Wizara ya Maji yaidhinishiwa na Bunge la Tanzania jumla ya Bajeti ya Shilingi 627,778,338,000

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
846
WIZARA YA MAJI KUANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA GRIDI YA TAIFA YA MAJI - WAZIRI AWESO

Abainisha kuwa wizara imefanikiwa kukwamua miradi 157 kati ya miradi 177 ya maji vijijini iliyokuwa na changamoto ya kutokukamilika kwa muda mrefu.

Waziri wa Maji Nchini Mhe. Jumaa Aweso amesema Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeanza utekelezaji wa mkakati wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito mabwawa kwa ajili ya kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya uhakika.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 Bungeni Dodoma leo tarehe 9 Mei, 2024 , Waziri Aweso ametolea mfano wa utekelezaji wa Gridi ya Taifa ya Maji ambapo amesema mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria umenufaisha miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga na Shelui pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka kwenye bomba kuu.

Pia ametolea mfano mradi wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kupeleka kwenye mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ambapo upo kwenye hatua ya usanifu.

Vilevile, Waziri Aweso amesema wizara hiyo imeanza utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati ikiwemo mabwawa ya Kidunda na Farkwa pamoja na Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi - Simiyu.

Aidha, Aweso ameongeza kuwa Wizara imefanikiwa kukwamua miradi 157 kati ya miradi 177 ya maji vijijini iliyokuwa na changamoto ya kutokukamilika kwa muda mrefu.

Sambamba na hayo, Waziri Aweso amebainisha kuwa Wizara hiyo imefanikisha kuanzishwa kwa Consultancy Bureau katika Chuo Cha Maji inayosaidia kutoa huduma za ushauri elekezi kwenye sekta ya maji na sekta nyinginezi ikiwa ni pamoja na uandaaji na usimamizi wa miradi pamoja na kuwajengea uwezo Vijana wanaohitimu masomo na kusaidia kuongeza mapato ya Taasisi.

Uwasilishaji wa Makadirio ya Bajeti
Wizara Ya Maji 2024/2025
KaziIendelee.
=====

UPDATES;

=====

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania laridhia kwa kishindo na asilimia mia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa kuidhinisha jumla ya Shilingi 627,778,338,000 kwenda kutekeleza kazi na shughuli mbalimbali za Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2015 leo tarehe 10 Mei 2024.

SOMA HAPA HOTUBA KAMILI
IMG-20240509-WA0105(2).jpg

HOTUBA YA WAZIRI WA MAJI MHE. JUMAA

HAMIDU AWESO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA MAJI KWA MWAKA 2024/25

1. UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika
, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira,

Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga (Mb) kuwasilisha taarifa ya Kamati iliyochambua utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka 2023/24 na kupokelewa na Bunge lako Tukufu, ninaomba sasa kutoa hoja kwamba, Bunge lako likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2024/25.


Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutupatia afya njema na kutuwezesha kukutana kwa siku ya leo. Aidha, kwa moyo wa unyenyekevu mkubwa ninamuomba Mwenyezi Mungu atujalie busara, hekima na kutuongoza vema wakati wa kujadili wasilisho la hotuba yangu pamoja na bajeti kuu ya Serikali kwa nia thabiti ya kujenga taifa letu na kuendeleza ustawi wa wananchi wetu.


Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee na dhamira ya dhati ya moyo wangu napenda kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi imara, madhubuti na wa vitendo aliotuonesha katika

1​


kipindi cha miaka mitatu chini ya Serikali yake ya Awamu ya Sita. Mheshimiwa Rais ameonesha uongozi mahiri unaojali shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


Mheshimiwa Spika, katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, sote tumeendelea kushuhudia utumishi wenye kujali utu wa watu na kujenga nchi yetu kwa pamoja kupitia falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahilimivu, Mageuzi na Kujenga upya Taifa letu) iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais. Aidha, Mheshimiwa Rais ameendelea kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya nchi yetu na nchi nyingine pamoja na taasisi na jumuiya za kimataifa na hivyo, kung’arisha taswira ya nchi yetu kwenye anga za kimataifa na kufungua fursa mbalimbali za maendeleo. Hakika sote tunapaswa kumshukuru Mheshimiwa Rais na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, amzidishie busara na hekima ili aweze kuendelea kutekeleza majukumu yake.




Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini katika nafasi hii ya Waziri wa Maji. Heshima na imani niliyopewa na Mheshimiwa Rais ni kubwa sana, ninaahidi kupitia Bunge lako Tukufu kuwa nitaitumikia nafasi hii kwa uadilifu na uaminifu mkubwa, na kwa uwezo wangu wote ili kuhakikisha matarajio na imani yake kwangu yanafikiwa; na muhimu zaidi ni

2​


kuhakikisha huduma ya maji safi, salama na ya kutosheleza inawafikia wananchi wote wa vijijini na mijini.


Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango kwa kazi kubwa anayoifanya katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuijenga Tanzania kuwa nchi yenye uchumi shindani.


Mheshimiwa Spika, vilevile, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), kwa uongozi wake mahiri, ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusimamia kikamilifu uwajibikaji wa viongozi na watumishi mbalimbali serikalini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na wanayostahili. Sote

tumekuwa tukishuhudia na kuona namna anavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu akiwa ndani na nje ya Bunge.


Mheshimiwa Spika, naomba pia kumshukuru Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb) kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia wananchi. Usimamizi na maelekezo yake yamekuwa ni chachu katika utendaji wa Serikali na maendeleo ya taifa kwa ujumla.


Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru Spika

3​


wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu (Mb), kwa uongozi mahiri wa kuliongoza Bunge letu Tukufu. Aidha, naomba kutoa pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU) na kutengeneza historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuchaguliwa kutumikia nafasi hiyo. Kuchaguliwa kwako kwa nafasi hiyo ya juu na yenye ushawishi mkubwa duniani ni uthibitisho wa kutosha kuhusu umahiri na weledi wako katika kutekeleza majukumu yako na kwa hakika umeijengea heshima kubwa nchi yetu. Vilevile, naomba niwapongeze Wenyeviti wa Bunge, Mheshimiwa Najma Murtaza

Giga (Mb), Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika (Mb) na Mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama

(Mb)
kwa kazi nzuri wanazozifanya kwenye Bunge letu Tukufu. Pia, natoa pongezi kubwa kwa wabunge wote kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwatumikia wananchi na ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu yangu kwenye maeneo yao.


Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti,

Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira
kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya sekta ya maji. Kamati imefanya kazi kubwa ya kuchambua Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti

4​


ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2024/25. Maoni na ushauri uliotolewa na Kamati umetusaidia wakati wa maandalizi ya bajeti ya Wizara yangu. Napenda kuiahidi Kamati kuwa tutaendelea kutoa ushirikiano, kupokea maoni na ushauri wao na kuufanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya maji.

Mheshimiwa Spika, natoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waheshimiwa Wabunge, familia za marehemu pamoja na Watanzania wote kwa vifo vya wapendwa wetu Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Hayati Edward Ngoyai Lowasa, Waziri Mkuu Mstaafu. Vilevile, naomba kutoa pole kwako wewe Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu, familia za marehemu, ndugu na wananchi wa majimbo ya Mbarali na Kwahani kwa vifo vya Mheshimiwa Francis Leonard Mtega aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali na Mheshimiwa Ahmed Yahya Abdulwakil aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.


Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pole kwa wananchi wa Wilaya za Hanang’, Rufiji, Arusha pamoja na maeneo mbalimbali nchini walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua za Elinino. Mafuriko hayo yamesababisha madhara makubwa kwa taifa ikiwemo watu kupoteza maisha, majeruhi, uharibifu wa mali na

miundombinu ya barabara, umeme, maji na kadhia

5​


nyingine mbalimbali. Aidha, niwashukuru wadau wote walioshiriki na wanaoendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa misaada mbalimbali ya kusaidia wananchi walioathirika na maafa ya mafuriko hayo.


Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii, kumshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kwa hotuba yake aliyoiwasilisha hapa Bungeni kwa umahiri wa hali ya juu. Hotuba hiyo, imetoa dira na mwelekeo wa utekelezaji wa kazi za Serikali. Vilevile, hotuba hiyo imeelezea mapitio ya uendeshaji wa shughuli za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha mwaka 2023/24 pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2020 – 2025). Aidha, nawapongeza Mawaziri wenzangu wote walionitangulia kuwasilisha hoja zao na Wabunge waliochangia hoja hizo.


Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara yangu umezingatia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 - 2025/26); Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2020 – 2025); Sera na Mikakati ya Maendeleo ya Kitaifa na Kimataifa; Sheria, Kanuni na Miongozo pamoja na maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge na wadau mbalimbali.


Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, napenda sasa kuchukua fursa hii kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara yangu yenye sehemu kuu tano (5) kama ifuatavyo:- Hali ya Sekta ya Maji nchini;

6​


Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/24; Mafanikio yaliyopatikana; Changamoto na Hatua zilizochukuliwa; na Mpango na Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2024/25.

2. HALI YA SEKTA YA MAJI NCHINI


Mheshimiwa Spika
, naomba nichukue fursa hii kuelezea hali ya Sekta ya Maji nchini inayojumuisha hali ya rasilimali za maji, ubora wa maji na upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini na mijini kama ifuatavyo:-


2.1. Hali ya Rasilimali za Maji


Mheshimiwa Spika
, nchi yetu inakadiriwa kuwa na rasilimali za maji zinazofaa kwa matumizi mbalimbali za wastani wa mita za ujazo bilioni 126 kwa mwaka. Kiasi hicho kinahusisha maji juu ya ardhi mita za ujazo bilioni 105 na maji chini ya ardhi mita za ujazo bilioni

kwa mwaka. Kwa idadi ya watu milioni 59.8 wa Tanzania Bara kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, inaonesha kuwa kiasi cha maji kilichopo kwa kila mtu kwa mwaka ni takribani wastani wa mita za ujazo 2,105. Kiasi hicho kipo juu ya kiwango cha chini cha mita za ujazo 1,700 cha mahitaji ya maji kwa mtu kwa mwaka kinachokubalika kimataifa. Hali hiyo, inaonesha kuwa nchi yetu ipo juu ya kiwango cha uhaba wa maji (water stress). Hata hivyo, kutokana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa vyanzo vya maji unaosababishwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii zisizokuwa endelevu, kiwango hicho kinaweza kupungua hadi kufikia mita za ujazo 883 kwa mtu ifikapo

7​


mwaka 2035 endapo hatua stahiki hazitachukuliwa. Hivyo, kuna umuhimu wa kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda rasilimali za maji.




Mheshimiwa Spika, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa katika mwaka 2023, mahitaji ya maji kwa sekta mbalimbali nchini yalikuwa wastani wa mita za ujazo bilioni 64. Inakadiriwa mahitaji hayo yataongezeka hadi kufikia wastani wa mita za ujazo bilioni 80.2 kwa mwaka ifikapo mwaka 2035. Kwa kuzingatia kiasi cha rasilimali za maji zilizopo, nchi yetu ina kiasi cha kutosha cha rasilimali za maji zinazoweza kukidhi mahitaji ya maji kwa sekta mbalimbali. Hata hivyo, kutokana na mwenendo wa kuongezeka kwa mahitaji ya maji kunakosababishwa na ongezeko la watu pamoja na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, Serikali itaendelea kuwekeza katika utunzaji wa vyanzo vya maji, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuboresha ufanisi katika matumizi ya maji kwa lengo la kuepusha nchi yetu kuwa na uhaba wa maji.


Mheshimiwa Spika, wastani wa kiwango cha mvua nchini katika mwaka wa kihaidrolojia wa Novemba 2022 – Oktoba 2023 ulikuwa milimita 1200. Kiwango hicho hutofautiana katika maeneo mbalimbali kutokana na tabia tofauti za hali ya hewa. Maeneo ya nyanda za juu kusini yalipata mvua za wastani wa milimita 800 hadi 1700, ukanda wa kaskazini milimita 600 hadi 1600, ukanda wa pwani milimita 650 hadi 1200 na ukanda wa magharibi milimita 500 hadi 1300. Vilevile, katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2023 hadi Aprili, 2024

8​


kumekuwa na mvua za El-nino na mvua za masika ambazo zimekuwa juu ya wastani ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita. Kutokana na mvua hizo, kwa ujumla hali ya maji katika vyanzo vya maji imekuwa juu ya wastani na kusababisha mito, mabwawa na maziwa kujaa maji na maeneo mengine kupata mafuriko.


2.2. Hali ya Ubora wa Maji


Mheshimiwa Spika
, ubora wa maji katika vyanzo vya maji hutofautiana kulingana na jiografia, tabianchi na mabadiliko ya tabianchi, shughuli za kibinadam na hali ya miamba. Takwimu zinaonesha hali ya ubora wa maji kwenye vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi inawezesha ustawi wa ikolojia na hivyo vinaweza kuendelezwa kwa matumizi ya sekta mbalimbali. Pamoja na hali hiyo ya ubora wa maji, bado kunahitajika jitihada za pamoja za kuzuia uchafuzi na pia, kurejesha na kuimarisha ubora wa maji wa asili katika vyanzo vya maji.


Mheshimiwa Spika, maji yanayosambazwa vijijini na mijini yameendelea kukidhi viwango vya kitaifa vya ubora wa maji ya kunywa hivyo, kulinda afya ya jamii kwa ujumla. Hali hii inatokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa kushirikina na wadau mbalimbali katika ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kutibu maji pamoja na usimamizi na udhibiti wa ubora wa maji katika mifumo ya usambazaji maji kuanzia kwenye vyanzo hadi kwa watumiaji.






9​


2.3. Hali ya Upatikanaji wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini

Mheshimiwa Spika
, Serikali ina azma ya kuhakikisha wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanapata huduma bora na endelevu ya maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imeendelea na jitihada za kujenga na kukarabati miradi ya maji pamoja na kupanua mitandao ya kusambaza maji na kuimarisha usimamizi wa huduma ya maji vijijini. Jitihada hizo zimewezesha kuongezeka kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kutoka wastani wa asilimia 77 mwezi Desemba, 2022 hadi kufikia wastani wa asilimia 79.6 mwezi Desemba, 2023. Kiwango kilichoongezeka kimetokana na kutekelezwa kwa miradi 632 yenye vituo vya kuchotea 7,956 vyenye uwezo wa kuhudumia wananchi 4,740,959. Hali hiyo, inafanya jumla ya wananchi wa vijijini wanaopata huduma ya maji kufikia 34,950,368 kati ya wananchi 39,232,999 waishio vijijini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.




Mheshimiwa Spika, kwa upande wa usafi wa mazingira, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Afya imeendelea kutekeleza Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kwenye maeneo ya vijijini. Kupitia Kampeni hiyo, elimu kuhusu umuhimu wa usafi wa mtu binafsi imeendelea kutolewa na vyoo vya mfano na miundombinu ya kunawia mikono imejengwa kwenye shule na zahanati. Kampeni hiyo imekuwa na matokeo

chanya ambapo kwa sasa zaidi ya asilimia 97 ya

10​

wananchi vijijini wanatumia vyoo vya msingi.


2.4. Hali ya Upatikanaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miradi ya maji. Lengo ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025. Hadi mwezi Desemba 2023, upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya mijini umefikia wastani wa asilimia 90 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 88 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Ongezeko hilo limetokana na kukamilika kwa miradi 85 ya maji inayohudumia wakazi 4,641,505 wa maeneo ya mijini.


Mheshimiwa Spika, kwa upande wa huduma ya uondoshaji majitaka, Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya majitaka kwenye maeneo mbalimbali nchini. Hadi mwezi Aprili 2024, mtandao wa majitaka umefikia kilomita 1,455.93 ikilinganishwa na kilomita 1,416.9 za mwezi Aprili 2023. Vilevile, idadi ya wateja waliounganishwa katika mtandao imefikia 58,650 kutoka wateja 56,923 katika kipindi hicho. Kwa maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa majitaka, huduma ya uondoshaji majitaka hutolewa na magari maalum ya majitaka ambayo huyapeleka kwenye mabwawa ya majitaka kwa ajili ya kusafishwa na kutibiwa.

11​


MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

3.1. Upatikanaji wa Fedha


Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2023/24, Fungu

– Wizara ya Maji liliidhinishiwa jumla ya Shilingi 756,205,106,000.00. Kati ya fedha hizo Shilingi 60,375,474,000.00 zilikuwa ni fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi 695,829,632,000.00 zilikuwa ni fedha za maendeleo. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imepokea jumla ya Shilingi 639,485,602,279.06 sawa na asilimia 84.6 ya bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha zilizopokelewa, Shilingi 593,398,121,378.53 ni za kutekeleza miradi ya maendeleo na Shilingi 46,087,480,900.53 ni za matumizi ya kawaida.

3.1.1. Bajeti ya Matumizi ya Kawaida


Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2023/24, Wizara ya Maji - Fungu 49 ilitengewa jumla ya Shilingi 60,375,474,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 42,339,913,000.00 ni kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara, RUWASA na Chuo cha Maji na Shilingi 18,035,561,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo. Hadi mwezi Aprili, 2024 jumla ya Shilingi 46,087,480,900.53 sawa na asilimia 76.3 ya fedha zilizoidhinishwa zimetolewa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 36,527,791,160.00 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi na Shilingi 9,559,689,740.53 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.


12​

3.1.2. Bajeti ya Miradi ya Maendeleo


Mheshimiwa Spika
, kwa upande wa miradi ya maendeleo, katika mwaka 2023/24, Wizara ya Maji - Fungu 49 ilitengewa Shilingi 695,829,632,000.00. Kati ya fedha hizo Shilingi 407,064,860,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 288,764,772,000.00 ni fedha za nje. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imepokea jumla ya Shilingi 593,398,121,378.53 sawa na asilimia 85.3 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya fedha zilizopokelewa, Shilingi 356,910,567,637.62 ni fedha za ndani zilizoidhinishwa na Shilingi 236,487,553,740.91 ni fedha za nje zilizoidhinishwa.

3.2. Utekelezaji wa Programu na Miradi Mbalimbali ya Maji

Mheshimiwa Spika
, miradi ya maji inatekelezwa kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ipo katika Awamu ya Tatu inayotekelezwa kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2025/26. Utekelezaji katika mwaka 2023/24 umeainishwa katika maeneo ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji, huduma za ubora wa maji, huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini na mijini; na kazi mbalimbali zinazotekelezwa katika Taasisi chini ya Wizara pamoja na masuala mtambuka.

3.2.1. Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji

29. Mheshimiwa Spika, usimamizi na uendelezaji wa

13​


rasilimali za maji nchini unatekelezwa kupitia Bodi za Maji za Mabonde tisa (9) ambazo zimepewa majukumu yakufanya tathmini na ufuatiliaji wa rasilimali hizo; kuhifadhi na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji; kugawa maji kwa sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji na kiasi cha maji kilichopo; na kuendeleza rasilimali za maji.

3.2.1.1. Usimamizi wa Rasilimali za Maji


Mheshimiwa Spika
, usimamizi wa rasilimali za maji unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji, udhibiti wa matumizi ya maji na migogoro, udhibiti wa ujenzi na usajili wa mabwawa, udhibiti wa uchimbaji wa visima, ulinzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuzuia uchafuzi wa vyanzo. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa katika eneo la usimamizi wa rasilimali za maji ni kama ifuatavyo:-

Tathmini na Ufuatiliaji wa Rasilimali za Maji


Ujenzi na Ukarabati wa Vituo vya Kufuatilia Mwenendo wa Rasilimali za Maji

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Bodi za Maji za Mabonde imeendelea kufanya ukarabati na kujenga vituo vipya vya kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji ili kuhakikisha takwimu sahihi na za uhakika za rasilimali za maji zinapatikana. Takwimu hizo hutumika katika kufanya maamuzi ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo inayohusiana na maji ikiwemo miradi ya usambazaji maji, ujenzi wa mabwawa ya kufua umeme

14​


na miradi ya umwagiliaji. Hadi mwezi Aprili 2024, vituo 51 vimekarabatiwa na vituo 11 vimejengwa hivyo, kuwa na jumla ya vituo 1,276. Kati ya vituo hivyo, vituo 187 ni vya kufuatilia mwenendo wa mvua, vituo 129 vya kufuatilia hali ya hewa, vituo 318 vya kufuatilia mtiririko wa maji kwenye mito, vituo 18 vya kufuatilia kina cha maji ya maziwa, vituo 15 vya kufuatilia kina cha maji katika mabwawa, vituo 60 vya kufuatilia kiasi cha mashapo (sediments) katika mito, vituo 112 vya kufuatilia mwenendo wa maji chini ya ardhi na vituo 437 vya kufuatilia ubora wa maji. Kiambatisho Na. 1 kinaonesha utekelezaji wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji hadi mwezi Aprili, 2024.


