Wizara ya Elimu fuatilieni hili Elimu inakufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Elimu fuatilieni hili Elimu inakufa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wanafunzi wagoma kufanya mtihani

  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha iliyo mkoani Pwani wamegoma kwa siku nne kuendelea na mitahani ya ‘Mock’ kwa madai kuwa maswali mengi yaliyoulizwa yamerudiwa kwani yaliwahi kutoka katika mitihani ya mwaka 2008 na 2009.

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana wameilalamikia bodi ya utungaji wa mitihani Kanda ya Mashariki na Pwani (EZEB) na kusema badala ya kutunga mitihani mipya wamenakili iliyopita wakati wao wamechanga fedha kuiwezesha bodi hiyo kutunga mitihani ya kuwapima vyema.

  Walisema hawawezi kuendelea na mitihani hiyo kwani haiwawezeshi kujiandaa vizuri na mtihani wao wa mwisho badala yake inawadidimiza kitaaluma kwani tayari mitihani hiyo walishaifanyia mazoezi.

  Walitolea mfano wa marudio ya maswali katika somo la Civics wakisema kuwa wameulizwa swali la mwenyekiti wa AU ambalo katika majibu yake ya kuchagua hakuna jibu hata moja kwani waliowekwa wote wameshamaliza muda wao kwa sasa.

  “Hatuwezi kuendelea kufanya mtihani kwani haitusaidii chochote katika maandalizi ya mtihani wetu wa mwisho, wakitaka watunge tena tufanye tujipime vizuri lakini hiki walichokifanya bodi ya mtihani hakitufurahishi ndio maana tumeamua kugoma kuendelea na mtihani huu,” alisema mmoja wa wanafunzi kwa niaba ya wengine.

  Aidha wanafunzi hao walidai kuwa wamekuwa wakichangia sh 12,000 kwa ajili ya mtihani huo jambo ambalo limewashangaza kwa bodi hiyo kurudia mitihani wakati ingeweza kutumia muda kwa ajili ya kutunga maswali tofauti na mitihani iliyopita.

  Mkuu wa shule hiyo Sekundi Kayenga alithibitisha kutokea kwa mgomo huo na kukiri kuwa baadhi ya mitihani ukiwemo wa somo la Baiolojia ilinakiliwa kutoka katika mitihani iliyopita.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Good steps...hawa ndio vicha vilivyobakia!!sasa mitihani kama hii mtu ukikutana nayo,unapiga div 1 ya ajabu,..siku ya pepa ya mwisho..dah....zero ya ajabu!!
   
 3. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  napita tu!
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  elimu inajifia yenyewe kila mtu kawa mchakachuaji!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,519
  Trophy Points: 280
  wapo maofisini tu wanacopy na ku paste, hawa waalimu nao ni wa kata?
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  na wamewachangisha pesa hawa watoto elfu kumi na tatu kila mmoja
   
 7. data

  data JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,747
  Likes Received: 6,524
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi ndio wapuuzi.. wangefanya afu tuone kama wote wangepata one..... wapuuziiiii
   
Loading...