Wizara ya Kilimo ihamasishe mikoa ya K'njaro, Morogoro na Mbeya kulima ndizi aina ya Fhia

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kuna aina mpya ya ndizi inayoitwa FHIA Ambayo inazaa sana na inahimili maradhi imeanza kulimwa mkoa wa Kagera.Ndizi hii mpya inaweza kupunguza umasikini na kuwa na uhakika wa chakula.Nashauri mikoa ya Kilimanjaro,Morogoro ,Mbeya na mingineyo inayopenda ilime hiyo ndizi.

Video yake hiyo


HAPA KAZI TU

yehodaya123@gmail.com
 
Mkuu shukrani kwa kuliona hili japo napingana na mawazo yako. Mimi ni mwenyeji wa Kagera tena eneo ambalo hizi ndizi zinalimwa sana (Kiziba).

Tambua kuwa hizi ndizi zimeanza kulimwa baada ya ndizi za kawaida (matoke) kukumbwa na ugonjwa wa mnyauko, hapo kabla hizi ndizi hakuna aliyekuwa analima.

Ndizi hizi sio nzuri (Utamu) ila kutokana na shida inabidi tule hizo ndizi. Soko lake pia zuri kama ndizi aina ya matoke.Sana sana wakazi wakulima wanalima kwa ajili ya kupata mlo na kutengeneza pombe.

Labda mikoa hiyo walime kama kilimo cha kulisha familia zao lakini sio kwa zao la biashara.
 
Hayo sio yale ma-genetically modified kweli?


dudus
dunia ya sasa inabidi kwenda na wakati uliopo.

siku hizi mazao ambayo asili (organic) ni gharama na uchukua muda mrefu kukua.

hayo ma -genetically modified yanaweza kupata matumizi mbadala.
 
dudus
dunia ya sasa inabidi kwenda na wakati uliopo.

siku hizi mazao ambayo asili (organic) ni gharama na uchukua muda mrefu kukua.

hayo ma -genetically modified yanaweza kupata matumizi mbadala.

FHIA 17 NI NZURI HATA KWA KUPIKA NA BIASHARA. MBONA NDO ZINAUZWA SANA MIKOANI HASA DAR NA USUKUMANI
 
Back
Top Bottom