Udhibiti wa Matumizi ya Maji na Migogoro


Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kusimamia matumizi bora ya rasilimali za maji na kudhibiti migogoro inayojitokeza kwa kutoa elimu kuhusu sheria na kanuni za usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji pamoja na kuchukua hatua mbalimbali kunapotokea ukiukwaji wa sheria. Aidha, udhibiti huo unalenga kuhakikisha uwepo wa matumizi sawia ya maji kulingana na mahitaji na upatikanaji wa rasilimali hiyo. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara kupitia Bodi za Maji za Mabonde imetoa vibali vipya 948 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya maji hivyo, kuwa na jumla ya vibali 13,260 vya matumizi ya maji vilivyotolewa. Takwimu hizo za vibali zinasaidia kujua kiasi cha maji kwa matumizi ya sekta mbalimbali za kiuchumi. Aidha, hadi mwezi Aprili 2024, migogoro 23 kati ya 28 ya matumizi ya maji ilitatuliwa. Migogoro

15​

iliyobaki ipo katika hatua mbalimbali za utatuzi.


Udhibiti wa Ujenzi na Usajili wa Mabwawa


Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusajili, kudhibiti ujenzi na usalama wa miundombinu ya mabwawa ya maji na mabwawa ya topesumu kwa kutoa vibali vya ujenzi na miongozo ya matumizi na usalama wa mabwawa. Hadi mwezi Aprili 2024, vibali vinne (4) vya ujenzi wa mabwawa ya maji vimetolewa na mabwawa mawili (2) yaliyokidhi vigezo vya usalama wa mabwawa yamesajiliwa. Vilevile, vibali 9 vya ujenzi wa mabwawa ya topesumu vimetolewa ambapo bwawa moja (1) la topesumu limesajiliwa.

Udhibiti wa Uchimbaji wa Visima


Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kudhibiti uchimbaji na uendelezaji wa visima vya maji kwa kuratibu usajili wa kampuni za utafiti na uchimbaji wa visima pamoja na kutoa leseni na vibali vya uchimbaji ili kuhakikisha rasilimali ya maji chini ya ardhi inatumika kwa usahihi na sawia kulingana na uwepo wake na mahitaji. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya leseni 51 za makampuni ya uchimbaji visima, leseni 78 za wachimbaji na leseni 7 za utafiti wa maji chini ya ardhi zimetolewa na hivyo, kuwa na jumla ya leseni 100 za kampuni za uchimbaji leseni 117 za wachimbaji na leseni 22 za taasisi na makampuni ya utafiti wa maji chini ya ardhi. Aidha, jumla ya vibali 764 vya kuchimba visima vya maji katika maeneo mbalimbali vimetolewa na hivyo, kuwa na jumla ya vibali 6,836 vya kuchimba visima vilivyotolewa.

16​


Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Sekta zote zinazohusiana na maji inatekeleza Mpango wa Uhifadhi na Utunzaji wa Vidakio nchini wa mwaka

2021-2035. Kazi zinazotekelezwa zinahusisha kutambua, kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha vinakuwa endelevu. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya vyanzo vipya 314 vya maji juu ya ardhi vimetambuliwa na kati ya hivyo, vyanzo 37 vimewekewa mipaka. Kwa ujumla vyanzo vilivyotambuliwa vimefikia 3,296 na kati ya hivyo, vyanzo 327 vimewekewa mipaka na vyanzo 59 vimetangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa maeneo tengefu.

Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2024, kupitia kampeni ya upandaji wa miti rafiki wa maji katika vyanzo vya maji, miti 1,078,197 imepandwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na hivyo, jumla ya miti yote iliyopandwa kufikia 3,620,000. Kampeni hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia Azimio la pamoja kuhusu ushirikiano katika utunzaji wa rasilimali za maji unaohusisha Wizara zenye dhamana ya Maji, Mazingira, Kilimo, Nishati, Madini, Ardhi, TAMISEMI, Maliasili na Mifugo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, katika kuhakikisha jamii inashirikishwa kwenye usimamizi wa rasilimali za maji na kuongeza ufanisi wa usimamizi katika ngazi ya jamii, Wizara imeendelea kuunda na kuzijengea uwezo Jumuiya za Watumia Maji ambapo hadi mwezi Aprili 2024, Jumuiya saba (7) zimeundwa na hivyo kuwa na jumla ya Jumuiya za Watumia Maji 199. Pia, Wizara imeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji, madhara ya

17​


uharibifu wa vyanzo vya maji, na elimu ya Sheria na Kanuni mbalimbali za usimamizi wa rasilimali za maji.

Udhibiti wa Uchafuzi wa Vyanzo vya Maji


Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji, Wizara imeendelea kusimamia shughuli za utiririshaji wa majitaka kwenye mazingira. Hadi mwezi Aprili 2024, vibali 24 vya kutiririsha majitaka vimetolewa kwa kampuni na taasisi mbalimbali na hivyo, kuwa na jumla ya vibali vya kutiririsha majitaka vilivyotolewa kwenye mabonde yote kufikia 231.

Majukwaa ya Wadau wa Maji


Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika usimamizi wa rasilimali za maji kupitia Mipango Shirikishi ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji (Integrated Water Resources Management and Development Plan - IWRMDP). Lengo ni kuhakikisha uwepo wa matumizi bora na endelevu ya rasilimali za maji. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya majukwaa saba

(7)
ya wadau yamefanyika ambapo katika ngazi ya mabonde majukwaa sita (6) na ngazi ya Taifa jukwaa moja (1). Vilevile, vikao viwili (2) vya vikundi kazi vya Jukwaa la Taifa vimefanyika. Kufanyika kwa majukwaa hayo kumesaidia kuhamasisha wadau kuendelea kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji.









18​


Mfumo wa Kielekroniki wa Kusaidia Ufanyaji wa Maamuzi katika Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na maandalizi ya mfumo wa kielektroniki wa Kusaidia Ufanyaji wa Maamuzi katika Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji (Operational Decision Support System - ODSS). Mfumo huo unahusisha mifumo midogo ya utoaji taarifa za rasilimali za maji (Water Resources Management Information System), vibali vya matumizi ya maji (Water Use Permit Analysis Tool), utabiri wa mafuriko na tahadhari (Flood Forecasting and Early Warning System), utabiri wa misimu ya maji katika vyanzo vya maji (Seasonal and Flow Prediction Tools) na uendeshaji wa mabwawa ya maji (Dam Operational Support Tool). Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imekamilisha maandalizi ya mifumo midogo ya utabiri wa mafuriko na tahadhari, utabiri wa misimu ya maji katika vyanzo vya maji, uendeshaji wa mabwawa ya maji na mfumo wa utoaji taarifa kwa wadau. Aidha, mtaalam mshauri anaendelea na maandalizi ya mfumo wa vibali vya matumizi ya maji na uhakiki wa mfumo wa utabiri wa mafuriko.


Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Majishirikishi

Mheshimiwa Spika, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji katika vyanzo vya majishirikishi unalenga kulinda maslahi na kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya nchi wanachama. Tanzania ina vyanzo vya majishirikishi 14 ambavyo ni maziwa ya Victoria,

19​


Tanganyika, Nyasa, Natron, Chala na Jipe pamoja na Mito ya Kagera, Mara, Malagarasi, Momba, Mwiruzi, Umba, Ruvuma na Songwe. Ushirikiano na nchi wanachama unahusisha nchi za Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji na Zambia. Nchi nyingine tunazoshirikiana nazo ni Angola, Botswana, Eritrea, Ethiopia, Misri, Namibia, Sudan, Sudan Kusini na Zimbabwe. Ushirikiano huo hufanyika kupitia Mikataba na Hati za Makubaliano iliyoanzisha taasisi za kikanda na kimataifa ikiwemo Taasisi ya Mpito ya Bonde la Mto Nile, Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi na Kamisheni ya Bonde la Mto Ruvuma. Katika mwaka 2023/24, utekelezaji wa shughuli za usimamizi na ushirikiano wa rasilimali za majishirikishi ulifanyika kama ifuatavyo: -

Taasisi ya Mpito ya Bonde la Mto Nile


Mheshimiwa Spika, katika Bonde la Mto Nile utekelezaji wa mradi wa usimamizi wa maji chini ya ardhi katika mwambamaji (aquifer) wa Kagera kati ya Tanzania, Burundi, Rwanda na Uganda unaogharimu Dola za Marekani 5,329,452 kupitia ufadhili wa Mfuko wa Mazingira (Global Environmental Facility-GEF) unaendelea. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na maandalizi ya mtandao wa kufuatilia mwenendo wa maji chini ya ardhi kupitia mfumo wa Managed Aquifer Recharge; kujenga uwezo wa nchi wanachama katika usimamizi wa maji chini ya ardhi; na kuandaliwa kwa mpango kazi wa kusimamia

20​


na kuendeleza rasilimali za maji chini ya ardhi kitaifa na kikanda.

Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe

Mheshimiwa Spika, kupitia Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe, Tanzania na Malawi zinatekeleza Programu ya Maendeleo ya Bonde la Mto Songwe (Songwe River Basin Development Programme) inayolenga kutatua changamoto za mafuriko kwa kujenga mabwawa kwenye mto huo. Aidha, mabwawa hayo yatatumika kuzalisha umeme, kilimo cha umwagiliaji pamoja na matumizi mengine. Kwa sasa, hatua inayoendelea ni kutafuta fedha ambapo majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Afrika na makampuni ya wawekezaji yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuandaa mkataba wa kuuziana umeme (Power Purchase Agreement) kati ya Tanzania na Malawi. Vilevile, mradi wa hifadhi ya mazingira katika maeneo ya Ileje (Tanzania) na Chitipa (Malawi), na mradi wa kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika usimamizi wa maliasili (strenghthen transboundary corporation and integrated natural resources management) unaohusisha kutabiri mafuriko na kutoa taarifa za tahadhari unaendelea ambapo mtandao wa kufuatilia mwenendo wa maji na kufanya utabiri umejengwa.

Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria


Mheshimiwa Spika, kupitia Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika Jiji la Mwanza chini ya

21​


Programu ya Pamoja ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji ya Bonde la Ziwa Victoria. Hadi mwezi Aprili 2024, Serikali imekamilisha usanifu na kuanza taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi na upanuzi wa mtandao wa majitaka kwa awamu ya kwanza itakayogharimu Euro 5,300,000. Vilevile, jumla ya Euro 45,000,000 zimepatikana kutoka Serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kupanua mtandao wa majitaka pamoja na kujenga uwezo wa taasisi. Aidha, maadhimisho ya 12 ya Siku ya Bonde la Mto Mara yaliyofanyika tarehe 12-15 Septemba, 2023 Serengeti, Mkoani Mara yalihusisha Kongamano la Kisayansi kuhusu uhifadhi wa mazingira ya Bonde la Mto huo na upandaji wa miti rafiki wa maji 10,000 katika Bonde na Bwawa la Manchira.


Maandalizi ya Miradi ya Majishirikishi


Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali za majishirikishi na ushirikiano, Serikali inashirikiana na nchi wanachama kuandaa miradi mbalimbali ya usimamizi na ushirikiano wa majishirikishi. Hadi mwezi Aprili 2024, kupitia Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), Tanzania itanufaika na mradi wa uchimbaji visima vitatu (3) katika eneo la Nzuguni, Jijini Dodoma utakaogharimu Dola za Marekani 125,000.


Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imeandaa maandiko ya miradi ifuatayo: mradi wa kusimamia Bonde la Mto Ruvuma (Strengthening integrated transboundary source-to-sea management of the

Ruvuma River Basin and its coastal zones to ensure

22​


ecosystem health and livelihood security) utakaogharimu Dola za Marekani 7,763,000 kwa ufadhili wa Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Global Environmental Facility - GEF) utakaotekelezwa kwa kushirikiana na nchi za Msumbiji na Malawi pamoja na mashirika ya the International Union for Conservation of Nature (IUCN) na Global Water Partnership Southern Africa (GWPSA); mradi wa kusimamia maji chini ya ardhi katika mwambamaji wa Kilimanjaro (Unlocking the groundwater potential of the Kilimanjaro Water Tower) utakaogharimu Dola za Marekani 8,000,000.00 kwa ufadhili wa GEF utakaotekelezwa kwa kushirikiana na nchi ya Kenya pamoja na mashirika ya Food and Agricultural Organization (FAO) na UNESCO; na mradi wa usimamizi wa Bonde la Mto Zambezi (Strengthening Zambezi River Basin Management towards Climate Resilience and Ecosystem Health) utakaogharimu Dola za Marekani 10,566,750.00 kwa ufadhili wa GEF utakaotekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji


Mheshimiwa Spika, Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji kimeanzishwa kupitia Awamu ya Pili ya Mradi wa Kusaidia Sekta ya Maji unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Lengo la kituo hicho ni kuzijengea uwezo Taasisi zinazosimamia rasilimali za maji katika maeneo ya tafiti za kina na ugezi (callibration) wa vifaa vya kukusanyia takwimu za rasilimali za maji. Hadi mwezi Aprili 2024, Kituo kimewajengea uwezo Wataalam 102 wa Bodi za Maji za

Mabonde na Wizara katika matumizi ya model

23​


mbalimbali za kubaini na kutambua kiasi cha maji kilichopo katika maeneo yasiyo na mtandao wa kufuatilia mwenendo wa maji mitoni pamoja na kutumia Remote Sensing na GIS kutambua maeneo ambayo yanapatikana maji chini ya ardhi.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Kituo Mahiri kimeendelea kushirikiana na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), University College of London (UCL), Institute of Development Studies (IDS), University of Sussex (UOS), na Cardiff University kufanya utafiti wa kutambua njia mbadala za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa huduma za maji katika maeneo kame ya Mkoa wa Dodoma ikihusisha Wilaya za Chemba, Chamwino, Bahi na Kongwa. Mradi huo unafadhiliwa na Climate Adaptation and Resilience in Tropical Drylands (CLARITY) kwa gharama ya Shilingi 2,464,800,000.


3.2.1.2. Uendelezaji wa Rasilimali za Maji

Utafutaji wa Vyanzo vya Maji


Mheshimiwa Spika, uendelezaji wa rasilimali za maji unahusisha utafutaji na uendelezaji wa vyanzo vya maji chini na juu ya ardhi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kama vile mabwawa; na kufanya utafiti na uchimbaji wa visima virefu nchini. Kwa upande wa maji chini ya ardhi, Serikali imeendelea kufanya utafiti kwa lengo la kutatua changamoto ya maji kwenye maeneo yasiyo na vyanzo vya uhakika wa maji juu ya ardhi. Utafiti huo husaidia kubainisha maeneo na miamba yenye hifadhi ya maji

chini ya ardhi kwa ajili ya kuyaendeleza ambapo

24​


hadi sasa jumla ya maeneo 172 yanayodhaniwa kuwa na maji mengi chini ya ardhi yametambuliwa nchini kote. Kwa sasa kazi inayoendelea ni uchimbaji visima 112 vya uchunguzi kwenye mabonde ya Pangani, Wami Ruvu, Rufiji na Bonde la Kati. Hadi mwezi Aprili 2024, uchimbaji wa visima 17 umekamilika na utafiti unaendelea kwenye maeneo yaliyobaki.


Ujenzi na Ukarabati wa Mabwawa

Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Farkwa

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa bwawa la Farkwa kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa maji katika Jiji la Dodoma pamoja na Wilaya za Chemba, Chamwino na Bahi; kuzuia mafuriko; na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi. Hadi mwezi Aprili 2024, Wataalamu Washauri wamepatikana na wanaendelea na kazi ya mapitio ya usanifu wa bwawa. Aidha, Wizara imeunda timu ya wataalam wa usalama wa mabwawa watakaohakikisha masuala ya usalama wa bwawa katika ngazi zote za utekelezaji wa mradi. Vilevile, kazi ya uandaaji wa mpango wa kulinda na kutunza mazingira katika vyanzo vya maji vitakavyopeleka maji kwenye bwawa inaendelea. Ujenzi wa bwawa unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2024 baada ya kupatikana kwa mkandarasi.

Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na ujenzi wa bwawa la Kidunda unaogharimu Shilingi 329,466,814,886.00. Ujenzi wa bwawa hilo unalenga

25​


kuimarisha utiririshaji wa maji wa Mto Ruvu ili uwe na maji katika kipindi chote cha mwaka kwa ajili ya kulisha mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini; kuzuia mafuriko; kuzalisha umeme Megawati 20; kilimo cha umwagiliaji; na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi zinazotumia maji. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi eneo la mradi; ujenzi wa makazi ya wafanyakazi; kuimarisha kingo na tuta la muda la kukinga ujenzi wa power house na spill way; ujenzi wa barabara za ndani; na usanifu wa mkondo wa umeme kutoka Kidunda kwenda Chalinze Substation. Kazi zilizokamilika ni ujenzi wa makazi ya muda ya mkandarasi na ofisi; uchunguzi wa miamba na mtiririko wa maji eneo la ujenzi; ujenzi wa tuta la kukinga eneo la ujenzi wa mchepusho; na ujenzi wa nyumba ya kuzalisha umeme. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 17.9.

Ujenzi na Ukarabati wa Mabwawa ya Ukubwa wa Kati na Madogo

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na adha ya uhaba wa maji hususan kwenye maeneo kame, Wizara imeendelea na ujenzi wa mabwawa ya ukubwa wa kati na madogo katika maeneo mbalimbali nchini. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imekamilisha ujenzi na ukarabati wa mabwawa 14. Mabwawa yaliyokamilika ni Uhelera na Bahimakuru katika Wilaya ya Bahi;

Igumangobo na Ilambambasa (Maswa); Ng’walukwa (Shinyanga); Ngofila (Kishapu); Qang’dend (Karatu); na

Horohoro na Mbuta (Mkinga); Chole (Kisarawe); Kwamaizi (Handeni); Makame (Kiteto), Enguikumet II

26​


(Monduli) na bwawa la Mwadila Wilayani Maswa. Kati ya hayo, mabwawa mawili (2) ya Kwamaizi na Makame yamejengwa kwa kutumia seti mpya za ujenzi wa mabwawa zilizonunuliwa na Serikali.


Mheshimiwa Spika, aidha, ujenzi na ukarabati wa mabwawa 26 unaendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo kati ya hayo, mabwawa manne (4) yanajengwa kwa kutumia seti mpya za mitambo ya ujenzi wa mabwawa. Mabwawa hayo ni Kwenkambala katika Wilaya ya Handeni, Kizengi (Kaliua), Lepruko (Monduli) na Kwamjembe (Bagamoyo). Vilevile, seti za mitambo hiyo mipya zinatumika katika ujenzi wa mabwawa madogo nane (8) kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kupitia Programu ya Build Better Tommorow inayosimamiwa na Wizara ya Kilimo katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Uvunaji wa Maji ya Mvua

Mheshimiwa Spika, uvunaji wa maji ya mvua kupitia mapaa ya majengo ni muhimu, hususan katika kukabiliana na uhaba wa upatikanaji wa maji kwenye maeneo kame. Kutokana na umuhimu huo, Wizara imeandaa Mwongozo wa Uvunaji wa Maji ya Mvua wa Mwaka 2020 mahususi kwa ajili ya kusaidia jamii na taasisi mbalimbali katika kujenga miundombinu bora ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua kupitia mapaa ya nyumba. Hadi mwezi Aprili 2024, miundombinu ya kuvuna maji ya mvua imejengwa kwenye shule 760; hospitali, zahanati na vituo vya afya (701), ofisi za Serikali za vijiji, Halmashauri, masoko, mahakama na ofisi za CBWSOs (697) na Taasisi za dini (255). Aidha,

27​


Serikali imeendelea kuzihamasisha Taasisi za Kijamii, Asasi na Watu Binafsi kujenga miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua kwenye majengo yao.

3.2.2. Huduma za Ubora wa Maji

Mheshimiwa Spika
, ubora wa maji ni kigezo muhimu katika kutoa maamuzi ya matumizi ya maji kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchimi kwa lengo la kulinda afya ya jamii na mifumo ya ikolojia. Huduma za ubora wa maji hutolewa kupitia Maabara 17 za Ubora wa Maji zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Kigoma, Singida, Dodoma, Manyara, Arusha, Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza. Katika mwaka 2023/24, Wizara ilipanga kuendelea kutekeleza shughuli za usimamizi wa ubora wa maji kwa kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji kwenye vyanzo 2,091, skimu 4,600 za usambazaji maji vijijini na mijini na mifumo 150 ya uchakataji majitaka; kuhakiki ubora wa madawa ya kusafisha na kutibu maji kabla ya ununuzi na wakati wa matumizi; na kutoa elimu kuhusu viwango vya ubora wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara ilipanga kuwezesha uandaaji na utekelezaji wa mipango ya usalama wa maji inayohimili mabadiliko ya tabianchi kwa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira 34 na Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamiii 100; na kuendelea kuboresha utendaji kazi wa Maabara za Ubora wa Maji kwa kuzipatia vitendea kazi, pamoja na kuwezesha maabara saba (7) za ubora wa maji kudumisha hadhi ya ithibati.

