MHE. NORAH WAZIRI MZERU, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Anauliza Swali Bunge kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,296
1,100

MHE. NORAH WAZIRI MZERU, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Anauliza Swali Bunge kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

"Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha Wanafunzi wasichana wanaokatiza masomo kwasababu ya kupata ujauzito wanarejea Shuleni. Hatua hizo ni pamoja na kutoa Waraka wa Elimu namba mbili wa mwaka 2021 kuhusu kuwarejesha Wanafunzi waliokatiza masomo kwasababu mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito" - Mhe. Juma Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Waraka umetoa fursa kwa mwanafunzi wa kike aliyepata ujauzito kurudi Shule Kukamilisha mzunguko wake wa Kielimu katika Shule yake ya awali au Shule yoyote ambayo mzazi au mlezi na mwanafunzi watakubaliana na Mamlaka husika kwa lengo la kuhakikisha mwanafunzi anakamilisha mzunguko wake wa kielimu wa kupata Elimu"

"Serikali imeweka mfumo usio rasmi ambao unaruhusu mtu yeyote kujiendeleza kielimu ili Kukamilisha malengo yake hususani katika Elimu ya watu wazima. Vyuo vya maendeleo ya wananchi ambapo hata mwanafunzi aliyekatiza masomo anaruhusiwa kujiunga ili Kukamilisha mzunguko wake wa kupata Elimu"

"Nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa huruma, kufanya maamuzi magumu na kuwarejesha wasichana waliopata mimba na kukatiza masomo yao" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Je, mikakati gani Serikali imetekeleza ili kuhakikisha wahanga wa ubakaji wanapata sauti na mifumo ya Sheria na haki inaboreshwa ili kuzuia wasichana wasikatishe masomo? - Mhe. Norah Waziri Mzeru

"Zipo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuwalinda watoto wetu wa kike dhidi ya ubakaji na ukatili kwa ujumla. Jitihada hizo ni pamoja na Kuimarisha ulinzi na usalama wa Wanafunzi wawapo Shuleni kwa ujenzi wa mabweni na hosteli. Kuanzisha madawati ya ushauri nasaha kwenye maeneo ya Shule na mpaka Vyuo kwa ujumla"

"Serikali imeendelea na utoaji Elimu kwa jamii dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto. Vitendo vya ubakaji ni kosa la jinai na adhabu yake hutolewa chini ya Sheria ya adhabu kifungu (16) ya Sheria ya Bunge. Sheria inatoa adhabu kali ikiwemo kifungo cha miaka 30 au zaidi ya hapo" - Mhe. Juma Kipanga, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
 
Hivi huyu mbunge baba yake ya nae alikuwa mbunge miaka ya 2000 mzeru??
 
Back
Top Bottom