Wizara ya Elimu itoe ufafanuzi juu ya matumizi ya mtaala mpya wa Elimu ya msingi utakaoanza kutumika mwakani 2024

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,150
7,725
Kwanza nampongeza waziri wa Elimu na Timu yake kwa kuchakata na hatimaye kutuletea mtaala mpya wa elimu ya msingi ambao unatarajiwa kuanza kutumika mwakani 2024.

Hakika mtaala una mambo mengi mazuri wenye faida kwa kizazi chetu.

Kwa sasa kichotakiwa ni kutoa maelekezo na ufafanuzi jinsi utakavyoanza kutumika mtaala huo mwakani, tusisubirie kutokee mkanganyiko ndipo tuanze kutoa ufafanuzi, muda ni sasa.

Mfano; suala la watoto waliopo darasa la sita mwaka huu, je, mwakani wataendelea na darasa la saba au watajiunga form one?

Mambo hayo pamoja na mengine mengi yanapaswa yatolewe ufafanuzi muda huu sio mwakani.
 
Mtaala MPYA utaanza mwaka 2024 ila utaanza kwa darasa la awali, la kwanza,la pili na la tatu, mfano Hawa ambao wako darasa la tatu mwaka huu wataendelea darasa la nne kwa kutumia mtaala wa zamani Hadi wahitimu darasa la saba na ndio watakukuwa wa mwisho kumalizia mtaala wa zamani na hao wanafunzi walioko darasa la pili mwaka huu ndio watakuwa wahitimu wa kwanza wa mtaala MPYA mwaka 2027 wataishia darasa la 6.

Na sekondari mtaala MPYA utaanza na wanaoingia kidato Cha kwanza 2024.
 
Back
Top Bottom