Tangu nipone red eyes naona Picha mbilimbili (double images)

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
877
2,427
Habari wakuu!

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Ilikuwa jumanne ilopita tarehe 12 mwez huu wa 3 niliamka jicho la kushoto linachoma choma na kutoa machozi na tongotongo kidogo nikajicheki kwenye kioo nikaona limekuwa jekundu basi moja kwa moja nikajua hii red eyes (conjunctivitis).

Nikaanza kutumia maji ya baridi kujisafisha mara kwa mara machoni.

Niliapa sitatumia dawa yoyote kwasababu niliona Millard kapost kuna baadhi ya watu wamekuwa vipofu jumla kwasababu ya kutumia madawa kutibu hii red eyes.

Kesho yake nikaamka jicho la kulia nalo limepata maambukizi basi vita ikazidi kuwa nzito kwa waliowahi kupatwa na huu ugonjwa wanaelewa karaha zake.

Nikatumia maji ya baridi kusafisha macho kwa ndani ya siku mbili macho yakapona.

Red eyes imepona ila shida ilobaki ni kuona taswira mbilimbili ya kitu kimoja yani kama nasoma namba 1 naona 11 kama 2 naona 22 kama 3 naona 33.

Hiyo shida nimeanza kuipata baada ya kupona red eyes naombeni msaada wa kiafya hapa wataalam naboeka.
 
Back
Top Bottom