28​

Ubora wa Maji katika Vyanzo

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinatumika pasipo kuathiri ikolojia, Wizara imeendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji katika vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya vyanzo vya maji 1,625 vilihakikiwa ubora wake ikiwemo visima (1,501), maziwa manne (4), mito (86), mabwawa manne (4) na chemchemi (30). Matokeo ya uhakiki na ufuatiliaji yanaonesha hali ya ubora wa maji katika vyanzo hivyo inaridhisha na inaendelea kulinda afya ya ikolojia licha ya kuwepo kwa changamoto za uchafuzi katika baadhi ya vyanzo vya maji juu ya ardhi na uwepo wa kiwango kikubwa cha madini ya chumvichumvi kwa vyanzo vya maji chini ya ardhi.


Ubora wa Maji kwa Matumizi ya Majumbani

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhakikisha jamii inapata maji safi na salama kwa kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji yanayosambazwa na Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs), Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira, Taasisi Binafsi pamoja na vyanzo vya maji vinavyomilikiwa na watu binafsi. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya skimu 763 za maji vijijini na skimu 185 za maji mijini zilifanyiwa uhakiki na ufuatiliaji ambapo jumla ya sampuli za maji 4,461 zilikusanywa na kuhakikiwa ubora wake. Matokeo ya uhakiki yameonesha kuwa sampuli 3,190 sawa na asilimia 71.5 zilikidhi viwango na sampuli 1,271 sawa na asilimia 28.5 hazikukidhi viwango vya kitaifa vya ubora wa maji ya kunywa.

29​


Changamoto kubwa katika skimu za usambazaji maji ni uwepo wa kiasi kikubwa cha madini ya Fluoride, Chumvi, Chuma na Manganese pamoja na Tope (turbidity) kwa baadhi ya skimu. Katika kukabiliana na changamoto hizo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madini hayo kwenye maji. Vilevile, Wizara imeendelea kuzijengea uwezo CBWSOs; Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira pamoja na taasisi na watu binafsi kuhusu namna bora ya kudhibiti na kuboresha ubora na usalama wa maji ili kulinda afya ya jamii ikiwa ni pamoja udhibiti wa magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu uwezeshaji wa uandaaji na utekelezaji wa Mipango ya Usalama wa Maji (Water Safety Plans) kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira na Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii ili kuhakikisha ubora wa maji unadhibitiwa kuanzia kwenye vyanzo hadi kwa watumiaji. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imewezesha kuandaliwa kwa mipango ya usalama wa maji kwa Mamlaka za maji na usafi wa mazingira za Dar es Salaam, Tabora, Dodoma, Musoma, Njombe, Mwanza na Bukoba. Aidha, Wizara imeendelea kusisitiza uzingatiaji wa miongozo na viwango mbalimbali vya usimamizi wa ubora wa maji ya kunywa ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji wa Maji ya Kunywa na Uandaaji wa Taarifa wa Mwaka 2018; Mwongozo wa Kitaifa wa Kusafisha na Kutibu Maji wa Mwaka 2020; na Viwango vya Ubora wa Maji ya Kunywa vya Kitaifa (TZS 789:2018).




30​

Ubora wa Maji kwa Matumizi Mengineyo

Mheshimiwa Spika, ubora wa maji ni kigezo muhimu katika matumizi ya maji kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi. Uhakiki na ufuatiliaji wa ubora wa maji kwa matumizi ya kiuchumi husaidia kutumika kwa maji yenye ubora stahiki na kuwezesha kupatikana kwa matokeo bora kwa kazi iliyotarajiwa hali inayochochea ukuaji wa biashara na uchumi wa nchi kwa ujumla. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imehakiki na kufuatilia ubora wa maji kwa kukusanya jumla ya sampuli 288 za maji ambapo sampuli 62 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani, ujenzi (100), umwagiliaji (59) na sampuli 58 kwa ajili ya shughuli za utafiti. Matokeo yalionesha asilimia 99 ya sampuli zilikidhi viwango kwa matumizi yaliyokusudiwa na asilimia 1 ya sampuli hazikukidhi viwango kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha chumvi katika maji.

Uhakiki wa Madawa ya Kusafisha na Kutibu Maji

Mheshimiwa Spika, katika kuongeza ufanisi wa madawa ya kutibu na kusafisha maji, Serikali imeendelea kuhakiki ubora wa madawa yanayotumika kutibu na kusafisha maji wakati wa ununuzi na kipindi cha matumizi. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya sampuli

za madawa ya kusafisha na kutibu maji

yanayotumika kwenye Taasisi mbalimbali yalichunguzwa ubora wake ambapo sampuli saba (7) zilikuwa za madawa ya kusafisha maji aina ya Aluminium Sulphate (Shabu) na sampuli 12 za madawa ya kutibu maji aina ya Calcium Hypochlorite. Matokeo yamebaini kuwa sampuli zote za madawa hayo zilikidhi

31​

viwango vinavyokubalika.


Ubora wa Majitaka Yanayorudishwa Kwenye Mazingira

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa majitaka katika mifumo ya majitaka ili kuhakikisha majitaka yanayorudishwa kwenye mazingira yanakidhi viwango vya ubora unaokubalika. Hadi mwezi Aprili 2024, majitaka kutoka mifumo 10 ya kusafisha majitaka ya mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira na mifumo 54 ya kusafisha majitaka ya viwanda na taasisi nyingine yalihakikiwa ubora wake. Matokeo yalionesha majitaka kukidhi viwango vya ubora wa kurudishwa kwenye mazingira kwa asilimia 42. Majitaka ambayo hayakukidhi viwango yalitokana na kutokuwepo kwa kiasi cha kutosha cha hewa ya oxygen. Mamlaka za maji na viwanda ambavyo majitaka hayakukidhi viwango vya ubora, ushauri wa kitaalam ulitolewa ili kuongeza ufanisi wa mifumo ya kusafisha na kutibu majitaka.

Uimarishaji wa Maabara za Maji

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuziimarisha maabara za ubora wa maji ili ziweze kutoa huduma bora za ubora wa maji nchini. Hadi mwezi Aprili 2024, Wizara imeziwezesha maabara za ubora wa maji za Dar es Salaam na Mwanza kununua vifaa vya upimaji wa madini tembo pamoja na kufanya matengenezo ya mashine za Inductive Couple Plasma(ICP) na Atomic Absorption Spectroscopy (AAS) ambazo zina uwezo wa kupima kwa pamoja na kwa

32​

ufanisi viashiria vingi zaidi vya ubora wa maji.


Mheshimiwa Spika, aidha, ili kuongeza ufanisi katika uchunguzi, Wizara imeziwezesha maabara za ubora wa maji kushiriki mazoezi ya kujipima uwezo yanayoratibiwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo SADCMET na BIPEA. Matokeo yameonesha maabara za ubora wa maji kuwa na uwezo wa kupima viashiria mbalimbali vya ubora wa maji kwa usahihi hivyo, majibu kutoka katika maabara hizo kukubalika Kimataifa. Vilevile, Wizara imeziwezesha maabara saba

(7)
za ubora wa maji zenye hadhi ya ithibati ambazo ni Dar es Salaam, Singida, Shinyanga, Mwanza, Musoma, Kigoma na Bukoba kuendelea kudumisha hadhi hiyo.

3.2.3. Huduma za Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeendelea kujenga, kukarabati, kupanua mitandao ya kusambaza maji pamoja na kuimarisha usimamizi wa huduma ya maji katika maeneo ya vijijini. Lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya majisafi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025. Kutokana na kukamilika kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 77 mwezi Desemba, 2022 hadi kufikia wastani wa asilimia 79.6 mwezi Desemba, 2023. Aidha, kwa upande wa usafi wa mazingira, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, imeendelea kubainisha maeneo ya kujenga miundombinu ya kutibu na kusafisha majitaka ambapo hadi sasa Halmashauri za Wilaya za Ludewa, Njombe

33​


na Nkasi zimekamilisha Mpango Kabambe wa Maji na Usafi wa Mazingira. Ukamilishaji wa Mpango huo unaendelea katika Wilaya zilizobaki za Mikoa ya Rukwa na Njombe. Maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa shughuli zinahusu huduma ya majisafi na usafi wa mazingira vijijini ni kama ifuatavyo:-

3.2.3.1. Utekelezaji wa Baadhi ya Miradi ya Maji Vijijini

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2023/24, Wizara ilipanga kutekeleza jumla ya miradi 1,546 katika maeneo ya vijijini. Hadi mwezi Aprili, 2024, miradi 632 yenye jumla ya vituo 7,956 imetekelezwa na inatoa huduma kwa wananchi 4,740,959 (Kiambatisho Na. 2). Aidha, utekelezaji wa miradi 872 unaendelea na ipo kwenye hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabwawa 18 ya kuvuna maji ya mvua. Maelezo kuhusu utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maji vijijini ni kama ifuatavyo:-

Mradi wa Maji Ruangwa, Lindi na Nachingwea


Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa kutoa maji Mto Nyangao uliopo Wilaya ya Lindi kwenda Wilaya tatu (3) za Lindi, Ruangwa na

Nachingwea kwa gharama ya Shilingi 119,555,923,438.00. Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha kupeleka maji kwenye vijiji 29 ambapo katika Wilaya ya Ruangwa, vijiji 25; Nachingwea vijiji vitatu (3); na Lindi kijiji kimoja (1).



34​


Mheshimiwa Spika, kazi zinazotekelezwa katika awamu ya kwanza ya mradi ni ujenzi wa chanzo cha maji, ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji ya umbali wa kilomita 211, ujenzi wa mfumo wa kutibu maji, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji, ujenzi wa matanki sita (6) ya kuhifadhi maji yenye jumla ya lita 4,750,000, ujenzi wa nyumba tatu (3) za watumishi na Ofisi ya CBWSO. Hadi mwezi Aprili, 2024 utekelezaji umefikia asilimia 18 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2024. Awamu ya pili ya mradi inahusisha ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lenye ujazo wa lita 50,000, ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 100,000, ujenzi wa vituo 30 vya kuchotea maji na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilomita 105. Utekelezaji wa awamu hiyo utaanza baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza. Mradi utakapokamilika utawanufaisha wananchi wapatao 130,000 wa vijiji 56 ambapo katika Wilaya ya Ruangwa vijiji 34; Wilaya ya Nachingwea vijiji 21 na Wilaya ya Lindi kijiji kimoja (1).

Mradi wa Maji Mkinga – Horohoro

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza mradi wa maji Mkinga – Horohoro kwa gharama ya Shilingi 35,899,392,562.00. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa matanki nane (8) yenye ujazo wa lita milioni 1.29; ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 196; ujenzi wa vituo 60 vya kuchotea maji na ofisi ya CBWSO. Hadi mwezi Aprili, 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 36 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024. Kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi 74,795 wa Mji wa Horohoro

35​

na vijiji 37 vya Wilaya ya Mkinga.


Mradi wa Maji Diburuma - Songe

Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa maji Diburuma - Songe uliopo Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga kwa kutumia chanzo cha maji cha Mto Diburuma kwa gharama ya Shilingi 22,956,445,680.00. Mradi huo unahusisha ujenzi wa matanki 11 yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 2.2; ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 155.7; ujenzi wa mtambo wa kutibu maji; ununuzi na ufungaji wa pampu mbili zenye uwezo wa kuzalisha maji lita 48,000 kwa saa; ujenzi wa vituo 60 vya kuchotea maji na ofisi ya CBWSO. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2025 na kuwanufaisha wananchi 75,224 waishio kwenye Vijiji 24 vya Kikunde, Mafulila, Tunguli, Msamvu, Mtoro, Lusane, Kitingi, Mapanga, Ngeze, Kwekivu, Lusimbi, Mheza, Misheni, Sambu, Kigunga, Kwamba, Mvungwe, Vilindwa, Songe, Bokwa, Nkama, Kwastemba, Kwamwande na Masigalu katika Wilaya ya Kilindi.

Mradi wa Maji Morong’anya - Morogoro Vijijini

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa maji Morong’anya wilayani Morogoro kwa gharama ya Shilingi 23,186,021,991.00. Mradi utahudumia vijiji 19 vya Kalundwa, Kibwaya, Tandai, Mkuyuni, Madamu, Luholela, Mwarazi, Kivuma, Kungwe, Kikundi, Lukonde, Vuleni, Lubungo, Muhunga - Mkola, Newland, Kibuko, Maseyu, Kinonko na Gwata. Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa banio la

maji, mtambo wa kusafisha na kutibu maji, matanki 12

36​


yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 1.84, vituo 100 vya kuchotea maji na Ofisi ya CBWSO; na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 117. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 80 na umeanza kutoa huduma kwenye vijiji 10. Mradi unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni, 2024 na kunufaisha wananchi wapatao 52,000.

Mradi wa Maji Ukiliguru, Sumve hadi Koromije

Mheshimiwa spika, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Miji ya Usagara, Ukiliguru, Sumve hadi Koromije na vijiji 24 vya Wilaya za Misungwi na Kwimba kwa gharama ya Shilingi 32,756,175,561.00. Mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji, matanki sita (6) yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 5.63, mtambo wa kusafisha na kutibu maji, vituo 80 vya kuchotea maji, jengo la pampu, nyumba moja (1) ya watumishi na ofisi mbili (2) za CBWSO; ununuzi na ufungaji wa pampu; na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 261.1. Hadi mwezi Aprili, 2024 utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwezi machi, 2025 na kuwanufaisha wananchi 162,377.

Mradi wa Maji Ilujamate - Buhingo

Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kutekeleza mradi wa maji Ilujamate - Buhingo unaotoa maji Ziwa Victoria kwenda vijiji 16 vya Gukwa, Mbalama, Buhunda, Mwagimagi, Kifune, Gulumungu, Lukanga, Nyambiti, Busongo, Ng'hamve, Nyamayinza, Songiwe, Seeke, Buhingo, Kabale na Mwasagela kwa gharama ya

Shilingi 2,469,397,202.00. Mradi huo unahusisha

37​


ujenzi wa matanki matatu (3) yenye jumla ya ujazo wa lita 800,000, vituo 50 vya kuchotea maji na ofisi moja

ya CBWSO; ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 97.43. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024 na kuwanufaisha wananchi wapatao 61,088.

Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Kahama kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha maandalizi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji Ushetu kwa gharama ya Shilingi 44,271,886,678.17. Mradi huo utachukua maji kutoka bomba kuu la Kahama - Shinyanga na kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 164.6; ujenzi wa matanki matatu (3) yenye jumla ya ujazo wa lita 900,000, vituo 35 vya kuchotea maji na ofisi ya CWBSO; na kuunganisha wateja wa majumbani wapatao 1,000. Kwa sasa mradi upo kwenye hatua za kumuajiri mkandarasi na utekelezaji unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Mei, 2024 na kukamilika ndani ya Miezi 24. Kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha wananchi 234,455 waishio kwenye Vijiji 54 vya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.


Mradi wa Matumizi ya Dira za Maji za Malipo ya Kabla

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia RUWASA kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), na Dar

38​


Teknohama Business Incubator - (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) inatekeleza mradi wa kubuni, kuunda na kufunga dira za maji za malipo kabla ya matumizi katika skimu za maji vijijini ili kudhibiti upotevu wa maji pamoja na mapato ya mauzo ya maji. Kupitia mradi huo, jumla ya dira 300 zinazoendana na mazingira ya vijijini zitabuniwa na kuundwa. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya dira 150 zimeundwa na kufungwa kwa majaribio kwenye skimu mbalimbali za maji na kuonesha ufanisi katika ufanyaji kazi.

3.2.3.2. Programu ya Uendelevu wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inatekeleza Programu ya Uendelevu wa Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini. Awali, Programu hiyo ililenga kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwenye Halmashauri za Wilaya 86 katika mikoa 17 na kujenga uwezo kwa taasisi zinazosimamia huduma ya maji vijijini. Programu ilipangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2019/20 - 2024/25 na ilipangwa kunufaisha wananchi milioni 3. Gharama za utekelezaji wa programu hiyo zilikuwa ni Dola za Marekani milioni 350 na utekelezaji unafanyika kwa utaratibu wa Malipo kwa Matokeo, yaani Program for Results almaarufu PforR.

Mheshimiwa Spika
, kupitia programu hiyo, jumla ya miradi 540 imetekelezwa hadi sasa yenye vituo vya kuchotea maji 4,569 na kunufaisha wananchi wapatao

39​


milioni 4.1 katika vijiji 1,118. Matokeo hayo, yamevuka lengo la awali la kuhudumia wananchi milioni 3 na hivyo, katika Mkutano wa Mawaziri wa Maji na Fedha wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia mwezi Novemba 2023, Benki ya Dunia iliitambua Tanzania kuwa kinara katika utekelezaji wa Programu hiyo. Kutokana na mafanikio hayo, Tanzania imeongezewa fedha za Programu kutoka Dola za Marekani milioni 350 hadi Dola za Marekani milioni 654 na kuongeza mikoa inayonufaika kutoka 17 hadi 25 na kutoka Halmashauri 86 hadi 137.

3.2.3.3. Matumizi ya Teknolojia ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy)

Mheshimiwa Spika
, katika kupunguza gharama za uendeshaji ili kufikia lengo la kuwa na huduma endelevu ya maji vijijini, Wizara kupitia RUWASA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, REA pamoja Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) inatekeleza mradi wa kupunguza au kuondoa matumizi ya nishati ya dizeli (“Accellerating Solar Water Pumping Via Innovative Financing - ASWPIF). Mradi huo utatekelezwa kwenye skimu 332 za maji vijijini. Jumla ya skimu 100 zimepangwa kubadilishwa kutoka kutumia nishati ya dizeli na kufungiwa mifumo ya umeme jua katika Mikoa ya Dodoma (47), Singida (25), Shinyanga (12) na Mtwara (16). Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya skimu 65 zimebadilishiwa mifumo ya dizeli na kuwekewa mifumo inayowezesha matumizi ya umeme wa gridi pamoja na umeme jua katika mikoa ya Dodoma (25), Singida (17), Shinyanga (11) na Mtwara (12).


40​


3.2.3.4. Uimarishaji wa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii

Mheshimiwa Spika
, Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (Community Based Water Supply Organizations - CBWSOs) vina jukumu la kuhakikisha uendelevu wa miradi ya maji vijijini kwa kuendesha na kufanya matengenezo madogo ya skimu za maji. Kwa kutambua umuhimu wa vyombo hivyo, pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa skimu, Serikali imeendelea kuunda, kusajili, kuunganisha na kuzijengea uwezo CBWSOs zilizopo. Hadi mwezi Aprili, 2024, Wizara kupitia RUWASA imeunda na kusajili CBWSOs

na kuunganisha CBWSOs 517 hivyo, kufanya jumla ya idadi ya CBWSO zilizosajiliwa kuwa 1,382. Katika kuimarisha utendaji kwenye vyombo hivyo, CBWSOs zimeajiri wataalam 5,342 katika kada za ufundi, uhasibu pamoja na kada saidizi. Uwepo wa wataalam hao umeboresha hali ya uendeshaji na utoaji wa huduma ya maji vijijini.

Mheshimiwa Spika
, RUWASA iliwezesha CBWSOs 136 kuandaa Vitabu vya Hesabu (Financial Statements) za mwaka 2022/2023 na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Ripoti ya CAG imeonesha kati ya CBWSOs zilizokaguliwa, 133 sawa na asilimia 98 zimepata hati safi. Vilevile, katika kuimarisha udhibiti wa mapato ya fedha za umma, RUWASA imeziwezesha CBWSOs 661 katika mikoa 16 kujiunga katika Mfumo wa GePG na kuanza kukusanya mapato ya mauzo ya maji kupitia mfumo huo.


41​


3.2.3.5. Mitambo ya Uchimbaji wa Visima na Mabwawa

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeandaa Mwongozo wa Matumizi ya Mitambo 25 ya Uchimbaji Visima na Seti

za Mitambo ya Ujenzi wa Mbawawa ili mitambo hiyo itumike ipasavyo na kuleta tija iliyokusudiwa. Mwongozo huo unaainisha namna bora ya matumizi ya mitambo ikiwemo utaratibu wa muda wa ufanyaji kazi, muda wa matengenezo kinga na matengenezo makubwa ya mitambo.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Wizara imekamilisha uchimbaji wa visima 289 kwenye maeneo mbalimbali ya vijijini. Kati ya hivyo, visima 283 vimechimbwa kwa kutumia seti za mitambo mipya na visima sita (6) vimechimbwa na mitambo mingine ikiwemo kampuni binafsi.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara imefanya tathimini na kuandaa mpango wa kufikisha huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana huduma hiyo. Kupitia mpango huo, Serikali imepanga kuchimba visima vitano (5) katika kila jimbo la uchaguzi kwenye maeneo ya vijijini katika mikoa yote 25 ya Tanzania Bara ambapo jumla ya visima 900 vyenye gharama ya Shilingi 58,800,000,000 vinatarajiwa kuchimbwa. Hadi sasa kazi ya uchimbaji visima imeanza katika mikoa ya Kigoma na Songwe na utafiti unaendelea kwenye mikoa mingine. Aidha, kipaumbele cha mpango huo kitatolewa kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma na hakuna mradi wowote unaondelea.


