Wizara ya elimu yapandisha ada ya vyuo vya ualimu serikali kuwa kama vyuo binafsi

Daaaah huyu jamaa anabana kila sehemu ....

Sijui wananchi watapumulia wapi.........

Kweli Kikwete alikuwa mwanaume kama ni hivi.......
 
mkiambiwa CCM ni ile ile na wana CCM wenyewe watu mnakataa sasa mnataka tuwasaidiaje...ila uzur tumepata rais anayesikiliza wanyonge wakat ukifika atawasikilza tu
 
2020 akili itakua imekaa sawa, mahakimu wenye dip na cert. nje watafuata walimu, manesi nk
 
Sasa kama serikali haina vyanzo vya mapato unategemea ifanye nn? Imeongeza karo ili ipate mapato
 
Huo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?

Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Ada ya vyuo vya Serikali kwa wanaochaguliwa moja kwa moja ndio ada yake, labda ulisoma private
 
Huo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?

Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Wajinga ndio waliwao ulikuwa unaliwa.
 
Huo ualimu ni wa levo gani ulikua ukilipiwa elfu 70? Pia umesema zamani ni zamani mwaka gani?

Nimesoma chuo cha serikali na ada ya ualimu ukitoa michango mingine ilikua laki tisa (9) kwa levo ya shahada.
Ongeza umakini ili na wanafunzi wako waige kuwa makini. Laiti ungesoma vizuri bandiko la muhusika haya maswali usingeyauliza
 
Wizara ya elimu sayansi na tekonolojia imepandisha karo na michango kwa vyuo vya ualimu vya serikali kuwa kama vyuo binafsi miaka ya nyuma vyuo hivi wanafunzi walikuwa wakichaguliwa na vyuo vya serikali vya ualimu walikuwa wanalipia elfu sabini kwa mwaka (70,000/=) lakini sasa hivi serikali imepandisha karo hii ghafla kufikia laki sita (600,000) kwa mwaka hii ni karo tu jumla na michango inafika million Moja na sehemu .

Hii inapelekea watoto wa masikini washindwe kujilipia hivi vyuo lilikuwa kimbilio la watoto wa wakulima watanzania ambao hawawezi kulipa vyuo binafsi sasa hivi vyuo vya ualimu vya serikali na binafsi vinalingana hivyo watoto wa masikini wanachaguliwa vyuo na kushindwa kuripoti vyuoni kutokana na gharama hizi kuwa kubwa sana .


Pia naiomba serikali iwape ufadhili wanafunzi watakaochaguliwa kusomea ualimu wa sayansi ngazi ya stashahada mfano chuo cha kleruu, monduli nk kwa sekondari kwenye vyuo vya serikali mwaka huu wasilipie karo wawe wanasainisha mikataba baada kumaliza masomo yao wafanye kazi serikalini ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa sayansi pia wanafunzi hawa wanashindwa kufika chuoni kufatana na gharama kubwa za vyuo vya serikali hivyo kupelekea kukoswa walimu wa sayansi .

Mwisho niwaombe serikali ipunguze karo na gharama za vyuo vya ualimu ili kuwasaidia watoto wa wakulima kupata fursa ya kusoma kama ilivyokuwa zamani .




Naomba maghufuli aliposhika asiachie
 
hpo sasa kuwapata walimu ni issue hsa sayansi kwani wtoto wengi ni wa kutoka familia maskini sana hyo 600000 shughuli.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom