technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 11,975
- 48,843
Sasa hivi laki sita unachokataa ni nn ?acha uongo cc mbona tuliluwa tunalipia laki mbili kwa mwaka 2015
Na lazima akili irudi tu, ngoja tuendelee kuisoma namba ya kirumi.
kweli?Waziri alisema kuna ziada ya walimu wa sekondari 7000
Ongea logic ww unafikria mkulima anaweza kuafford ?sio kila kitu tumuonee magufuli, hii ada ilipandishwa toka enz za kikwete ili vyuo hiv viweze kujiendesha badla ya kutegemea ruzku. hakuna chuo cha binafsi ada laki sita. nitajie hicho chuo.??
Ada ya vyuo vya Serikali kwa wanaochaguliwa moja kwa moja ndio ada yake, labda ulisoma privateHuo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?
Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Wajinga ndio waliwao ulikuwa unaliwa.Huo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?
Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Ongeza umakini ili na wanafunzi wako waige kuwa makini. Laiti ungesoma vizuri bandiko la muhusika haya maswali usingeyaulizaHuo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?
Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Wizara ya elimu sayansi na tekonolojia imepandisha karo na michango kwa vyuo vya ualimu vya serikali kuwa kama vyuo binafsi miaka ya nyuma vyuo hivi wanafunzi walikuwa wakichaguliwa na vyuo vya serikali vya ualimu walikuwa wanalipia elfu sabini kwa mwaka (70,000/=) lakini sasa hivi serikali imepandisha karo hii ghafla kufikia laki sita (600,000) kwa mwaka hii ni karo tu jumla na michango inafika million Moja na sehemu .
Hii inapelekea watoto wa masikini washindwe kujilipia hivi vyuo lilikuwa kimbilio la watoto wa wakulima watanzania ambao hawawezi kulipa vyuo binafsi sasa hivi vyuo vya ualimu vya serikali na binafsi vinalingana hivyo watoto wa masikini wanachaguliwa vyuo na kushindwa kuripoti vyuoni kutokana na gharama hizi kuwa kubwa sana .
Pia naiomba serikali iwape ufadhili wanafunzi watakaochaguliwa kusomea ualimu wa sayansi ngazi ya stashahada mfano chuo cha kleruu, monduli nk kwa sekondari kwenye vyuo vya serikali mwaka huu wasilipie karo wawe wanasainisha mikataba baada kumaliza masomo yao wafanye kazi serikalini ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa sayansi pia wanafunzi hawa wanashindwa kufika chuoni kufatana na gharama kubwa za vyuo vya serikali hivyo kupelekea kukoswa walimu wa sayansi .
Mwisho niwaombe serikali ipunguze karo na gharama za vyuo vya ualimu ili kuwasaidia watoto wa wakulima kupata fursa ya kusoma kama ilivyokuwa zamani .