42​


3.2.4. Huduma za Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imeendelea kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka katika maeneo ya mijini kwa lengo la kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wakazi wote waishio mijini. Katika mwaka 2023/24, jumla ya miradi 244 ilipangwa kutekelezwa ambapo hadi mwezi Aprili 2024, miradi 85 imekamilika (Kiambatisho Na. 3) na miradi 159 inaendelea na ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Utekelezaji wa baadhi ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa, Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo, na Miradi ya Kitaifa ni kama ifuatavyo:-

3.2.4.1. Miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Jiji la Mbeya


Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa majisafi katika Jiji la Mbeya kwa kutumia chanzo cha Mto Kiwira kwa gharama ya Shilingi 99,659,532,284.92. Mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 66.5 kwa siku hadi lita milioni 184 kwa siku pamoja na kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Mbeya. Hadi mwezi Aprili 2024, ujenzi wa banio na tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 5 unaendelea na utekelezaji umefikia asilimia 11. Mradi unatarajiwa

43​


kukamilika mwezi Machi, 2025 na kuwanufanisha wakazi wapatao 1,452,751.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inatekeleza kipande cha kwanza na cha pili cha mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Kata za Mwansekwa na Iganzo kwa gharama ya Shilingi 5,200,000,000. Utekelezaji wa kipande cha kwanza umefikia asilimia

na kazi zinazotekelezwa zinahusisha ujenzi wa chujio la maji na ujenzi wa tanki la lita milioni 2. Utekelezaji wa kipande cha pili umefikia asilimia 76 na kazi zinazotekelezwa ni ujenzi wa banio katika vyanzo vya Hanzya na Hasara pamoja na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 15.8 ambapo kilomita 7.8 zimelazwa. Mradi umeanza kuzalisha maji lita milioni 2 kwa siku na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 42,000 wa kata za Mwansekwa na Iganzo.

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Mji wa Geita na Maeneo ya Pembezoni


Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji Katoro - Buseresere

uliogharimu Shilingi 1,300,315,203. Kazi zilizotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba katika njia kuu ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 5, ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 35 na uunganishaji wa wateja wapya 850. Mradi huo unahudumia wakazi wapatao 1,200 wa maeneo ya Katoro na Buseresere.





44​


Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji Nyankanga kwa gharama ya Shilingi 1,100,000,000. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki la maji la lita 100,000; ujenzi wa nyumba ya pampu; ujenzi wa miundombinu ya kutibu maji; na ununuzi na ufungaji wa pampu mbili (2) zenye uwezo wa kuzalisha maji lita 150,000 kwa saa. Kazi iliyobaki ni ununuzi na ufungaji wa pampu yenye uwezo wa kuzalisha maji lita 300,000 kwa saa. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Mradi utakapokamilika utawanufaisha wakazi wapatao 3,000 wa Nyankanga.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imekamilisha mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji katika Mji wa Geita kwa gharama ya Shilingi 613,822,621.50. Mradi unatoa huduma ya maji kwa wakazi wapato 3,000 wa Mji wa Geita. Kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji yenye umbali wa kilomita 45; ununuzi wa pikipiki 15; ununuzi wa mabomba yenye jumla ya urefu wa kilomita 10 kwa ajili ya maunganisho ya wateja; na ufungaji wa jenereta la ofisi.

Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha

Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa majisafi na usafi wa Mazingira katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Dola za Marekani 233,915,581. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na uchimbaji wa visima 56; ujenzi wa mabwawa mapya 18

45​


ya kutibu majitaka; upanuzi na ukarabati wa miundombinu na mifumo ya majisafi na majitaka maeneo ya katikati ya Jiji; ujenzi wa vyoo 42 vya mfano vyenye jumla ya matundu 184; ujenzi wa mtandao mpya wa majitaka umbali wa kilomita 180.503; ujenzi wa mitambo ya kusafisha maji; ujenzi wa ofisi tatu (3) za kanda, Karakana na Bohari katika eneo la Safari City; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; ujenzi wa ofisi kuu; na upanuzi wa mtandao wa majitaka nje ya maeneo ya katikati ya Jiji; ufungaji wa mfumo wa mawasiliano; ujenzi wa matanki; na ujenzi wa mfumo wa kuchanganya maji (blending). Kwa sasa mradi upo katika muda wa matazamio. Kukamilika kwa mradi kumeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 kwa siku hadi lita milioni 200 kwa siku; muda wa upatikanaji wa huduma ya majisafi kutoka saa 12 za sasa hadi saa 24 kwa siku; huduma ya uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 7.6 za sasa hadi asilimia 30; kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 48 hadi asilimia 39; na kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.


Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara inaendelea na ujenzi wa mradi wa majisafi Oldonyosambu kwa gharama ya Shilingi 6,382,532,295.20. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 21.6 kati ya kilomita 37.34 zilizopangwa; ujenzi wa vituo viwili (2) vya kusukuma maji; ujenzi wa tanki la lita 350,000 kati ya matanki matatu (3) yenye lita 575,000; na ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 47 na unatarajiwa kukamilika mwezi

Juni, 2025. Mradi utakapokamilika

46​


utawanufaisha wakazi wapato 29,449 wa Oldonyosambu.

92. Mheshimiwa Spika, pia, Wizara inatekeleza ujenzi wa mradi wa majisafi Mageri - Ngorongoro kwa gharama ya Shilingi 6,105,995,066.21. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa chanzo, ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 6 kati ya kilomita 28 zilizopangwa, ujenzi wa matanki 17 ya kupunguza msukumo wa maji, ujenzi wa matanki sita (6) yenye jumla ya lita 975,000 na ujenzi wa vituo 64 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 52 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025. Mradi utakapokamilika utawanufaisha wakazi wapatao 33,969 wa Mageri - Ngorongoro.

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Jiji la Tanga na Maeneo ya Pembezoni


Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na awamu ya pili ya ujenzi pamoja na uboreshaji wa mradi wa maji katika maeneo ya Mabokweni - Kibafuta, Chongoleani na Mleni unaogharimu Shilingi 516,551,200. Mradi huo unahusisha ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 11.7, ununuzi na ufungaji wa pampu, ujenzi wa chemba 33, ujenzi wa nguzo za alama 147 na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 9.2; ununuzi wa pampu; na ujenzi wa chemba tatu (3). Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia

na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo, kutawanufaisha wakazi wapatao 15,000 wa maeneo ya Mabokweni, Kibafuta,

47​

Chongoleani na Mleni.


Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na uboreshaji wa mfumo wa maji katika Mji wa Pangani kwa gharama ya Shilingi 1,000,000,000. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni uchimbaji wa kisima kirefu; ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 15; ununuzi na ufungaji wa pampu; ujenzi wa chemba; na ujenzi wa nguzo za alama. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 10.5; na uchimbaji wa kisima kirefu. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo, kutawanufaisha wakazi wapatao 16,000 wa Mji wa Pangani.

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa mfumo wa maji katika Mji wa Muheza kwa gharama ya Shilingi 700,000,000. Mradi huo unahusisha ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 7.5; ujenzi wa chemba 32; ujenzi wa anchor block 20; na ujenzi wa nguzo za alama 182. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 7.47; na ujenzi wa nguzo za alama 182. utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wakazi wapatao 14,160 wa Mji wa Muheza.








48​


Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Miji ya Kibaha, Kisarawe, Mkuranga, Chalinze na Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani


Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha kipande cha kwanza na cha pili cha mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kutoka katika visima virefu vya Kimbiji kwa gharama ya Shilingi 21,278,706,991. Kukamilika kwa mradi kumeimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wakazi wapatao 250,000 wa Chanika, Luzando, Mpera, Chamazi, Kitunda, Kinyerezi, Temeke, Kisarawe, Kibada, Kimbiji, Kigamboni, Tuangoma, Mkuranga, Kongowe, Mbagala, Kurasini, Mtoni, Keko na Chang’ombe. Kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki la lita milioni 15 katika eneo la Kisarawe II; ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika eneo la Kimbiji; ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 6.9 kutoka Kibada hadi Maweni kwa Mwingira; ulazaji wa bomba la kusafirisha maji umbali wa kilomita 8 kutoka Kibada kupitia Daraja la Nyerere hadi bomba la kusambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam; ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 6.3 kutoka kwenye visima kupeleka maji kwenye tanki; ufungaji wa pampu 10; na ulazaji wa bomba la kusafirisha maji umbali wa kilomita 15.8 kutoka kwenye visima hadi kwenye kituo cha kusukuma maji.




Mheshimiwa Spika, pia, Wizara inaendelea kutekeleza kipande cha tatu cha mradi kinachohusu ujenzi wa mfumo wa mabomba ya maji Kimbiji –

Kigamboni kutoka kwenye tanki la Kimbiji kwa
49​


gharama ya Shilingi 8,000,000,000. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 44 kati ya kilomita 65 zilizopangwa. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2024.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji na matanki ya kuhifadhi maji Kusini mwa Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi 35,149,404,125. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa kituo cha kusukuma maji; ujenzi wa tanki la kukusanyia maji la lita 500,000; ulazaji wa bomba kuu la chuma umbali wa kilomita 10.8; ulazaji wa bomba za kusambaza maji umbali wa kilomita 108.15; na ujezi wa tanki la lita milioni 9. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 1.164 na ujenzi wa tanki la lita milioni 9. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 19 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2024. Mradi unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 450,000 wa maeneo ya Bangulo, Mwanagati, Kitunda, Kipunguni, Majohe, Kivule, Magole, Msongola, Chanika na Chalambe.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inatekeleza kipande cha kwanza na cha pili cha mradi wa usambazaji maji katika maeneo yaliyo nje ya mtandao kwa gharama ya Shilingi 22,079,079,033 na unatarajiwa kuwanufaisha wakazi wapatao 215,380. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji umbali wa kilomita

414 kati ya kilomita 138.446 zilizopangwa na utahudumia vitongoji 13 vya Kisewe, Magengeni, Dovya,

50​


Mwembebamia, Mianzini, Mwanamtoti, Butiama, Mgeule, Mgeule Juu, Upendo, Tungi, Magogoni na Ferry vilivyopo Kigamboni na Temeke; ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji umbali wa kilomita 69.278 ambao utahudumia vitongoji sita (6) vya Nzasa A, Somelo, Kifurukwe, Kichangani, Yangeyange na Vumba vilivyopo Kigamboni na Ilala; na ujenzi wa tanki la lita milioni 2 katika eneo la Somelo. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 96 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2024.

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Jiji la Mwanza na Maeneo ya Pembezoni

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank-EIB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (French Development Agency-AFD) imekamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chujio la Butimba kwa gharama ya Euro 31,172,568.93. Kukamilika kwa mradi huo kumeboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wapatao 450,000 katika Jiji la Mwanza.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inatekeleza mradi wa kuongeza mfumo wa usambazaji wa maji katika miji ya Magu na Misungwi kwa gharama ya Shilingi 1,939,814,086.65. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zinazoendelea kutekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 85.94 ambapo kilomita 40.24 zimelazwa; ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji; ujenzi wa kituo cha kusukuma maji; ujenzi wa tanki la kukusanyia maji la lita 50,000; ujenzi wa matanki mawili (2) yenye uwezo wa lita 240,000; na ujenzi wa njia ya mfumo wa umeme. Utekelezaji wa

51​


mradi umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kunufaisha wakazi wapatao 33,000 wa miji ya Magu na Misungwi.

Mheshimiwa Spika, pia, Wizara inatekeleza mradi wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Mwanza kwa gharama ya Shilingi 4,624,246,101.32. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 54.5 kati ya kilomita 71.3 zilizopangwa; na ujenzi wa chemba za valvu 40. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 33,000. Vilevile, Wizara inatekeleza mradi wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji kwa gharama ya Shilingi 405,640,707.20. Kazi zinazoendelea kutekelezwa ni ulazaji wa bomba za kusambaza maji umbali wa kilomita 10.85 kati ya kilomita 18.263 zilizopangwa; ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji; ujenzi wa chemba za valvu 9; na ujenzi wa ofisi ya mlinzi. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuwanufaisha wakazi wapatao 12,000 wa Mwanza.

Upanuzi wa Huduma ya Maji kupitia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Lindi

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji kutoka Lindi

Mjini hadi Mchinga unaogharimu Shilingi 12,419,342,808.31. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni uchimbaji wa visima vitatu (3); ujenzi

52​


wa vioski 20; ulazaji wa mabomba katika njia kuu umbali wa kilomita 30 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 80. Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa tanki la lita 680,000; ujenzi wa uzio kuzunguka tanki; na ujenzi wa nyumba ya mlinzi. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuwanufaisha wakazi wapatao 40,000 wa maeneo ya Mchinga.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji katika eneo la Angaza kwa gharama ya Shilingi 1,138,328,705.12. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ufungaji wa pampu; ujenzi wa tanki la lita 200,000; ulazaji wa mabomba katika njia kuu umbali wa kilomita 1.6; na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 16.4. Hadi mwezi Aprili 2024, ujenzi wa tanki, ulazaji wa mabomba katika njia kuu na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umekamilika; na kazi iliyobaki ni ufungaji wa pampu. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 5,600 wa eneo la Angaza.

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Manispaa ya Musoma na Maeneo ya Pembezoni


Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi katika Mji wa Musoma kwa gharama ya Shilingi 400,000,000. Mradi huo unahusisha ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji yenye jumla ya urefu wa kilomita 36.768. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi

53​


zilizotekelezwa ni ununuzi wa mabomba yenye urefu wa kilomita 29.759 na ulazaji wa mabomba kwenye mtandao wa maji umbali wa kilomita 11.9. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. kukamilika kwa mradi kutawanufaisha wakazi wapatao 40,000.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa maji Rorya – Tarime kwa gharama ya Shilingi 134,398,706,754.46. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 29; ujenzi wa chujio lenye uwezo wa kusafisha na kutibu maji lita milioni 28; ujenzi wa matanki matatu (3) yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10; ujenzi wa kituo cha kusukuma maji eneo la Gamasara - Tarime; ununuzi na ulazaji wa mabomba katika mtandao wa kusambaza maji umbali wa kilomita 20; na ununuzi na ulazaji wa mabomba katika njia kuu ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 90. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizoanza kutekelezwa ni ujenzi wa matanki mawili (2) yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 4 na ujenzi wa kituo cha kusukuma maji eneo la Gamasara. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 11 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2025. Kukamilika kwa mradi kutawanufaisha wakati wapatao 487,533 wa miji ya Rorya na Tarime.


Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kutekeleza Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Mugumu kwa gharama ya Shilingi 22,369,967,795. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 15; ujenzi wa chujio lenye uwezo wa kusafisha na kutibu maji lita milioni

54​


14.5; ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2; ununuzi na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 31; na ununuzi na ulazaji wa mabomba katika njia kuu ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 6.6. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizoanza kutekelezwa ni ujenzi wa tanki na ujenzi wa chujio. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 6 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2025. Kukamilika kwa mradi kutawanufaisha wakazi wapatao 166,960 wa Mji wa Mugumu.

(i) Kuboresha Huduma ya Maji katika Mji wa Babati


Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Dareda – Singu – Sigino - Bagara unaogharimu Shilingi 12,724,407,807.85. Mradi huo unahusisha ujenzi wa matanki matano (5) ya kuhifadhi maji yenye jumla ya lita milioni 4.1; ulazaji wa mabomba usambazaji maji umbali wa kilomita 63.31; ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 26.83; ujenzi wa vituo viwili (2) vya kusukuma maji; ununuzi na ufungaji wa pampu mbili (2) za kusukuma maji; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; na ujenzi wa chanzo. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa matanki matatu (3) ya kuhifadhi maji yenye ujazo wa lita milioni 2.45; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; ulazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 20; na ujenzi wa chanzo. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 90. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 60,000.


55​


Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Jiji la Dodoma

Mheshimiwa Spika
, mahitaji ya maji kwa Jiji la Dodoma ni lita milioni 149.5 ikilinganishwa na uzalishaji wa lita milioni 79.1 kwa siku hivyo, kuwa na upungufu wa lita milioni 70.4 kwa siku. Kutokana na hali hiyo, Wizara imeendelea kutekeleza mipango ya muda mfupi inayolenga kukabiliana na adha ya upatikanaji wa maji ambapo utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi na uboreshaji wa mtandao wa majisafi Nzuguni umekamilika. Mradi huo unawanufaisha wakazi wapatao 75,968 wa maeneo ya Nzuguni, Ilazo, Swaswa na Kisasa. Aidha, Serikali imeanza kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa mtandao wa majisafi Nzuguni kwa gharama ya Shilingi 5,509,671,097.11. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ufungaji wa pampu tano

(5); ujenzi wa jengo la kuendeshea visima; ulazaji wa mabomba kutoka kwenye visima na kupeleka maji kwenye tanki umbali wa kilomita 4.3; kubadilisha mabomba ya kusambaza maji kwa kuweka yenye kipenyo kikubwa umbali wa kilomita 20; na ufungaji wa mfumo wa SCADA wa kuendeshea visima. Mradi upo kwenye hatua za awali za utekelezaji na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025 na kuwanufaisha wakazi wapatao 80,000 wa Jiji la Dodoma.

Mheshimiwa Spika, pia, Wizara inatekeleza mradi wa kupanua na kuboresha huduma ya majisafi kwenye maeneo ya Dodoma mjini na Chamwino kwa gharama ya Shilingi 4,181,321,572.74. Kazi zinazotekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 64.387 kati ya kilomita 146.437 zilizopangwa;

56​


ujenzi wa chemba 84; ujenzi nguzo 143 za alama katika njia ya bomba za maji; na ujenzi wa nguzo za kushikilia mabomba. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2024 na kunufaisha wakazi wapatao 150,000 wa Dodoma na Chamwino.

Miradi ya Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Miji ya Vwawa – Mlowo


Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji katika Miji ya

Vwawa na Mlowo unaogharimu Shilingi 2,205,767,425.21. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni uchimbaji wa kisima kirefu eneo la Hasanga; ujenzi wa tanki la kukusanya maji la lita 75,000; ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji la lita 250,000 eneo la Ichenjezya; ujenzi wa uzio kuzunguka tanki; ununuzi na ulazaji wa mabomba katika njia kuu umbali wa kilomita 2.46; ulazaji wa mabomba ya mtandao wa kusambaza maji umbali wa kilomita 39.25 kati ya kilomita 48.7 zilizopangwa; na ujenzi wa nyumba ya pampu. Kazi zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 9.45; uchimbaji, ununuzi na ufungaji wa pampu nne (4); ununuzi na ufungaji wa dira kubwa za maji 21 kwa ajili ya kupima maji; ununuzi wa gari na pikipiki sita

(6); ununuzi na ufungaji wa jenereta na mashine ya kuunga mabomba; na uwekaji wa umeme kwenye chanzo. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 64 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wakazi wapatao 23,294.


57​


Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa ukarabati wa vyanzo vya maji vya Mwasanya na Mlowo kwa gharama ya Shilingi 1,763,598,600. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 17.35, ujenzi wa chemba 17, uwekaji wa alama za bomba (marker post), ukarabati wa jengo la ofisi, ununuzi wa pikipiki tano (5), ununuzi wa kompyuta tatu (3) na ukarabati wa uzio kuzunguka chujio la maji lililopo Mlowo. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi iliyotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 15.442. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuwanufaisha wakazi wapatao 13,294.

Kuboresha Huduma ya Majisafi katika Manispaa ya Iringa na Maeneo ya Pembezoni


Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Kilolo unaogharimu Shilingi 825,812,568.80. Mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji ya mtiririko cha Mwosongela II chenye uwezo wa kuzalisha maji lita

691,000 kwa siku; na ulazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 16.2 kutoka kwenye chanzo hadi kwenye tanki lililopo eneo la Luganga. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi iliyotekelezwa ni ujenzi na ulazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 14.256. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 88 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 6,871.


58​


Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara imeendelea na uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Ilula na vijiji vya Imalutwa na Mazombe kwa gharama ya Shilingi 445,739,445.15. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki la lita 75,000; ulazaji wa bomba la kusafirisha maji umbali wa kilomita 3.4; na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 6.3. Kazi inayoendelea ni ujenzi wa vituo sita (6) vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 7,455.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Ismani - Kilolo kwa gharama ya Shilingi 9,270,306,365. Hadi mwezi Aprili, 2024, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuboresha chanzo cha maji Mgera; ununuzi na ufungaji wa pampu mbili (2); ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 84 kati ya kilomita 111.8 zilizopangwa; ujenzi wa matanki nane (8) yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 1.725; na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 89.54 kati ya kilomita 106.99 zilizopangwa. Kazi zinazoendelea ni upanuzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji Ndiuka, ukarabatia wa vituo 14 vya kuchotea maji na ufungaji wa dira za maji 1,000. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 58,821.










59​


Kuboresha Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Songea na Maeneo ya Pembezoni

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi eneo la Mwengemshindo kwa gharama ya Shilingi 547,521,500. Kazi zilizotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita

Kukamilika kwa mradi huo, kumeimarisha huduma ya maji kwa wakazi wapatao 3,000 wa eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji katika eneo la viwanda - Lilambo kwa gharama ya Shilingi 415,980,885. Kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa nyumba ya pampu; ununuzi na ufungaji wa pampu; ujenzi wa tanki la lita 100,000; ununuzi na ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 5; ununuzi na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 8.1; ujenzi wa uzio kuzunguka tanki; na ujenzi wa mfumo wa kutibu maji. Kukamilika kwa mradi kumenufaisha viwanda 200 vilivyopo eneo la Lilambo.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa maji katika eneo la Subira unaogharimu Shilingi 1,168,863,390. Mradi huo unahusisha ujenzi wa nyumba mbili (2) za pampu; ununuzi na ufungaji wa pampu mbili (2); ujenzi wa tanki la lita 200,000; ununuzi na ulazaji wa mabomba katika mtandao wa kusambaza maji umbali wa kilomita 42.5; na ujenzi wa mfumo wa kutibu maji. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ununuzi wa mabomba

60​


yenye jumla ya urefu wa kilomita 39.6 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 17. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 12,691.

Kuboresha Huduma ya Maji katika Manispaa ya Mtwara na Maeneo ya Pembezoni


Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chujio la maji katika eneo la Mangamba kwa gharama ya Shilingi 3,451,853,994. Kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa tanki la maji kwa ajili ya huduma ya zimamoto; ununuzi na ufungaji wa mabomba na viungio; ujenzi wa jengo la pampu; ufungaji wa pampu; ukarabati wa karakana; na ujenzi wa mifumo ya usalama ya umeme. Kukamilika kwa mradi huo, kumewezesha wakazi wa Mji wa Mtwara kupata huduma ya maji yaliyosafishwa na kutibiwa kwa viwango vinavyokubalika.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara inaendelea kutekeleza mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Mtwara kwa gharama ya Shilingi 20,361,599,950. Mradi huo unatekelezwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa matanki mawili (2) yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 7; pamoja na ukarabati wa mtandao wa bomba kuu. Awamu ya pili inahusisha ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 500,000. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 85 na awamu ya pili umefikia asilimia 35. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2024 na kuboresha hali ya upatikanaji

61​


wa huduma ya maji kwa wakazi 139,336 wa Mji wa Mtwara.

3.2.4.2. Miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa

(a) Miji ya Tinde na Shelui


Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya India kupitia Benki ya Exim - India imekamilisha utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa kuboresha huduma ya maji katika miji ya Tinde na Shelui kwa gharama ya Shilingi 24,753,848,782. Vilevile, katika kuhakikisha wananchi wengi zaidi wa miji hiyo wanafikiwa na huduma ya maji, Serikali inaendelea na upanuzi wa mradi huo ambapo hadi mwezi Aprili 2024, ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 7.6 umekamilika kwa gharama ya Shilingi 1,150,000,000. Awamu ya pili ya mradi inahusisha upanuzi wa mtandao wa usambazaji maji katika miji ya Tinde na Shelui itakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani 6,000,000. Taratibu za kupata kibali cha kuanza utekelezaji wa awamu hiyo kutoka Serikali ya India zinaendelea. Mradi huo utakapokamilika utawanufaisha wakazi wapatao 86,983 wa miji hiyo.

Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Mji wa Turiani

Mheshimiwa Spika
, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Turiani kwa gharama ya Shilingi

62​


3,905,699,196. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 150,000 na chujio katika Kijiji cha Luamba; ujenzi wa vyanzo vitatu (3) vya maji vya mserereko katika vijiji vya Luamba, Mlaguzi na Ubiri; ulazaji wa mabomba za kusafirisha na kusambaza maji umbali wa kilomita 70; na ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizoanza kutekelezwa ni ujenzi wa tanki, ujenzi wa vyanzo vya maji viwili (2) vya Luamba na Mlaguzi; na ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 15. Kwa wastani utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 40,700.

Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Tunduma

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha awamu ya kwanza ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya maji katika Mji wa Tunduma uliogharimu Shilingi 818,237,830. Kazi zilizotekelezwa ni ununuzi na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 6.6; ujenzi wa vituo vitano (5) vya kuchotea maji; ununuzi wa dira za maji 100 na viungio vya maunganisho mapya; ujenzi wa uzio; na ununuzi wa pikipiki tatu (3). Mradi unatoa huduma kwa wananchi wapatao 15,562 wa mji huo.


Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea na utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya maji katika Mji wa Tunduma kwa gharama ya Shilingi 918,626,905.5. Kazi zinazoendelea kutekelezwa ni ujenzi wa tanki la lita 50,000; ulazaji wa

63​


mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 14.5; utafiti wa waji chini ya ardhi katika maeneo 16; uchimbaji wa visima virefu sita (6); ununuzi wa transfoma 50KVA; ujenzi wa nyumba za mitambo mbili (2); uvutaji wa umeme wa njia tatu; ujenzi wa chemba 14 na ufungaji wa pampu nne (4). Hadi mwezi Aprili, 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuwanufaisha wananchi 25,071 wa mji huo.

(d) Mradi wa Kitaifa wa HTM


Mheshimiwa Spika
, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa maji Segera-Kabuku ambao ni sehemu ya mradi wa kitaifa wa Handeni Trunk Main (HTM) kwa gharama ya Shilingi 25,585,976,283.13. Mradi huo unalenga kuwapatia huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza wananchi wa vijiji 15 vya Kwamgwe, Chanika Kofi, Seza Kofi, Bondo, Kwadoya, Ngojoro, Kwedizinga, Ugweno, Taula, Kwedibago, Kabuku Nje, Kabuku Mjini, Komsanga, Kabuku Kaskazini na Kabuku Ndani pamoja na Kambi ya Jeshi Mgambo-Kabuku. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizoanza kutekelezwa ni ununuzi wa mabomba yenye jumla ya urefu wa kilomita 10 na ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 2. Kazi nyingine za mradi zinahusisha ujenzi wa kidakio cha maji; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 6.27 kwa siku; ulazaji wa mabomba umbali wa kilomita 106; ujenzi wa jengo la mitambo; na jengo la maabara. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024 na kuwanufaisha wananchi wapatao 120,000.

64

(e) Mradi wa Maji Mugango – Kiabakari – Butiama


Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (Saudi Fund for Development – SFD) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji utakaohudumia maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama kwa gharama ya Dola za Marekani 30,690,000. Kazi zinazoendelea kutekelezwa ni ujenzi wa choteo la maji katika Ziwa Victoria; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; pamoja na ujenzi wa mantaki manne (4) yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 7 katika maeneo ya Kong, Kiabakari, Butiama Hill na Bumangi; ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 48 kutoka Mugango kwenda Kiabakari hadi Butiama; ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 140; ujenzi wa ofisi na nyumba za wasimamizi wa mitambo; ukarabati wa matanki mawili (2) katika maeneo ya Kyatungwe na Bisarye; ujenzi wa vioski 40 vya maji na ununuzi wa dira za maji 2,000. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 98.5 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Mradi huo utawanufaisha zaidi ya wananchi 100,000 waliopo katika eneo la mradi; vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu; na wananchi wa Kata ya Nyamswa yenye vijiji vya Nyamswa, Makongoro A, Makongoro B na Bukama ambao watanufaika na upanuzi wa mradi huo.

(f) Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe


Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Mashirika ya BADEA, OPEC Fund na Kuwait Fund

65​


inaendelea kutekeleza mradi wa maji Same – Mwanga - Korogwe utakaohudumia Miji ya Same na Mwanga pamoja na vijiji 38 kwenye Wilaya za Same na Mwanga na vijiji vitano (5) katika Wilaya ya Korogwe. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa chanzo; ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; ujenzi wa matanki 16 yenye ukubwa kuanzia lita laki 3 hadi lita milioni 9; ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 260; na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 306. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa chanzo; ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme; ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 81.7; ulazaji wa mabomba ya mtandao wa kusambaza maji umbali wa kilomita 207 katika Miji ya Same na Mwanga; ujenzi wa mtambo wa kusafisha na kutibu maji; na ujenzi wa matanki saba (7) ya kuhifadhi maji. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 86.7 na kwa sasa upo kwenye majaribio ya kutoa maji kutoka katika chanzo kuyapeleka kwenye chujio. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi 456,931 wa wilaya za Same, Mwanga na Korogwe.


Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Sengerema

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Nyasigu – Lubungo – Ngoma kwa gharama ya Shilingi 13,742,895,491.14. Mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo la mtambo wa kusukuma maji; ufungaji wa pampu; ujenzi wa mtambo

66​


wa kusafisha na kutibu maji wenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 12 kwa siku; ujenzi wa matanki matatu

yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 2.6; ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 108.4; ujenzi wa vituo 70 vya kuchotea maji; ununuzi wa gari na pikipiki saba (7); ujenzi wa chemba; ujenzi wa jengo la ofisi kuu na jengo la ofisi ya uendeshaji eneo la Ngoma; ujenzi wa njia ya umeme kutoka Nyasigu hadi katika chanzo cha Mabiru; na uunganishaji wa wateja wa majumbani. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizoanza kutekelezwa ni ujenzi wa njia ya umeme kutoka Nyasigu hadi kwenye chanzo cha Mabiru; ujenzi wa jengo la mtambo wa kusukuma maji; ujenzi wa jengo la ofisi kuu na jengo la ofisi ya uendeshaji eneo la Ngoma. Kwa wastani, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 30 unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024 na utawanufaisha wakazi wapatao 20,024 wa maeneo ya Nyasigu, Lubungo na Ngoma.

Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Mafinga

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Mafinga unaogharimu kiasi cha Shilingi 866,957,377. Mradi huo unahusisha ununuzi na ufungaji wa pampu; ukarabati wa banio la maji la Ikangafu, ukarabati wa tanki la kutibu maji; ukarabati wa nyumba ya kuendeshea mitambo; ukarabati wa mtambo wa kutibu maji; na ukarabati wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 13.5. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ukarabati wa nyumba ya kuendeshea mitambo na ununuzi wa mabomba yenye

67​


urefu wa kilomita 11.06. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 18 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2024. Mradi huo utaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi 48,807.

Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Busega

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi katika kata za Nyashimo, Lamadi na Mkula uliogharimu Shilingi 685,000,509. Kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba katika njia kuu ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 3 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 20. Mradi unatoa huduma kwa wananchi wapatao 8,290 wa kata hizo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea na mradi wa kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Nyashimo, Mkula na Shule ya Sekondari Mwabayanda kwa gharama ya Shilingi 639,772,790.70. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 23; ufungaji wa surge tank; na ufungaji wa pampu tatu (3). Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 17.4 na ufungaji wa pampu moja. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia

na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi wapatao 7,103 wa maeneo hayo.






68​


Mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji Ngara Mjini

Mheshimiwa Spika
, Wizara inatekeleza mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Ngara kwa gharama ya Shilingi 1,256,556,468.93. Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na ununuzi na ufungaji wa Pampu; ufungaji wa control pannel; ujenzi wa tanki la lita 200,000; ulazaji wa mabomba ya kusafirisha maji umbali wa kilomita 16.06; ukarabati wa jengo la mitambo; ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la jengo la mitambo; na ufungaji wa miundombinu ya umeme kwenye jengo la mitambo. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 16 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2024 na kuwanufaisha wakazi wapatao 13,560 wa Mji wa Ngara.

Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Miji 28

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika miji 28 ambapo miradi katika miji 24 inatekelezwa kupitia fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim na miradi katika miji minne (4) inatekelezwa kwa fedha za ndani. Mradi unatekelezwa kwa utaratibu wa usanifu na ujenzi (Design & Build) na kwa mujibu wa Mkataba, mradi unatarajiwa kukamilika mwaka 2025/26. Aidha, misamaha ya kodi imepatikana na malipo ya awali yamefanyika kwa Wakandarasi wote wa miji 28. Hadi mwezi Aprili 2024, Wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa miradi na hatua zilizofikiwa ni kama

69​

ifuatavyo:-


Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Kipande cha Kwanza kinachohusisha Miji ya Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani umefikia asilimia 30; Kipande cha Pili chenye Miji ya Kilwa Masoko na Nanyumbu (asilimia 28); Kipande cha Tatu chenye Miji ya Ifakara,

Rujewa, Chunya, Njombe, Makambako na Wanging’ombe (asilimia 9); Kipande cha Nne chenye Miji ya Kiomboi, Singida, Manyoni, Mugumu, Chemba na Chamwino (asilimia 9); Kipande cha Tano chenye Miji ya Kasulu, Mpanda, Sikonge, Urambo na Kaliua (asilimia 40); Kipande cha Sita chenye Miji ya Kayanga, Chato na Geita (asilimia 10); Kipande cha Saba kinachohusisha mradi wa Makonde Plateau chenye Miji ya Newala, Nanyamba, Tandahimba na sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (asilimia 23.5); Kipande cha Nane chenye Mji wa Mafinga (asilimia

5)
; Kipande cha Tisa chenye Miji ya Rorya na Tarime (asilimia 13); na Kipande cha Kumi chenye Mji wa Songea, utekelezeji umefikia asilimia 3. Kwa mujibu wa Mkataba, mradi huo wa miji 28 unatarajiwa kukamilika mwaka 2025/26.


Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Mkoa wa Simiyu

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund - GCF) inatekeleza Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa gharama ya Euro

70​


171,000,000. Mradi huo unatekelezwa kwenye wilaya tano (5) za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu katika Mkoa wa Simiyu. Utekelezaji wa mradi utahusisha ujenzi wa chanzo chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 73.2 kwa siku; ulazaji wa mtandao wa bomba kuu la kusafirisha maji umbali wa kilomita 151; ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 358.93; ujenzi wa matanki sita (6) yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 39.5; ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 1.1 ndani ya Ziwa Victoria; ujenzi wa kituo cha kusukuma maji ghafi; ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 2.75 kutoka kituo cha kusukuma maji ghafi hadi kituo cha kusafisha maji; ufungaji wa SCADA System; ujenzi wa kituo cha kusafisha na kutibu maji chenye ujazo wa lita milioni 69.5 kwa siku; ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika eneo la Nyangokolwa; ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mitambo, nyumba ya mlinzi, jengo la ofisi na nyumba ya mtambo wa kusuma maji; na ununuzi wa dira za maji 2,800. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zinazoendelea ni maandalizi ya awali ya kuleta vifaa vya ujenzi na wataalam; na upimaji (survey) wa njia kuu yatakapopita mabomba pamoja na maeneo yanayotarajiwa kujengwa matanki. Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wananchi wapatao 662,500 wa Wilaya hizo.


3.2.4.3. Miradi ya Usafi wa Mazingira

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeendelea kuboresha huduma ya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mijini kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya uondoshaji majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, mtandao wa majitaka mijini umefikia kilomita

71​


1,455.93 kutoka kilomita 1,416.93 mwezi Aprili, 2023. Vilevile, maunganisho ya huduma ya uondoshaji majitaka yameongezeka kutoka wateja 56,923 mwezi Aprili, 2023 hadi wateja 58,650 mwezi Aprili, 2024. Miradi ya uondoshaji majitaka inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na: -

Kuboresha Huduma ya Uondoshaji Majitaka katika Jiji la Tanga

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka kutoka Duga hadi Makorora katika Jiji la Tanga unaogharimu Shilingi 509,234,651. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa nyumba ya pampu; ununuzi na ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 3.2 na ujenzi wa chemba 30. Hadi mwezi Aprili 2024, mradi umefikia asilimia 80 na kazi iliyotekelezwa ni ujenzi wa chemba

Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 3,500 wa maeneo ya Duga na Makorora.


Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Majitaka katika Mji wa Muheza

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika Mji wa Muheza kwa gharama ya Shilingi 1,013,234,000. Utekelezaji wa mradi unahusisha ujenzi wa mtambo wa kutibu tope kinyesi; ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya kukusanya majitaka; ununuzi wa gari la usimamizi wa mradi; ununuzi wa gari la uondoshaji wa majitaka; na ujenzi wa vyoo vitatu (3) katika maeneo ya

72​


stendi, choo kimoja (1) na shule vyoo viwili (2). Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi unaendelea na umefikia asilimia 85. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2024 na kuimarisha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 38,131.

Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Majitaka katika Mji wa Pangani

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika Mji wa Pangani kwa gharama ya Shilingi 995,519,888. Utekelezaji wa mradi unahusisha ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka; ununuzi wa gari la uondoshaji wa majitaka; ununuzi wa gari la usimamizi wa mradi na ujenzi wa vyoo vitatu (3) katika maeneo ya stendi, choo kimoja (1) na shule vyoo viwili (2). Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi unaendelea na umefikia asilimia 90. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2024 na kuimarisha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazo wapatao 38,131.

Kuboresha Huduma ya Uondoshaji Majitaka katika Jiji la Mwanza

Mheshimiwa Spika
, katika kuboresha huduma ya uondoshaji majitaka katika Jiji la Mwanza, Wizara imetekeleza na kukamilisha mradi wa upanuzi wa mabwawa ya kutibu majitaka kwenye Manispaa ya Ilemela kwa gharama ya Shilingi 6,739,048,681.80. Aidha, ujenzi wa mfumo rahisi wa uondoshaji majitaka uliogharimu Shilingi 3,720,864,077.92 umekamilika katika maeneo ya Mabatini, Kilimahewa A, Kilimahewa

73​

B na Pasiansi. Vilevile, ujenzi wa mfumo rahisi wa

uondoshaji majitaka uliogharimu Shilingi 3,844,768,482.50 umekamilika kwenye sehemu za milimani katika maeneo ya Igogo – Sahara, Kabuhoro, Isamilo, na Ibungiro. Kukamilika kwa miradi hiyo kumeboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 355,000 wa maeneo hayo.


Kuboresha Huduma ya Uondoshaji Majitaka katika Jiji la Dar es Salaam

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa mfumo rahisi wa uondoshaji majitaka na mtambo wa kutibu majitaka katika Jiji la Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi 9,022,243,047.85. Mradi unahusisha ujenzi wa mtandao wa majitaka wenye urefu wa kilomita 54.5 na ujenzi wa mitambo minne (4) ya kutibu majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji umefikia asilimia 12 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2024. Mradi utakapokamilika utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 36,000 wa maeneo ya Kinyerezi, Kipawa, Buguruni - Kisiwani, Mivinjeni, Mikocheni, Faru na Kombo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea na ujenzi wa mtandao wa uondoshaji majitaka na kituo cha kusukuma majitaka eneo la Mbezi Beach kwa gharama ya Shilingi 52,407,401,646.15. Kazi zinazotekelezwa ni ujenzi wa mtandao wa majitaka umbali wa kilomita 101 ambapo kilomita 53.1 zimejengwa; ujenzi wa vituo viwili

(2) vya kusukuma majitaka; na ujenzi wa chemba za majitaka 2,383. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji

74​


umefikia asilimia 44 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024. Mradi huo utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 130,000 wa Mbezi Beach.

Mradi wa Ukarabati wa Mfumo wa Majitaka katika Maeneo ya Area C na Area D katika Jiji la Dodoma


Mheshimiwa Spika
, utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa mfumo wa majitaka unaendelea katika maeneo ya Area C na Area D yaliyopo Jijini Dodoma. Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 4,958,631,400 na unahusisha ujenzi wa chemba 962 za majitaka na ukarabati wa mabomba ya majitaka umbali wa kilomita 19. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa chemba 936 za majitaka na ukarabati wa mabomba ya majitaka umbali wa kilomita

Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 96 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na kuboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi 16,200 wa maeneo ya Area C na Area D.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara inaendelea na ujenzi wa mtandao wa majitaka katika eneo la Chamwino – Ikulu kwa gharama ya Shilingi 452,288,600. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa chujio la majitaka; ujenzi wa chemba 30; ulazaji wa bomba za majitaka umbali wa mita 500; na ujenzi wa mabwawa mawili ya majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa kazi zilizopangwa unaendelea na umefikia asilimia 50. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024 na kuboresha huduma ya uondoshaji

75​


majitaka kwa wakazi 300 wa maeneo ya Chamwino – Ikulu.

