LTN USU WA MADOSO
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 1,193
- 859
Wizara ya elimu sayansi na tekonolojia imepandisha karo na michango kwa vyuo vya ualimu vya serikali kuwa kama vyuo binafsi miaka ya nyuma vyuo hivi wanafunzi walikuwa wakichaguliwa na vyuo vya serikali vya ualimu walikuwa wanalipia elfu sabini kwa mwaka (70,000/=) lakini sasa hivi serikali imepandisha karo hii ghafla kufikia laki sita (600,000) kwa mwaka hii ni karo tu jumla na michango inafika million Moja na sehemu .
Hii inapelekea watoto wa masikini washindwe kujilipia hivi vyuo lilikuwa kimbilio la watoto wa wakulima watanzania ambao hawawezi kulipa vyuo binafsi sasa hivi vyuo vya ualimu vya serikali na binafsi vinalingana hivyo watoto wa masikini wanachaguliwa vyuo na kushindwa kuripoti vyuoni kutokana na gharama hizi kuwa kubwa sana .
Pia naiomba serikali iwape ufadhili wanafunzi watakaochaguliwa kusomea ualimu wa sayansi ngazi ya stashahada mfano chuo cha kleruu, monduli nk kwa sekondari kwenye vyuo vya serikali mwaka huu wasilipie karo wawe wanasainisha mikataba baada kumaliza masomo yao wafanye kazi serikalini ili kuziba pengo la uhaba wa walimu wa sayansi pia wanafunzi hawa wanashindwa kufika chuoni kufatana na gharama kubwa za vyuo vya serikali hivyo kupelekea kukoswa walimu wa sayansi .
Mwisho niwaombe serikali ipunguze karo na gharama za vyuo vya ualimu ili kuwasaidia watoto wa wakulima kupata fursa ya kusoma kama ilivyokuwa zamani .