Wizara ya Afya yakanusha taarifa ya watu saba kupata upofu kutokana na ugonjwa wa red eyes

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Screenshot 2024-02-19 at 16.07.43.png

Pia Soma:
- Dar: Watu 7 wapofuka Macho kwa kujitibu Ugonjwa wa 'Red Eyes' kienyeji
 
Attachments

  • KANUSHO LA TAARIFA YA WATU SABA KUPOFUKA KWASABABU YA RED EYES.pdf
    148.7 KB · Views: 1
Baada ya kusambaa kwa taarifa za watu 7 kupata upofu kutokana na ugonjwa wa macho mekundu (Red Eyes), Wizara ya Afya nchini, imekanusha taarifa hiyo, huku ikisisitiza kuwa taarifa hiyo haijatolewa na Wizara hiyo kama ambavyo imeripotiwa.

Kupitia Taarifa ya kanusho iliyolewa na Wizara hiyo leo Februari 19, 2024, imebainisha kuwa mnamo Februari 6, 2024, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya, Prof. Paschal Ruggajo, alisema kuwa Wizara hiyo imepokea taarifa za watu ambao wamefika kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya wakiwa na vidonda kwenye kioo cha mbele cha jicho, baada ya kutumia tiba zisizo rasmi kutibu Red Eyes, lakini hakutaja idadi ya watu waliopata upofu kutokana na ugonjwa huo.

Kutokana na sintofahamu hiyo, Wizara hiyo imevitaka vyombo vya Habari kuzingatia weledi wa taaluma ya habari kwa kutoa habari za ukweli kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa kwani kusambaa kwa taarifa hiyo inaweza kuleta taharuki zaidi ndani ya jamii juu ya ugonjwa wa macho mekundu (Red Eyes).

Chanzo: ITV
 
Baada ya kusambaa kwa taarifa za watu 7 kupata upofu kutokana na ugonjwa wa macho mekundu (Red Eyes), Wizara ya Afya nchini, imekanusha taarifa hiyo, huku ikisisitiza kuwa taarifa hiyo haijatolewa na Wizara hiyo kama ambavyo imeripotiwa.

Chanzo: ITV
Kwahio wamekanusha kwamba hawajatoa taarifa sio kwamba watu hawajapofuko (yaani suala la kupofuka hawajui) na je hizo tina mbadala sinapofusha ? Na kama zinapofusha kwanini watu wasipofuke ?

Hili short hili kanusho uliloleta bado lina utata....
 
inamaana hiyo taarifa ya upofu wa hao watu bado haina ithibati (mpaka muda huu ni yauzushi)
 
inamaana hiyo taarifa ya upofu wa hao watu bado haina ithibati (mpaka muda huu ni yauzushi)
Kwanini wao wasifuatilie ukweli wake na wakati wanafuatilia waseme kwamba Hatujatoa hii Habari wala Hatuna Taarifa (Tunafuatilia) Sababu wakisema hakuna upofu wakati watu wanaendelea na hizo Tiba mbadala ambazo zinaweza kuleta Upofu huoni bado kuna sintofahamu ?
 
Back
Top Bottom