Mradi wa Upanuzi wa Mfumo wa Majitaka katika Maeneo ya Korongoni na Longuo “A” Manispaa ya Moshi

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha mradi wa kuboresha huduma ya uondoshaji wa majitaka katika

Kata za Korongoni na Longuo “A” zilizopo katika

Manispaa ya Moshi kwa gharama ya Shilingi 1,000,000,000. Mradi huo ulihusu upanuzi wa mfumo wa uondoshaji wa majitaka. Kukamilika kwa mradi kumeboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 7,500 wa kata hizo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mtandao wa majitaka kuunganisha kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi kwa gharama ya Shilingi 2,118,431,709.38. Mradi huo unahusu ujenzi wa mtandao wa majitaka wenye urefu wa kilomita 12.99. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 15 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024.

Kuboresha Huduma ya Uondoshaji Majitaka katika Jiji la Arusha

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na ujenzi wa mtandao wa majitaka kutoka eneo la Kisongo hadi Olasiti kwa gharama ya Shilingi 2,515,456,580. Kazi zinazoendelea kutekelezwa ni upimaji na usanifu wa njia mpya ya mtandao wa majitaka; ujenzi wa chemba 188

76​


za majitaka; na ulazaji wa bomba za mtandao mpya wa majitaka umbali wa kilomita 9.21. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 36 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025. Mradi utakapokamilika utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 1,200.


Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Majitaka katika Mji wa Nzega

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya uondoshaji wa majitaka katika Mji wa Nzega kwa gharama ya Shilingi 1,586,916,242. Mradi huo ulihusisha ujenzi wa chemba ya kupokea majitaka; ujenzi wa mabwawa ya anaerobic mawili (2) na facultative mawili (2); ujenzi wa jengo la mlinzi; ujenzi wa eneo oevu; ujenzi wa mfumo wa kukausha topekinyesi; uwekaji wa geomembrane; na ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la mabwawa. Mradi unatoa huduma ya uondoshaji wa majitaka kwa wananchi wapatao 133,000 wa Mji huo.




Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Kutibu Majitaka katika Manispaa ya Singida

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kutibu majitaka katika Manispaa ya Singida unaogharimu Shilingi 1,764,606,000. Utekelezaji wa mradi unahusisha ujenzi wa mabwawa ya kusafisha majitaka, ujenzi wa jengo la walinzi, eneo oevu, ujenzi wa maabara, ujenzi wa jengo la ofisi na ununuzi wa gari

77​


la uondoshaji wa majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi inayoendelea ni ujenzi wa mabwawa ya kusafisha majitaka na utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 50. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2024 na utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi 112,934.

Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Kutibu Majitaka Omurushaka/Kayanga

Mheshimiwa Spika
, utekelezaji wa mradi wa

ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka Omurushaka/Kayanga unahusisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 1.2 kutoka barabara kuu kwenda kwenye mabwawa; ujenzi wa mabwawa mawili

(2) ya anaerobic; ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya Facultative; ujenzi wa mabwawa matatu (3) ya maturation; ujenzi wa jengo la walinzi; ujenzi wa mfumo wa kukausha topekinyesi; ununuzi wa vifaa vya kupima ubora wa majitaka yanayorudishwa kwenye mazingira; na ununuzi wa gari la uondoshaji wa majitaka. Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 1,071,954,550.84. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Mradi unatarajiwa kuboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 45,000 wa eneo hilo.


Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Kutibu Majitaka Kyaka-Bunazi

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka Kyaka – Bunazi unatekelezwa kwa

78​


gharama ya Shilingi 970,355,684. Mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 800 kutoka barabara kuu kwenda kwenye mabwawa; ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya anaerobic; ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya Facultative; ujenzi wa mabwawa matatu (3) ya maturation; ujenzi wa jengo la walinzi; ujenzi wa mfumo wa kukausha topekinyesi; ununuzi wa vifaa vya kupima ubora wa majitaka yanayorudishwa kwenye mazingira; na ununuzi wa gari la uondoshaji wa majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 15 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 na utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 35,000.

Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Majitaka katika Mji wa Chato

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika Mji wa Chato unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 1,594,256,565. Mradi huo unahusu ujenzi wa mabwawa ya majitaka; ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la mabwawa; na ununuzi wa magari mawili (2) ya uondoshaji majitaka. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024. Mradi huo utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 16,000 wa mji huo.

Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Majitaka Eneo la Ngalanga katika Mji wa Njombe

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa mabwawa ya majitaka katika eneo la Ngalanga katika Mji wa

79​


Njombe unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 1,240,186,800. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mabwawa ya anaerobic mawili (2) na mabwawa ya facultative mawili (2); ujenzi wa wetland; ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la mabwawa; ujenzi wa maabara na jengo la walinzi; na ununuzi wa gari la uondoshaji majitaka. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi ya ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka inaendelea na utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 10. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2024 na utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka wa wakazi wapatao 90,353 wa eneo hilo.

Mradi wa Kuboresha Huduma ya Usafi wa Mazingira katika Kata ya Sinde Jijini Mbeya

Mheshimiwa Spika
, Wizara imekamilisha utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya usafi wa mazingira katika Kata ya Sinde Jijini Mbeya kwa gharama ya Shilingi milioni 167.07. Kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 1.5; ujenzi wa chemba 71 za majitaka; ukarabati wa bomba umbali wa mita 220; na ukarabati wa chemba 12. Kukamilika kwa mradi huo kumeboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 5,800 wa Kata hiyo.


Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Majitaka katika Manispaa ya Musoma

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa miundombinu ya uondoshaji wa majitaka katika Manispaa ya Musoma unatekelezwa na Wizara kwa

80​


kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa gharama ya Shilingi 30,812,999,179.47. Mradi huo unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kukusanya majitaka katika kata za Kitaji, Iringo, Mwigobero, Mwisenge na Mkendo; ujenzi wa vituo vinne (4) vya kusukuma majitaka; ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka katika Kata ya Makoko; na ujenzi wa vyoo 60 katika shule za msingi na vyoo vitano (5) kwa ajili ya masoko na machinjio. Hadi mwezi Aprili 2024, kazi inayoendelea ni ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka na utekelezaji umefikia asilimia 48. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2024 na utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 12,209.

Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Kutibu Majitaka katika Manispaa ya Tabora

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa mabwawa ya majitaka katika Manispaa ya Tabora unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 1,613,830,289.76. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya anaerobic, ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya Facultative, ujenzi wa wetland, ujenzi wa mfumo wa kukausha topekinyesi, ujenzi wa uzio, ujenzi wa incinerator, matengenezo ya barabara kwenda kwenye mabwawa ya majitaka na ujenzi wa mtaro wa kuondosha maji yaliyotibiwa. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 35 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2024. Mradi huo utaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 16,353.




81​


Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya Majitaka katika Mji wa Babati

Mheshimiwa Spika
, mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka katika Mji wa Babati unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi 6,900,000,000. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mabwawa mawili (2) ya anaerobic, ujenzi wa bwawa la Facultative, ujenzi wa bwawa la maturation, ujenzi wa mfumo wa kukausha topekinyesi na ujenzi wa mtaro wa kuondosha maji yaliyotibiwa. Hadi mwezi Aprili 2024, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 67 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kukamilika kwa mradi huo kutaboresha huduma ya uondoshaji majitaka kwa wakazi wapatao 389,000.

3.2.5. Gridi ya Taifa ya Maji

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na maandalizi ya Gridi ya Taifa ya Maji na kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ya kuajiri Mtaalam Mshauri atakayefanya upembuzi yakinifu wa mpango huo. Aidha, Wizara imeanza kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito mikubwa na mabwawa kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya uhakika vya maji. Kwa mfano; mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao umenufaisha Miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga na Shelui. Vilevile, taratibu za manunuzi za kumpata mtaalam mshauri wa kutoa maji Ziwa Tanganyika na kuyapeleka katika mikoa ya Katavi, Rukwa mpaka Kigoma zimeanza. Pia, Wizara imesaini Mkataba na Mtaalam Mshauri atakaefanya upembuzi

82​


yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria na kuyapeleka Dodoma.

3.2.6. Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji (National Water Master Plan)

Mheshimiwa Spika
, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeanza zoezi la uandaaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji katika mikoa ya Rukwa, Njombe na Dodoma. Kupitia mpango huo miradi yote itabainishwa na kuanza kusanifiwa kulingana na vipaumbele vya mikoa na wilaya husika. Mpango huo utaainisha vyanzo vya maji katika maeneo husika, aina ya miundombinu inayofaa kutumika katika maeneo hayo, teknolojia ya usambazaji maji inayofaa kwa eneo husika, teknolojia inayofaa ya kusafisha na kutibu maji, na kama hakuna chanzo cha uhakika mpango utabainisha vyanzo vitakavyotumika kupeleka maji kwenye maeneo yasiyo na vyanzo na hatimaye kujua kiwango cha uwekezaji kinachohitajika. Katika mwaka 2024/25 zoezi hilo litaendelea katika mikoa mingine iliyobaki.

3.2.7. Matumizi ya Dira za Maji za Malipo Kabla

Mheshimiwa Spika
, matumizi ya dira za maji za malipo kabla (pre-paid water meters) yana manufaa makubwa ikilinganishwa na dira za kawaida (post-paid water meters) ikiwemo kukusanya madeni na kuimarisha ufanisi katika makusanyo ya maduhuli; kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji pamoja na kudhibiti mivujo inayosababisha hasara kwa mteja. Kwa kutambua umuhimu wa dira hizo, Wizara kupitia Mamlaka za Maji na CBWSOs zimeendelea kuwafungia

83​


wateja ambapo hadi mwezi Aprili 2024, wateja 13,526 wamefungiwa dira kati ya wateja 2,019,951 wa vijijini na mijini. Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira zilizowafungia wateja dira hizo ni pamoja na Iringa ambayo imefunga dira 6,544, Dodoma (1,085), Tanga (627); na kwa upande wa vijijini, RUWASA imefunga jumla ya dira 1,986 kwenye mikoa mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ufanisi ulioonekana kwenye matumizi ya dira za maji za malipo kabla ikiwemo kupunguza malalamiko ya wateja kwenye ankara za maji, mnamo tarehe 4 Machi, 2024, Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
aliielekeza Wizara ya Maji kuongeza kasi ya ufungaji wa dira za maji za malipo kabla ili kuwafikia wananchi wote nchini. Katika kutekeleza agizo hilo, Wizara imeandaa Mkakati wa Kuongeza Kasi ya Ufungaji wa Dira za Maji za Malipo Kabla ambapo kupitia Mkakati huo asilimia 50 ya wateja wa maji vijijini na mijini watafungiwa dira hizo ifikapo Desemba 2025. Utekelezaji wa Mkakati huo umezingatia masuala muhimu yakiwemo kuandaa mpango wa pamoja wa ununuzi wa dira ili kurahisisha upatikanaji wake na kwa bei nafuu; kuunda mfumo jumuishi wa TEHAMA wa dira za maji za malipo kabla ili kuondoa utegemezi wa mifumo ya Wazabuni; kuhamasisha wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji wa dira hizo; na kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya dira hizo.








84​

3.2.8. Udhibiti wa Huduma ya Maji Mijini

Mheshimiwa Spika
, huduma za maji mijini zinadhibitiwa na EWURA kupitia Kifungu Na. 414 cha Sheria Na.11 ya EWURA ya mwaka 2001. Sheria hiyo inaitaka EWURA kudhibiti utoaji wa huduma kwenye Sekta za Maji na Nishati katika maeneo ya maji na usafi wa mazingira, umeme, mafuta ya petroli pamoja na gesi asilia. Majukumu ya EWURA ni pamoja na kutoa leseni, kusimamia utekelezaji wa masharti ya leseni, kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma, kutathmini na kupitisha bei za huduma na kutatua migogoro baina ya watoa huduma na wateja wao.

Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2024, EWURA ilitoa leseni nne (4) za kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Miji ya Rombo, Kyela-Kasumulu, Njombe na Busega. Aidha, EWURA ilitathmini na kuidhinisha bei mpya za huduma ya maji kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira saba

ambazo ni Dodoma, Makonde, Sumbawanga, Orkesumet, Mombo, Bariadi na Lindi. Vilevile, katika kipindi hicho, EWURA ilifanya mapitio ya mipango-biashara ya mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira 11 na kuidhinisha mikataba sita (6) ya huduma kwa mteja kwa mamlaka za Musoma, Liwale, Makambako, Lindi, Biharamulo na Geita.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, EWURA ilitoa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Taarifa hiyo inaainisha utendaji wa mamlaka za maji nchini na kuweza kusaidia

85​


Wizara pamoja na wadau wa sekta ya maji katika kuandaa na kutekeleza mipango mbalimbali ya kuimarisha na kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira. Taarifa hiyo, imebainisha kuwepo kwa mafanikio katika ongezeko la uzalishaji wa maji kwa lita bilioni 7 sawa na asilimia 1.78, kuongezeka kwa uwezo wa miundombinu ya kuzalisha maji kwa lita bilioni 126 sawa na asilimia 16.94 na kuongezeka kwa idadi ya wateja wanaopata huduma ya maji kwa asilimia 11. Aidha, taarifa imebainisha changamoto zinazokabili mamlaka za maji zikiwemo: kuongezeka kwa upotevu wa maji ambao umefikia asilimia 37, upungufu wa miundombinu ya huduma ya usafi wa mazingira; na uwiano usioridhisha wa ongezeko la mahitaji ya maji ikilinganishwa na uzalishaji wa maji.

3.3. Taasisi zilizo Chini ya Wizara

3.3.1.
Mfuko wa Taifa wa Maji

Mheshimiwa Spika
, Mfuko wa Taifa wa Maji ulianzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 44 cha Sheria Na. 12 ya mwaka 2009 ya Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Kwa sasa Mfuko unatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya Huduma za majisafi na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Mfuko ni Taasisi yenye dhamana ya kutafuta na kutoa rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji nchini. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mfuko ni kuwa na rasilimali fedha ya uhakika kwa ajili ya kusaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini pamoja na kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa vyanzo vya maji. Chanzo cha mapato cha Mfuko kwa

86​


sasa ni tozo ya Shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta ya diseli na petroli. Fedha hizo hutumika kutekeleza miradi ya maji inayosimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini na Bodi za Maji za Mabonde.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, Mfuko uliidhinishiwa Shilingi 175,912,837,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji. Hadi mwezi Aprili, 2024, kiasi cha fedha kilichopokelewa ni Shilingi 102,657,068,560.15 sawa na asilimia 58.4. Fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi ya maji kwenye maeneo mbalimbali nchini na kipaumbele kimetolewa kwa miradi inayoendelea na iliyo kwenye hatua za mwisho kukamilika ili wananchi wengi zaidi wanufaike na huduma ya maji kwa wakati. Jumla ya miradi 165 kati ya miradi 332 iliyopangwa kutekelezwa katika bajeti imepokea fedha ambapo miradi 46 imekamilika na inatoa huduma. Vilevile, Mfuko wa Taifa wa Maji umetoa fedha kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji ambapo takribani vyanzo 40 vimelindwa na kutunzwa kwa kuwekewa mipaka, kupanda miti na kuzuia shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo.

Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuongeza wigo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini, Mfuko umeanza rasmi kutumia dirisha lake la mikopo ya riba nafuu lililozinduliwa mwezi Aprili, 2023. Hadi mwezi Aprili 2024, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda imenufaika na dirisha hilo na Mamlaka nyingine 12 zimewasilisha maombi ya kupata mkopo. Aidha, Mfuko umeendelea kuzijengea uwezo taasisi zinazotekeleza miradi ya maji

87​


nchini kwa kutoa mafunzo ya uandaaji wa maandiko ya miradi (Bankable Project Proposals) kwa ajili ya kutafuta fedha za uwekezaji katika sekta ya maji. Hadi mwezi Aprili 2024, maandiko ya miradi mitatu (3) kutoka Mamlaka za Maji za Mafinga, Makambako na Morogoro yameandaliwa.

3.3.2. Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)

Mheshimiwa Spika
, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ni Taasisi iliyoanzishwa kwa Kifungu cha 42 cha Sheria Na. 5 ya Huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Taasisi hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira vijijini. Vilevile, Taasisi hiyo ina jukumu la kudhibiti bei za maji zinazotozwa na CBWSOs kwenye maeneo ya vijijni.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuijengea uwezo RUWASA ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira vijijini. Katika mwaka 2023/24, Serikali imenunua jumla ya magari 15 na pikipiki 395 kwa ajili ya kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na uendeshaji wa miradi ya maji vijijini. Magari hayo yamepelekwa katika mikoa 13 ya Tanga, Arusha, Njombe, Dodoma, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Kagera, Morogoro, Shinyanga, Mara, Tabora na Iringa na magari mawili (2) yamebaki RUWASA makao makuu. Pikipiki zilizonunuliwa zimepelekwa katika ofisi za RUWASA Wilaya na kwenye Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii.


88​

3.3.3. Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira


Mheshimiwa Spika
, Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Mamlaka hizo zina jukumu la kutoa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwenye maeneo ya mijini. Utendaji kazi wa Mamlaka unasimamiwa na Bodi za Wakurugenzi zinazoteuliwa na Waziri mwenye dhamana na Maji. Hadi sasa, kuna jumla ya mamlaka za maji 90 zinazojumuisha mamlaka 25 za miji mikuu ya mikoa, miradi ya kitaifa nane (8), miji mikuu ya wilaya (51) na miji midogo, mamlaka sita (6). Mamlaka hizo zimegawanywa kwenye madaraja kulingana na uwezo wa kujiendesha ambapo kuna mamlaka za madaraja AA, A, B na C. Mamlaka za Daraja AA ni zile zinazoweza kumudu gharama zote za uendeshaji, matengenezo na uwekezaji wa miundombinu ya maji; Mamlaka za daraja A ni zile zenye uwezo wa kumudu gharama zote za uendeshaji na matengenezo ikiwa ni pamoja na gharama za uchakavu wa mali; Mamlaka za daraja B ni zile zenye uwezo wa kumudu gharama za uendeshaji na matengenezo bila gharama za uchakavu wa mali; na Mamlaka za daraja C zina uwezo wa kumudu sehemu ya gharama za uendeshaji na matengenezo ambapo hupata ruzuku kutoka Serikalini kwa ajili kusaidia gharama za uendeshaji.


Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma na kupunguza utegemezi kwa Serikali, katika mwaka 2023/24, Wizara ilifanya tathmini kubaini uwezo wa kujiendesha kwa mamlaka za maji.

Matokeo ya tathmini hiyo ilizipandisha hadhi ya

89​


madaraja baadhi ya mamlaka ambapo mamlaka sita (6) zilitoka A kwenda AA; nne (4) kutoka daraja B kwenda A; tisa (9) kutoka daraja C kwenda B na mamlaka nne

ambazo hazikuwa daraja maalum kwenda daraja C. Kupandishwa kwa hadhi kwa mamlaka hizo kunaziongezea motisha katika kutoa huduma bora, kukusanya mapato, kupunguza utegemezi kwenye ruzuku na kuhimili gharama za uendeshaji.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada za kuimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma kwa mamlaka za maji, bado kumekuwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, upotevu wa maji, malalamiko ya bili za maji, migawo ya maji, wateja kuchelewa kuunganishiwa huduma na utegemezi kwenye ruzuku. Katika kukabiliana na changamoto hizo, mamlaka za maji zimeelekezwa kufunga dira za maji kwa wateja wote, kufunga dira za maji za malipo kabla kwa wateja wa majumbani na taasisi pamoja na kuhakikisha wateja wanaunganishiwa huduma kwa wakati kulingana na mkataba wa huduma kwa mteja (client service charter).

Mheshimiwa Spika, aidha, katika kupunguza utegemezi wa ruzuku, mamlaka za maji zimeelekezwa kutafuta vyanzo mbadala vya fedha za uwekezaji ambapo hadi sasa mamlaka 13 zimekopa fedha za uwekezaji kutoka kwenye taasisi za fedha. Mamlaka hizo ni Arusha, Iringa, Moshi, Singida, Kahama, Dar es Salaam, Bunda, Tanga, Tabora, Songea, Mtwara, Mwanza na Shinyanga. Vilevile, mamlaka zimetakiwa kutumia fursa zilizopo katika soko la hisa ili kupata mitaji ya uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu ya majisafi na majitaka. Katika kutekeleza maelekezo hayo,

90​


Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga, imekuwa mamlaka ya kwanza kuzindua uuzaji wa hati fungani ya kijani yenye thamani ya Shilingi 53,120,000,000, fedha ambazo zitatumika kuboresha huduma ya maji kwenye maeneo yanayohudumiwa na mamlaka hiyo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara imeendelea kuzijengea uwezo Mamlaka za maji kwa kujenga ofisi katika Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira ambapo jengo la ofisi la mamlaka ya Maji Arusha limekamilika; na ujenzi wa majengo unaendelea na umefikia hatua mbalimbali za utekelezaji katika mamlaka ya Maswa (asilimia 98), Sengerema (asilimia 75), Mugango-Kiabakari (asilimia 95), Kondoa (asilimia 95) na Biharamulo (100). Vilevile, Wizara imezipatia magari sita (6) Mamlaka za Maji za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Ushirombo, Ngara na Biharamulo kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na matengenezo.

