Wizara ya Elimu imetoa madaftari elekezi?

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
18,143
20,712
Hii imetokea Tanga. Watoto wa shule wamerudishwa na wengine kuchapwa eti kwanini wamenunua madaftari ambayo siyo.

Sasa nataka kujuwa kama wizara imetowa maelekezo au tenda kwa mtu maalum wa kutengeneza madaftari maalum? Au hii ipo Tanga tu Masiwani S/M?
 
Last edited by a moderator:
Hii imetokea Tanga. Watoto wa shule wamerudishwa na wengine kuchapwa eti kwa nini wamenunua madaftari ambayo siyo. Sasa nataka kujuwa kama wizara imetowa maelekezo au tenda kwa mtu maalum wa kutengeneza madaftari maalum? Au hii ipo Tanga tu Masiwani S/M?
Mrija huo wa ulaji... Mwanafunzi hana kosa kwasababu kanunuliwa na mzazi
 
Tatizo ni ubongo wa watu wengine haufanyi kazi vizuri hao waalimu wamekariri kufundisha tu lakini hawajiongezi kwa mengine.
Unamchapa mwanafunzi au kumfukuzi kwani kaenda shule na MBUZI au madaftari
 
Hii imetokea Tanga. Watoto wa shule wamerudishwa na wengine kuchapwa eti kwa nini wamenunua madaftari ambayo siyo. Sasa nataka kujuwa kama wizara imetowa maelekezo au tenda kwa mtu maalum wa kutengeneza madaftari maalum? Au hii ipo Tanga tu Masiwani S/M?

Mkuu hatukuwahi kufanya hilo. Si tunabana matumizi! Elimu ni bure lakini wazazi pia mchagie gharama!! hah hah Kuwadanganya waTZ rahisi mbona!
 
Mkuu hatukuwahi kufanya hilo. Si tunabana matumizi! Elimu ni bure lakini wazazi pia mchagie gharama!! hah hah Kuwadanganya waTZ rahisi mbona!
Elimu bure iko wapi? Kuna shule za kata huko nyuma ziliamua kuanzisha boarding (hostel) kwa makubaliano ya wazazi ili watoto wanaokaa mbali na shule waweze kusoma kwa nafasi, hao serikali haijatoa pesa ya chakula; bado wazazi/walezi tunaendelea kupigika.

Hawa hawa watoto wa shule za kata wanaolala shuleni wazazi tulikubaliana kila mtoto achange TZS 5,000 kwa term kwa ajili ya generator je hizo serikali itapeleka? Shule za kata zinatambuliwa kama ni shule za kutwa sidhani kama serikali inajua kuna "prepo" kwenye shule za kata ili walipie umeme
 
Back
Top Bottom