Ubia na Kampuni ya UAE

Kamati ya Bunge ya Nishati ilitutangazia bungeni kuwa Mradi umechelewa, juzi tumeambiwa umefikia asilimia 67 kutoka 53.25 ya Disemba 2021 sasa leo ni Agosti 2022 karibu mwaka mzima unaambiwa imeongezeka asilimia 14 alafu unaleta ngonjera zako hapa
Kiukweli wewe ni taahira,umeelewa mada?
 
Nimekujibu wewe uliosema mradi uko asilimia 67 ndio nikakupa taarifa za Bunge kwamba mradi kufikia Disemba 2021 ulikuwa Asilimia 53.25 ndio ujue taarifa mnazoletewa mjiridhishe na zilizowahi kutolewa bungeni
Shida hapo ni ipi hasa? Mradi ndio uko 67% kutoka hiyo 53%
 
Bwawa hawalitaki, lakini hawana jinsi ya kuliacha,
Watanzania hawatawaelewa ndio maana wanaendelea kidogo kidogo,
Kuna crane Makamba alituambia inatoka nje ya nchi kuinua mlango bwawa kwani ilishafika?
Tunaomba bwawa liishe tupate umeme wa bei nafuu kidogo, pengine italeta nafuu kwenye uzalishaji, inaweza kupunguza mfumuko wa bei kidogo,
Saivi Jamani wajanja aka born town tupo lazima tupige hela kupitia tanesco Mana Kuna Ile kontract ya software tokea india.
Na hii Kuna per zetu jamani hebu tuachane. Wazeee wetu waliumia kuweka njia nzuri kwa sie wakati wa kwenu walikuwa wanachunga ng'ombe,kucheza ngoma,kuongeza wake wengi akili zao ziliishia hapohapo. Acheni kwanza tuwanyonye ili akili ziwakae sawa.
Nahitaji Niwe na mijengo kadhaa huko Paris , Sidney,London , Washington nyie endeleeni kuumia Ila ndio ivyo tunazidi kutengeneza ulaini wa kula kwa kizazi chetu. Si unaona washamba na malimbukeni,wachunga ng'ombe na wacheza ngoma hawakaii madarakani Wana bana sana. Saivi Ni ishu ya kamba yako na wewe itafute
 
Hatua za mwanzo ndio ngumu ila zinazofuatia sio ngumu kihivyo..

Mradi unatakiwa kukamilika 2025.
Kwa mujibu wa Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni inayojenga mradi ulitakiwa ukamilike Juni 15, 2022 hayo mabadiliko unayosema wewe umeyatoa kwenye chanzo gani cha taarifa?
 
Kwa iyo inamaanisha bwawa likizinduliwa kutakua na zaid ya megawatts 5000? Sidhan kama nchi tutakua na matumizi nazo zote izo wakat hakuna viwanda vyovyote vya maana.. wangemaliza ilo bwawa kwanza kwani lina megawatt nyingi za kutosha kabla ya kuingia uo ubia bila kujua izo zingine tutazipeleka wap
 
Bwawa hawalitaki, lakini hawana jinsi ya kuliacha,
Watanzania hawatawaelewa ndio maana wanaendelea kidogo kidogo,
Kuna crane Makamba alituambia inatoka nje ya nchi kuinua mlango bwawa kwani ilishafika?
Tunaomba bwawa liishe tupate umeme wa bei nafuu kidogo, pengine italeta nafuu kwenye uzalishaji, inaweza kupunguza mfumuko wa bei kidogo,
Watanzania gani ambao unasema hawataelewa? Halafu hata wasipowaelewa watafanya nini?
 
Kwa mujibu wa Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni inayojenga mradi ulitakiwa ukamilike Juni 15, 2022 hayo mabadiliko unayosema wewe umeyatoa kwenye chanzo gani cha taarifa?
Sababu za kutokamilika hiyo June zikielezwa ndio maana ya kuwa na revised completion date,so hakuna hoja hapo.
 
Umeme uliopo unazidi matumizi
Tanesco wanasema Nchi haipati wawekezaji wakubwa kwa sababu hatuna umeme,wanasema mfano Ili kuchimba na kuyeyusha chuma kule liganga zinahitajika megawatt 1000 hivyo tukipata megawatt walau 5,000 by 2025 tunaweza pata wawekezaji wa miradi mikubwa zaidi.
 
Kwa iyo inamaanisha bwawa likizinduliwa kutakua na zaid ya megawatts 5000? Sidhan kama nchi tutakua na matumizi nazo zote izo wakat hakuna viwanda vyovyote vya maana.. wangemaliza ilo bwawa kwanza kwani lina megawatt nyingi za kutosha kabla ya kuingia uo ubia bila kujua izo zingine tutazipeleka wap
Uchumi unakua,ziada haiwezi kuwa kubwa hivyo.
 
Kwa mujibu wa Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni inayojenga mradi ulitakiwa ukamilike Juni 15, 2022 hayo mabadiliko unayosema wewe umeyatoa kwenye chanzo gani cha taarifa?
Una matatizo wewe,taarifa za serikali zinasemaje? Angalia kwenye bajeti au taarifa specific za huo mradi.
 
Habari Wana jamvi..

Wizara ya Nishati kupitia Tanesco wameingia Makubaliano ya Ubia wa kuzalisha umeme wa Nishati jadidifu kiasi cha megawatt 2,000 ifikapo 2024 na Kampuni ya Kutoka Taifa la Arabuni la UAE..

Katika ubia wao hawajasema watazalisha kwa gharama kiasi gani.Ni muhimu tujue gharama Ili tuweze kulinganisha na gharama za kuzalisha megawatt 2115 za Bwawa la Mwl.Nyerere.,

Hii ni muhimu kwa sababu za kihistoria kwenye hiyo wizara kitumika kufanya upigaji wa pesa za Umma,hivyo Tanesco na Wizara kupitia Waziri Makamba ni vyema waje kuweka wazi hili.👇
Tanvu mwaka 1991 hadi TANESCO imekuwa conduit ya kuiba fedha za umma kwa visinguzio mbalimbali and it will continue ti be so for foreseable future.
 
Bwashee ni wewe mwenyewe, au akaunti yako imehakiwa?
Badala ya kuimba pambio za kushangilia mafanikio ya awamu ya 6, umeanza kuhoji? Hata siamini!
 
Tanesco wanasema Nchi haipati wawekezaji wakubwa kwa sababu hatuna umeme,wanasema mfano Ili kuchimba na kuyeyusha chuma kule liganga zinahitajika megawatt 1000 hivyo tukipata megawatt walau 5,000 by 2025 tunaweza pata wawekezaji wa miradi mikubwa zaidi.
Story za liganga za kitambo Sana,tangu jakaya..na uwekezaji ulikua njiani,tukaona na mirambo mikubwa ikiingia,umeme ulikua kiwango hiki hiki
 
Back
Top Bottom