3.3.4. Bodi za Maji za Mabonde


Mheshimiwa Spika
, Bodi za Maji za Mabonde (Basin Water Boards - BWBs) ni Taasisi zinazotekeleza majukumu yake kupitia Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Sura 331. Nchi yetu imegawanyika katika mabonde tisa (9) ambapo mgawanyo wake unatokana na mipaka ya kihaidrolojia. Mabonde hayo ni Pangani, Rufiji, Wami-Ruvu, Ruvuma na Pwani ya Kusini, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa na Bonde la Kati. Katika mwaka 2023/24, Bodi za Maji za Mabonde ziliendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya ufuatiliaji na tathmini

91​


ya rasilimali za maji nchini; kugawa na kudhibiti matumizi ya maji ili kuondoa migogoro; kuhifadhi na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji; na kuandaa na kutekeleza Mipango Shirikishi ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji. Katika kuziimarisha Bodi za Maji za Mabonde, Wizara imeendelea kuzijengea uwezo kwa kuzipatia ofisi, watumishi na vitendea kazi.

3.3.5. Chuo cha Maji

Mheshimiwa Spika
, Chuo cha Maji ni taasisi yenye jukumu la kuandaa wataalam wa maji, kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya maji. Chuo kinatoa mafunzo katika ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili (yaani Masters). Mafunzo yanayotolewa katika ngazi za Astashahada na Stashahada ni Uhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira (Water Supply and Sanitation Engineering); Uhandisi wa Umwagiliaji (Irrigation Engineering); Haidrojiolojia na Uchimbaji wa Visima (Hydrogeology and Water Well Drilling); Haidrolojia na Hali ya Hewa (Hydrology and Meteorology); Uhandisi wa Usafi wa Mazingira (Sanitation Engineering) pamoja na Teknolojia ya Maabara na Ubora wa Maji (Water Quality Laboratory Technology).

Mheshimiwa Spika, katika ngazi ya Shahada mafunzo yanatolewa katika fani za Uhandisi wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji (Bachelor Degree in Water Resources and Irrigation Engineering); Uhandisi wa Usafi wa Mazingira (Bachelor Degree in Sanitation

92​


Engineering); Maendeleo ya Jamii na Uhandisi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (Community Development for Water Supply and Sanitation Engineering); Haidrojiolojia na Uchimbaji (Hydrogeology and Drilling) na Uhandisi wa Haidrolojia (Engineering Hydrology). Aidha, katika ngazi ya Shahada ya Uzamili, mafunzo yanatolewa katika fani za Uhandisi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (Master in Water Supply and Sanitation Engineering) na Rasilimali Maji na Usimamizi wa Huduma (Master in Water Resources and Utility Management). Vilevile, Chuo kinaendesha kozi mbalimbali za muda mfupi katika sekta za maji na umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/24, jumla ya wanafunzi 1,785 wa Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili wamedahiliwa ambapo wanafunzi 1,619 wamedahiliwa Kampasi ya Ubungo na

Kampasi ya Singida. Hadi mwezi Aprili, 2024, Chuo kina jumla ya wanafunzi 3,546 ikilinganishwa na wanafunzi 2,835 katika mwaka 2022/23 ikiwa ni ongezeko la asilimia 25. Aidha, katika mahafali ya mwezi Novemba 2023, jumla ya wanafunzi 682 walihitimu mafunzo yao ambapo wanafunzi 230 ni wa Shahada, 423 ni Stashahada na wanafunzi 29 wa ngazi ya Astashahada. Uhitimu huo umeongezeka kwa asilimia 47 ikilinganishwa na wahitimu 464 wa mwezi Novemba, 2022.

Mheshimiwa Spika
, katika kuhakikisha taaluma bora inatolewa, Chuo kimeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake katika ngazi za Shahada ya kwanza, Uzamili na Uzamivu. Hadi mwezi Aprili, 2024, watumishi

93​


12 wanaendelea na mafunzo ya Shahada ya Uzamivu (PhD); Watumishi watano (5) Shahada ya Uzamili (Masters); watumishi Watatu (3) Shahada ya kwanza na watumishi 25 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi. Vilevile, Chuo kimeendelea kuongeza idadi ya watumishi ambapo katika mwaka 2023/24, Chuo kimeajiri watumishi 17 na hivyo kuwa na jumla ya watumishi 99. Mahitaji ya watumishi kwa sasa ni 180, na Chuo kipo katika hatua za kuajiri watumishi wengine 33 wa kada mbalimbali ambapo usaili umekamilika na watumishi hao watakuwa wamepatikana mwezi Juni, 2024. Aidha, Chuo kinaendelea na ujenzi wa jengo la maktaba na ukarabati mkubwa wa majengo, ikiwa ni pamoja na kuongeza floors (vertical extension) kwa gharama ya Shilingi 5,094,843,455. Hadi mwezi Aprili, 2024 kazi ya ujenzi na ukarabati wa jengo la maktaba imefikia asilimia 75, na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024.




3.4. Masuala Mtambuka

3.4.1.
Rasilimali Watu katika Sekta ya Maji

Mheshimiwa Spika
, mahitaji halisi ya rasilimali watu katika sekta ya maji kwa kada mbalimbali ni watumishi 10,640. Kwa sasa sekta ina watumishi 9,293 hivyo, kuwa na upungufu wa watumishi 1,347. Serikali imeendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya sekta ambapo katika mwaka 2023/24, jumla ya watumishi 420 wameajiriwa ikihusisha kada za Wahandisi, wahaidrolojia, wahaidrojiolojia, Wakemia na Kada Saidizi. Katika kutatua upungufu uliopo, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -

94​


UTUMISHI itaendelea kuajiri wataalam wa kada mbalimbali ili kufikia malengo ya sekta ya kuwahudumia wananchi.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ndani na nje ya nchi. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya watumishi 1,487 walipatiwa mafunzo ambapo watumishi 1,390 walipatiwa mafunzo ya muda mfupi na watumishi 97 walipatiwa mafunzo ya muda mrefu. Aidha, katika kukuza taaluma na weledi kwa wahandisi wa maji, Wizara imeendelea kuwajengea uwezo wahandisi hao kwenye fani zao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wamesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi nchini (Engineers Registration Board - ERB). Vilevile, wahandisi 77 wamesajiliwa na ERB kama wahandisi wataalam na wahandisi 85 wapo kwenye hatua mbalimbali za kusajiliwa.

3.4.2. Sheria


Mheshimiwa Spika
, katika utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019, Wizara imetayarisha Notisi mbili (2) kwa ajili ya kuongeza maeneo ya huduma kwa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira ya Handeni Trunk Main (HTM) kupitia Tangazo la Serikali Na. 774 la tarehe 03/11/2023 na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora kupitia Tangazo la Serikali Na. 771 la tarehe 13/11/2023. Vilevile, Wizara imetayarisha Notisi mbili

(2)
kwa ajili ya kuanzisha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkwajuni kupitia Tangazo la Serikali Na. 173

95​


la tarehe 03/11/2023 na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Kakonko kupitia Tangazo la Serikali Na. 754 la tarehe 20/10/2023.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara imeandaa Notisi za kupandisha madaraja ya Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira 23, ambapo Mamlaka za Maji sita

(6)
za Dar es Salaam, Iringa, Kahama, Moshi, Mwanza na Tanga zimepandishwa kutoka daraja A kwenda daraja AA kupitia Tangazo la Serikali Na. 473 la tarehe 14/7/2023; Mamlaka za Maji nne (4) za Bukoba, Kahama – Shinyanga, Igunga na Nzega zimepandishwa kutoka daraja B kwenda daraja A kupitia Tangazo la Serikali Na. 472 la tarehe 14/7/2023; Mamlaka za Maji tisa (9) za Babati, Bunda, Geita, Mafinga, Makambako, Masasi – Nachingwea, Mpanda, Lindi na Njombe zimepandishwa kutoka daraja C kwenda daraja B kupitia Tangazo Na. 471 la tarehe 14/07/2023; na Mamlaka za Maji nne (4) za Busega, Kyela – Kasumulu, Rombo na Same – Mwanga kupandishwa kutoka daraja lisilo maalum kwenda daraja C kupitia Tangazo la Serikali Na




3.4.3. Jinsia


Mheshimiwa Spika
, uwiano wa jinsia ni muhimu katika vyombo vya maamuzi, usimamizi, uendeshaji na utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Katika kutimiza azma hiyo, Wizara imeendelea kuhamasisha na kuhakikisha uwepo wa uwiano wa jinsia kwenye taasisi zilizopo chini ya Wizara katika ngazi mbalimbali za utekelezaji na utoaji maamuzi. Taasisi zilizopo chini ya Wizara ni Bodi za Maji za Mabonde, Mamlaka za Maji,

96​


Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, Mfuko wa Taifa wa Maji na Chuo cha Maji. Hadi mwezi Aprili 2024, idadi ya watumishi wanawake ni 5,663 sawa na asilimia 60 na wanaume 3,642 sawa na asilimia 40. Vilevile kwa upande wa utawala ngazi ya Wizara na Taasisi, kati ya viongozi wa ngazi mbalimbali waliopo, wanawake ni 201 sawa na asilimia 24 na wanaume ni 622 sawa na asilimia 76. Aidha, Wizara imeweka miongozo ya uundaji wa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii inayozingatia masuala ya jinsia ili kuleta usawa kwenye maamuzi. Vilevile, uteuzi wa kamati na vikosi kazi mbalimbali huzingatia uwiano wa jinsia ili kuhakikisha watumishi wote wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza majukumu na pia, kufanya maamuzi bila kujali jinsia zao.

3.4.4. Mapambano Dhidi ya Rushwa

Mheshimiwa Spika
, Wizara inaendelea na juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutekeleza na kusimamia Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji wa Awamu ya Nne (National Anti-Corruption Strategy and Action Plan - NACSAP IV). Aidha, Wizara inatekeleza Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa mwaka 2003 ambao unalenga kuhakikisha wananchi wanatambua haki na wajibu wao katika kupokea huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara na Taasisi zake. Vilevile, Kamati za Maadili zilizoundwa ngazi ya Wizara na Taasisi zake zimeendelea kusimamia masuala ya maadili mahali pa kazi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo yanayohusu maadili na mapambano dhidi ya rushwa. Kwa ujumla, hali ya mapambano dhidi ya rushwa imeendelea kuimarika na

97​


hivyo, kupunguza viashiria vya rushwa kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu ununuzi wa wakandarasi, wataalam washauri na huduma nyingine zinazotolewa.

3.4.5. UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeendelea kutoa elimu kuhusu afya hususan kujikinga dhidi ya maambukizi ya UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi wake pamoja na Taasisi zake. Hadi mwezi Aprili 2024, jumla ya watumishi 3,283 walipata mafunzo maalum kuhusu kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na yanayoambukiza ikiwa ni pamoja na kufanya vipimo ili kujua afya zao. Aidha, posho kwa ajili ya kununua lishe bora na usafiri kwa watumishi tisa (9) wanaoishi na virusi vya UKIMWI imeendelea kutolewa. Vilevile, Wizara imeendelea kuhamasisha watumishi wake kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

3.4.6. Ujenzi wa Majengo ya Wizara na Taasisi Zake

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi, Serikali inaendelea kujenga majengo ya ofisi kwenye maeneo mbalimbali nchini. Hadi mwezi Aprili 2024, Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu Mtumba, Dodoma kwa gharama ya Shilingi 22,957,343,341.80. Aidha, ujenzi wa jengo la ofisi ya RUWASA Makao Makuu umeanza na ujenzi wa majengo matano (5) ya ofisi za RUWASA Mkoa katika mikoa ya Njombe, Geita, Manyara, Morogoro na Mara unaendelea na upo kwenye hatua

mbalimbali za utekelezaji. Vilevile, ujenzi wa jengo la

98​


Kituo Mahili cha Rasilimali za Maji (Water Resource Centre of Execellence) unaendelea na umefikia asilimia 80. Pia, Wizara imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Rufiji.

3.4.7. Kuimarisha Mifumo ya TEHAMA

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeendelea kuongeza jitihada katika matumizi ya TEHAMA ili kuboresha huduma zinazotolewa na sekta. Katika mwaka 2023/24, Wizara imeendelea kujenga na kuboresha Mifumo ya Pamoja katika Sekta ya Maji kama ifuatavyo:-

Mfumo wa Pamoja wa Ankara za Maji (Unified Maji Billing System)

Mheshimiwa Spika
, Mfumo wa Pamoja wa Ankara za Maji umetengenezwa kwa ajili ya kusimamia ankara za maji zinazotolewa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira pamoja na Bodi za Maji za Mabonde. Pia, mfumo umelenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mauzo ya maji. Hadi sasa, mamlaka za maji 87 sawa na asilimia 96.7 ya mamlaka zote za maji na Bodi za Maji za Mabonde yote tisa (9) zinatumia mfumo huo. Aidha, mfumo huo umeboreshwa kwa kujumuisha Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii ambapo hadi mwezi Aprili 2024, CBWSOs 524 kwenye mikoa 14 ya Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Mwanza, Shinyanga, Katavi, Morogoro, Simiyu, Kagera, Mara, Geita, Singida na Tabora zimeanza kutumia mfumo huo.





99​


Mfumo wa Kusimamia Shughuli za Taasisi (Enterprise Resource Management Suite)

Mheshimiwa Spika
, Mfumo wa Kusimamia Shughuli za Taasisi umeundwa kwa lengo la kuziwezesha Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kutekeleza majukumu yake kwa njia ya kidijitali katika uchakataji wa masuala ya fedha, uhasibu, utumishi, ununuzi, usafiri na likizo. Hadi mwezi Aprili 2024, mamlaka za maji 36 sawa na asilimia 40 ya mamlaka zote zimeanza kutumia mfumo huo.


Mfumo wa Kusimamia Shughuli za Maabara za Maji (Water Laboratory Information System - LIMS)

Mheshimiwa Spika
, Mfumo wa Kusimamia Shughuli za Maabara za Maji umeundwa kwa lengo la kuziwezesha maabara kutekeleza majukumu yake kidijitali. Hadi mwezi Aprili 2024, mfumo huo umefungwa kwa majaribio katika maabara tano (5) za Mwanza, Kigoma, Musoma, Dodoma, na Dar es Salaam. Baada ya majaribio kukamilika, mfumo utafungwa kwenye maabara zote 17 za maji.

Water Resources Operational Decision Support System (ODSS)

Mheshimiwa Spika
, Water Resources Operational Decision Support System (ODSS) ni mfumo ulioundwa kwa ajili ya kuzisaidia Bodi za Maji za Mabonde kufanya maamuzi ya rasilimali za maji kupitia huduma za kihaidrolojia na hali ya hewa. Hadi mwezi Aprili 2024, mfumo huo umefungwa kwa majaribio katika Bodi za Maji za Mabonde matatu (3) ambazo ni Pangani, Rufiji na Wami Ruvu. Majaribio yatakapokamilika, mfumo utafungwa kwenye bodi zote tisa (9) za maji za mabonde.

MAFANIKIO YA SEKTA YA MAJI KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2023/24

Mheshimiwa Spika
, katika kipindi cha utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 chini ya uongozi mahiri wa

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sekta ya maji imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na:-

Kuongezeka kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 77 mwezi Desemba 2022 hadi asilimia 79.6 mwezi Desemba, 2023 na mijini kutoka wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022 hadi asilimia 90 mwezi Desemba, 2023;

Kupatikana kwa chanzo kipya cha fedha za utekelezaji wa miradi ya maji kupitia Hati Fungani ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga imekuwa mamlaka ya kwanza kuzindua uuzaji wa Hati Fungani ya Kijani yenye thamani ya Shilingi bilioni 53.12. Hadi mwezi Februari 2024, Shilingi bilioni 54.72 sawa na asilimia 103 zimekusanywa. Fedha hizo zitatumika kuboresha miundombinu ya usambazaji maji na utunzaji wa mazingira Jijini Tanga pamoja na miji ya Muheza, Pangani na Mkinga;

Kufikiwa kwa malengo ya programu ya PforR kwa muda uliopangwa ikiwa ni pamoja na kuvuka lengo la idadi ya wanufaika kutoka watu milioni 3 hadi milioni 4.07. Hali hiyo imeifanya Benki ya Dunia kuitambua nchi ya Tanzania kuwa ya kwanza kati ya nchi zaidi ya 50 duniani kufanya vizuri katika utekelezaji wa Programu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo. Mafaniko hayo yamesaidia kuongezeka kwa fedha za utekelezaji wa programu kutoka Dola za Marekani milioni 350 hadi Dola za Marekani milioni 654 na kuongeza mikoa inayonufaika kutoka 17 hadi 25 na Halmashauri kutoka 86 hadi 137;

Kukamilika kwa miradi mikubwa na ya kimkakati ikiwemo mradi wa maji Arusha ambao umeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 hadi lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya maji kutoka saa 12 hadi saa 24 kwa siku; na kukamilika kwa mradi wa maji wa Butimba unaonufaisha wakazi wapatao 450,000 katika Jiji la Mwanza;

Kuanzishwa kwa Consultancy Bureau katika Chuo cha Maji inayosaidia kutoa huduma za ushauri elekezi kwenye sekta ya maji na sekta nyinginezo ikiwa ni pamoja na uandaaji na usimamizi wa miradi; kuwajengea uwezo vijana wanaohitimu masomo na kusaidia kuongeza mapato ya taasisi;

Kuanza kwa utekelezaji wa mkakati wa kuwa na

Gridi ya Taifa ya Maji kwa kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito na mabwawa kwa ajili ya kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya uhakika. Kwa mfano; mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao umenufaisha miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga na Shelui pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka kwenye bomba kuu. Pia, mradi wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kupeleka kwenye mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi, ambao upo kwenye hatua za kumpata Mtaalam Mshauri atakayefanya usanifu wa mradi;

Kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati ikiwemo mabwawa ya Kidunda na Farkwa pamoja na Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi – Simiyu;

Kukwamuliwa kwa miradi 157 kati ya miradi 177 ya maji vijijini iliyokuwa na changamoto ya kutokukamilika kwa muda mrefu;

Kuimarika kwa mazingira ya kazi kutokana na kukamilika na kuanza kutumika kwa jengo jipya la ofisi za Wizara lililopo Mtumba pamoja na ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari, pikipiki na kompyuta;

Kuendelea na ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 ambapo utekelezaji upo katika hatua mbalimbali;

Kukamilika kwa ujenzi wa mabwawa 12 ya ukubwa wa kati na madogo ya kuvuna maji ya mvua kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 1.86. Uwepo wa mabwawa hayo unaongeza uhakika wa maji nchini (water security);

Kukamilika kwa uchimbaji wa visima 283 na kuendelea na ujenzi wa mabwawa 12 kwa kutumia seti 25 za mitambo ya kuchimba visima na seti tano

(5) za mitambo ya ujenzi wa mabwawa iliyonunuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
. Pia, mitambo hiyo imesaidia kukabiliana na janga la maafa la Hanang’ mkoani Manyara kwa kuchimba visima nane (8) na kurejesha huduma ya maji kwa wananchi; na kuchimba visima 6 vinavyohudumia wananchi waliohama kutoka Ngorongoro kwenda Msomera; na

Kuimarika kwa usimamizi wa CBWSOs ambapo kwa mara ya kwanza katika mwaka 2022/23, Wizara kupitia RUWASA imeziwezesha CBWSOS 136 kuandaa Vitabu vya Hesabu (Financial Statements) za mwaka 2023/24 na kukaguliwa na CAG. Kati ya hizo, CBWSOs 133 sawa na asilimia 98 zimepata Hati safi. Vilevile, katika kuimarisha udhibiti wa mapato ya fedha za umma, CBWSOs 661 zimejiunga katika Mfumo wa GePG na kuanza kukusanya mapato ya mauzo ya maji kupitia mfumo huo.

CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Mheshimiwa Spika
, katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24, Wizara imekabiliana na changamoto mbalimbali. Miongoni mwa changamoto zilizojitokeza na hatua zinazochukuliwa ni kama ifuatavyo:-

5.1. Uchafuzi, Uharibifu na Uvamizi wa Vyanzo vya Maji

Mheshimiwa Spika
, rasilimali za maji nchini zimeendelea kuathiriwa kutokana na uchafuzi, uharibifu na uvamizi wa vyanzo vya maji. Hali hiyo inatokana na ongezeko la watu linaloenda sambamba na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Pamoja na hayo, uelewa mdogo wa jamii juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji umechangia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa changamoto hizo katika rasilimali za maji.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo, Wizara imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha usimamizi na uendelevu wa rasilimali za maji. Vilevile, Wizara imeendelea kuimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kuviwekea mipaka na kuvitangaza kwenye gazeti la Serikali. Aidha, elimu kuhusu sheria, kanuni na miongozo ya usimamizi wa rasilimali za maji pamoja na umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji imeendelea kutolewa kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

5.2. Mahitaji Makubwa ya Fedha kwa ajili ya Uwekezaji wa Miradi Mikubwa ya Maji

Mheshimiwa Spika
, Wizara inakabiliwa na changamoto ya mahitaji makubwa ya fedha za uwekezaji kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati inayohusisha uvunaji wa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa makubwa na ya ukubwa wa kati pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji kwenye maeneo yenye vyanzo vya maji vya uhakika kama maziwa na mito kwenda kwenye maeneo yenye uhaba wa maji.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imeendelea kutafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia fedha za ndani kutekeleza miradi hiyo mikubwa. Jitihada hizo zimewezesha kupatikana kwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kidunda; kuendelea kwa kazi ya mapitio ya usanifu wa mradi wa bwawa la Farkwa pamoja na kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Mkoa wa Simiyu. Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ambayo ni muhimu katika kuchangia uchumi wa nchi yetu.

5.3. Mabadiliko ya Tabianchi

Mheshimiwa Spika
, mabadiliko ya tabianchi yameendelea kuathiri nchi yetu kwa kusababisha mafuriko, ukame wa muda mrefu na kupata mvua zisizotabirika. Athari za mabadiliko ya tabianchi zimechangia kupungua au kukauka kwa vyanzo vya maji, kupungua kwa uzalishaji wa maji na kusababisha kuongezeka kwa migao ya maji pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya maji kutokana na mafuriko. Katika kipindi cha hivi karibuni nchi yetu imeshuhudia uwepo wa mvua kubwa za El-nino kwenye maeneo mbalimbali. Mvua hizo zimesababisha mafuriko, uharibifu wa miundombinu na vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imeendelea na jitihada za ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua kwa lengo la kuhifadhi maji na kudhibiti mafuriko. Vilevile, Wizara inaendelea kuhakikisha miundombinu ya maji inayojengwa inakuwa himilivu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Aidha, Wizara inaendelea kuandaa maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuibua miradi itakayosaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

5.4. Uendelevu wa Miradi ya Maji Vijijini

Mheshimiwa Spika
, pamoja na jitihada za Serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini, uendelevu wa miradi umeendelea kuwa changamoto katika baadhi ya maeneo ya vijijini. Hali hiyo imetokana na kukauka kwa vyanzo vya maji, wananchi kushindwa kumudu gharama za uendeshaji na matengenezo, makusanyo hafifu ya mauzo ya maji pamoja na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo, RUWASA imeendelea kuviimarisha kwa kuvijengea uwezo Vyombo vya Watoa Huduma ya

Maji Ngazi ya Jamii ili viweze kusimamia na kuendesha skimu za maji kwa ufanisi; kufanya matengenezo makubwa ya miradi; kuboresha usimamizi wa mauzo ya maji na makusanyo kwa kufunga dira za malipo kabla ya matumizi, kuweka mfumo wa pamoja wa ankara (Unified Maji Billing System) na kujiunga kwenye mfumo wa makusanyo ya fedha za umma (GePG); kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia gharama za huduma ya maji pamoja na kujenga miradi inayotumia vyanzo vya maji vya uhakika. Vilevile, katika kupunguza gharama za uendeshaji, Serikali imeendelea kufanya jitihada za kubadili matumizi ya nishati ya dizeli kwenda kwenye matumizi ya umeme jua na umeme wa gridi.

VIPAUMBELE NA MPANGO WA UTEKELEZAJI KWA MWAKA 2024/25

6.1. Vipaumbele vya Sekta

Mheshimiwa Spika
, Wizara imeweka vipaumbele mbalimbali ambavyo vimezingatiwa katika mpango na bajeti ya mwaka 2024/25; lengo ni kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa vijijini na zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini. Utekelezaji wa vipaumbele, utazingatia majukumu ya Wizara yakiwemo kuimarisha usimamizi, uendelezaji, uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na kuimarisha na kusimamia huduma za ubora wa maji. Vipaumbele hivyo ni kama ifuatavyo:-

Kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea na kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa;
Kuongeza kasi ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa ya ukubwa wa kati na mabwawa ya kimkakati;

Kufikisha huduma ya maji kwenye vijiji ambavyo havina huduma;

Kukamilisha uandaaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji (Water Master Plan), Mtandao wa Taifa wa Kusambaza Maji (National Water Grid) na mapitio ya Sera ya Taifa ya Maji;

Kupunguza upotevu wa maji;

Kuongeza kasi ya ufungaji wa dira za malipo kabla ya matumizi ya maji (pre-paid water meters);

Kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye usafi wa mazingira; na

Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji na uendeshaji wa skimu za maji.

6.2. Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2024/25

Mheshimiwa Spika
, mpango na bajeti kwa mwaka 2024/25 umezingatia vipaumbele vya sekta pamoja na masuala ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji; usimamizi wa huduma za ubora wa maji; huduma ya majisafi na usafi wa mazingira vijijini; huduma ya majisafi na usafi wa mazingira mijini; na kujenga uwezo wa Wizara na Taasisi zake. Maelezo ya kina kuhusu mpango wa utekelezaji ni kama ifuatavyo:-
6.2.1. Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji

(a) Usimamizi wa Rasilimali za Maji


Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara itaendelea kuimarisha mfumo wa kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji ikiwemo ukarabati wa vituo 100 vya usimamizi wa rasilimali za maji; kutoa vibali 600 vya matumizi ya maji; kuunda jumuiya 18 za watumia maji na kuunda kamati tisa (9) za vidakio vya maji. Aidha, Wizara itaendelea kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji shirikishi; kuendesha majukwaa ya wadau wa sekta mtambuka wa rasilimali za maji; kufanya tathmini ya rasilimali za maji; na kufanya ukaguzi wa vyanzo vya maji katika Bodi za Maji za Mabonde.

Mheshimiwa Spika, vilevile Wizara imepanga kuimarisha uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kutambua vyanzo vya maji juu ya ardhi na maeneo yenye hifadhi ya maji chini ya ardhi. Kwa upande wa maji chini ardhi, utafiti wa kina utafanyika ili kubaini maeneo yenye maji na kuyafanya kuwa maeneo tengefu. Vilevile, Wizara itaendelea kutambua, kupima, kuweka mipaka na kutangaza vyanzo vya maji kuwa maeneo tengefu katika gazeti la Serikali. Aidha, Wizara imepanga kuimarisha mifumo ya ugawaji maji kwa kutoa vibali vya matumizi pamoja na kuimarisha uhifadhi na udhibiti wa uchafuzi wa vyanzo vya maji.

(b) Uendelezaji wa Rasilimali za Maji


. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2024/25,Wizara imepanga kuendeleza rasilimali za maji kwa kutumia maji chini ya ardhi na juu ya ardhi kwa lengo la kuhakikisha usalama wa maji unakuwepo. Miradi iliyopangwa kutekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa mabwawa ya kimkakati ikiwemo bwawa la Kidunda na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa mradi wa bwawa la Farkwa; kuanza ujenzi wa mabwawa 22 pamoja na kuendelea na ujenzi wa mabwawa 26 ya ukubwa wa kati na madogo; na kufanya usanifu wa mabwawa 45. Aidha, Wizara itakamilisha maandalizi ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji (National Water Master Plan) na Gridi ya Taifa ya Maji (National Water Grid) pamoja na kuendelea kusimamia uchimbaji wa visima virefu vya maji. Kiambatisho Na. 4 kinaonesha mabwawa yaliyopangwa kutekelezwa katika mwaka 2024/25.​

6.2.2. Usimamizi wa Huduma ya Ubora wa Maji

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara itaendelea kufanya tathmini na ufuatiliaji wa ubora wa maji katika vyanzo vya maji 2,200, mifumo ya usambazaji maji 8,245 vijijini na mijini, na mifumo 150 ya majitaka. Vilevile, Wizara imepanga kuweka mifumo ya ukusanyaji na utunzaji wa takwimu na taarifa za ubora wa maji; kuendelea na utekelezaji wa mkakati wa kupunguza madini ya flouride kwenye maji ya kunywa na ya kupikia; na kuwezesha uandaaji na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya usalama wa maji katika mamlaka za maji 40 na CBWSOs 120. Vilevile, Wizara itaendelea kuziboresha maabara za maji kwa kuzipatia vitendea kazi na kuziwezesha kupata na kudumisha hadhi ya ithibati katika viwango vya kimataifa.

6.2.3. Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara imepanga kuendelea kutekeleza jumla ya miradi 1,095 (Kiambatisho Na. 5) ya usambazaji maji vijijini katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo maeneo yanayozunguka vyanzo vya Bwawa la Kidunda na vijiji vilivyopitiwa na mradi wa Same - Mwanga. Aidha, kwa vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji, Serikali imepanga kuchimba visima vitano (5) katika kila jimbo la uchaguzi kwenye maeneo ya vijijini na kwa kuanzia, Wizara itaanza na uchimbaji wa visima 900. Utekelezaji wa miradi hiyo utaongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 79.6 hadi zaidi ya wastani wa asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha uendelevu wa huduma ya maji vijijini, Wizara itaendelea kubadili mitambo inayotumia dizeli na kuweka umeme wa gridi ya taifa au nishati ya jua ili kupunguza gharama za uendeshaji wa skimu za maji; kuimarisha usimamizi wa mauzo ya maji na makusanyo kwenye CBWSOs kwa kufunga dira za malipo kabla ya matumizi (pre-paid water meters); kuweka mfumo wa pamoja wa ankara za maji (Unified Maji Billing System); na kujiunga kwenye mfumo wa makusanyo ya fedha za umma (GePG). Aidha, Wizara itaendelea kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya maji, kuzijengea uwezo CBWSOs 1,382 na kuendelea kuziunganisha CBWSOs ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha.

6.2.4. Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi imepanga kutekeleza jumla ya miradi 247 ya maji mijini. Lengo ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025. Miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka Mto Kiwira kupeleka Jiji la Mbeya; mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma kupeleka Mtwara; mradi wa kutoa maji Mto Momba kwenda Tunduma; kutoa maji kutoka tanki la Bisarye mradi wa kutoa maji Mto Rufiji kwenda mikoa ya Dar es Salaam na Lindi; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji kupitia mradi wa miji 28; mradi wa maji na usafi wa mazingira Vwawa – Tunduma; utekelezaji wa miradi ya uondoshaji majitaka katika miji mikuu ya mikoa, miji mikuu ya wilaya na miji midogo; kuendelea kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma, uendeshaji na matengenezo ya skimu za maji; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni hatua za awali za maandalizi ya miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ikiwemo mradi wa kutoa maji Mto Rufiji kupeleka katika mikoa ya Dar es Salaam na Lindi. Miradi ya maji na usafi wa mazingira mijini itakayotekelezwa katika mwaka 2024/25 imeoneshwa kwenye Kiambatisho Na. 6.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Jiji la Dodoma, Wizara imepanga kuboresha huduma ya maji kwa kutekeleza mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Mpango wa muda mfupi ni kuendelea

na utekelezaji wa miradi ya majisafi maeneo ya Jiji la Dodoma na Chamwino, DTC Nala, Nala ITRACOM, Njedengwa National Housing hadi UDOM, Zuzu-Nala na mradi wa maji Nzuguni Awamu ya Pili. Vilevile, Wizara itajenga mtandao wa majisafi na kuchimba visima katika Mji wa Serikali ikiwa ni pamoja na maeneo ya pembezoni mwa Jiji. Katika mpango wa muda wa kati, Wizara itaanza ujenzi wa mradi wa bwawa la Farkwa; na mpango wa muda mrefu ni kutekeleza mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Jiji la Dodoma kupitia Singida.

6.2.5. Kupunguza Upotevu wa Maji

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara imepanga kufanya ukarabati wa miradi ya maji na kudhibiti wizi wa maji ili kupunguza kiwango cha maji yanayopotea ambacho hadi sasa kimefikia wastani wa asilimia 35.3 ya maji yanayozalishwa. Kiwango hicho ni kikubwa kikilinganishwa na kiwango kinachokubalika kimataifa cha asilimia 20. Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na ukarabati wa miundombinu ya maji iliyochakaa; kufunga dira za maji ya jumla (bulk meters); kufunga dira za maji kwa wateja wote; kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya maji; na kushirikisha viongozi wa mikoa, Jeshi la Polisi na wananchi katika kuwabaini na kuwachulia hatua stahiki wanaojihusisha na wizi wa maji na uharibifu wa miundombinu ya maji.

6.2.6. Kuimarisha Utoaji wa Huduma ya Maji


214. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea

katika mwaka 2024/25, kuimarisha utoaji wa

huduma bora ya maji kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya wananchi, kudhibiti bei za maji, kuondoa migao ya maji, kuunganisha huduma kwa wakati na kupunguza malalamiko yatokanayo na huduma ya maji. Katika kuhakikisha azma hiyo inatimia, Wizara itasimamia ufungaji wa dira za maji za malipo kabla (prepaid metres); kutumia na kuendelea kuboresha mfumo wa pamoja wa ankara za maji (Unified Maji Billing System); na kuhakikisha wateja wanaunganishiwa huduma ya maji kwa wakati.

6.2.7. Kujenga Uwezo wa Kitaasisi

Mheshimiwa Spika
, katika mwaka 2024/25, Wizara itakamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002; kuendelea kujenga uwezo wa kitaasisi wa sekta ya maji ikiwa ni pamoja na watumishi na kukiwezesha Chuo cha Maji kuendelea kutoa wataalam kulingana na mahitaji. Aidha, Wizara itaendelea kuujengea uwezo Mfuko wa Taifa wa Maji ili uweze kupata ithibati kwa ajili ya kupata fedha za Mifuko ya Mabadiliko ya Tabianchi. Vilevile, Wizara itaendelea kuimarisha mifumo ya TEHAMA; na ufuatiliaji na tathmini ili kuongeza ufanisi.

SHUKRANI

Mheshimiwa Spika
, kipekee napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi pamoja na wadau mbalimbali kwa ushrikiano wao katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu kwa mwaka 2023/24. Maandalizi ya bajeti hii ya wizara yamezingatia michango, maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau katika kuweka vipaumbele vinavyolenga kuboresha utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira. Ushirikishwaji wa wadau na makundi mbalimbali ya jamii unadhihirisha umuhimu wao katika kuhakikisha tunakuwa na bajeti inayokidhi matarajio ya wananchi na maendeleo ya Sekta ya Maji.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati ya moyo wangu, naomba nichukue nafasi hii kukushukuru wewe Spika na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa mnayoifanya katika kuhakikisha sekta yetu ya maji inafikia azma ya Serikali ya kuwapatia wananchi wote maji safi, salama na ya kutosheleza. Ninaomba Mwenyezi Mungu awabariki sana.

Mheshimiwa Spika, napenda pia, kutoa shukrani zangu kwa Nchi Rafiki, Washirika wa Maendeleo, Mashirika ya Misaada ya Kimataifa, Sekta Binafsi, Taasisi Zisizo za Kiserikali, Mashirika ya Kidini na Wadau Wengine kwa ushirikiano wanaoutoa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, kipekee ninapenda kuzishukuru nchi rafiki tunazoshirikiana nazo zikiwemo
Uingereza, Ujerumani, India, Marekani, Korea Kusini, Uholanzi, Hispania, Misri, Ufaransa, Kuwait, Ubelgiji, Italia na Saudi Arabia. Vilevile, ninayashukuru Mashirika ya Maendeleo na Taasisi za Kimataifa kwa misaada ya kitaalam na kifedha katika kuiwezesha Sekta ya Maji kutekeleza majukumu yake. Mashirika na Taasisi hizo ni pamoja na Benki ya Dunia (World Bank - WB), Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW), Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB), Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (BADEA), Mfuko wa Maendeleo wa Nchi zinazozalisha Mafuta (OPEC Fund for International Development-OFID), Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund), Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (SFD), Foreign Commonwealth and Development Office (FCDO), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GiZ), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Global Environment Facility (GEF), Green Climate Fund (GCF), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (BTC), Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Mheshimiwa Spika, viongozi na waumini wa dini mbalimbali wamekuwa na mchango muhimu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu. Kwa namna ya pekee ninawashukuru kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuliombea Taifa na ninawaomba waendelee kuliombea Taifa letu na viongozi wetu. Vilevile, ninayashukuru Mashirika na Taasisi za Kidini ambazo zimeendelea kusaidia Sekta ya Maji katika kufikia malengo yake. Mashirika na Taasisi hizo ni pamoja
na Catholic Agency for Overseas Aid and Development (CARITAS), Adventist Development Relief Agency (ADRA), Norwegian Church Aid, Livingwater International, World Islamic League, Shirika la Ahmadiya Muslim Jamaat Tanzania, Islamic Foundation, Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa Katoliki Tanzania na Kanisa la Anglikana Tanzania.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuzishukuru Taasisi zisizo za Kiserikali ambazo zimekuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya sekta ya maji nchini. Taasisi hizo ni pamoja na Association of Tanzanian Water Suppliers (ATAWAS), OIKOS,

Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET),
Wahamasishaji wa Maji, Maendeleo na Afya (WAMMA), World Vision; Worldwide Fund for Nature (WWF), Netherlands Volunteers Services (SNV), Plan International, Concern Worldwide, WaterAid Tanzania, Water Mission (T), Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Uasili na Maliasili (IUCN), Shahidi wa Maji na Mashirika mengine mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee kabisa naomba nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) ambaye kwa kipindi kifupi tangu kuteuliwa kwake, tumeshirikiana naye katika kuendeleza kazi kubwa ya kuhakikisha Sekta ya Maji inasonga mbele na wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma ya maji. Vilevile, naomba kuwapongeza Mhandisi Mwajuma Waziri kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji na Bibi Agnes Kisaka Meena kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Imani na dhamana waliyopewa na Mheshimiwa Rais ni kubwa na ninaamini katika utendaji wao tutafanya mageuzi makubwa katika kuongeza kasi ya maendeleo katika Sekta ya Maji. Aidha, kipekee napenda kuwashukuru Viongozi wa Taasisi, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo, na Watumishi wote wa Wizara ya Maji na Taasisi zake kwa ushirikiano wanaonipatia pamoja na kujituma kwao kwa kusimamia utekelezaji wa majukumu yao kwenye Sekta ya Maji kwa kiwango cha hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, naomba nieleze kuwa ninayo furaha kubwa kuendelea kuishukuru familia yangu na wananchi wa Jimbo la Pangani kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu. Napenda kuwaahidi kuwa nitatumia weledi, maarifa na uwezo wangu wote niliojaliwa na Mwenyezi Mungu katika kulijenga jimbo letu na Taifa kwa ujumla.

MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2024/25

Mheshimiwa Spika
, baada ya maelezo hayo, ninaomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 627,778,338,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2024/25, ambapo Shilingi 69,662,959,000 ni fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi 558,115,379,000 ni fedha za maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kati ya fedha za matumizi ya kawaida, Shilingi 17,542,812,000 ni kwa ajili ya kugharamia matumizi mengineyo (OC) na Shilingi
52,120,147,000 ni kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi (PE) wa Wizara, RUWASA, Mfuko wa Taifa wa Maji na Chuo cha Maji. Kwa upande wa fedha za maendeleo, Shilingi 340,463,656,000 sawa na asilimia 61 ni fedha za ndani na Shilingi 217,651,723,000 sawa na asilimia 39 ni fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, ninaomba tena kutoa shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara www.maji.go.tz

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.
 

Attachments

  • Hotuba_ya_Bajeti_ya_Wizara_ya_Maji_kwa_Mwaka_wa_Fedha_2024_2025.pdf
    1.9 MB · Views: 3
Tunataka gridi za kikanda, mambo ya gridi ya taifa yawe exceptional cases, kwa hiyo gridi ikisumbua Kibaha, mpaka Rorya hakuna maji?

Hiyo ni kuweka mayai yote katika kapu moja, likidondoka yanavunjika yote
 
Makadirio ya Bajeti
Wizara Ya Maji 2023/2024, ni kiasi Gani cha fedha kilitolewa na serikali?

Kwani kiasi kilichotengwa na bunge sicho kilichotolewa. Zinginge zilikwenda wapi???

Ninaona Kila mwaka bajeti ni mabilion ila fedha hazitolewi na zikitolewa hazitolewi kwa wakati.
Tatizo ni nini!!!!!😏
 
Back
Top Bottom