wizara ya afya tuwekane sawa katika hili

wizara ya afya tuwekane sawa katika hili

mng'oa kucha

Senior Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
150
Reaction score
179
Ndugu, jamaa au rafiki ameondoka nyumbani kwenda kujitaftia ridhiki mbahati mbaya amepata la kumpata labda ajali, wakatokea wasamaria wema wakampeleka hosipitali, nyumbani haonekani ametafutwa kote mpaka vituo vya polisi kumbe alipopelekwa hosipitali alikuwa ameshapoteza maisha (dead on arrival) ama alitibiwa siku mbili tatu kisha bahati mbaya jitihada za matabibu hazikuzaa matunda, tatizo linakuja pale ndugu wanapofika hosipitali na kuambiwa kuwa mpendwa wao aliletwa hosipitalini kisha kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, hosipitali wanadai kiasi cha pesa cha vipimo ambavyo hakuna mwenye uhakika kama vilifanyika, na gharama za kuhifadhi maiti ambapo huduma zote hizi wamefanya bila kuwa na uhakika wa malipo (bila makubaliano) mwisho wa siku unakuta maiti inazuiliwa hosipitali kwa hiyo wewe uliyekuwa unamtafuta nduguyo umempata akiwa marehemu badala ya kupanga taratibu za maazishi inabidi ulipie kuchukua mwili hosipitali kwanza....gharama ambazo mara nyingi huanzia 1.5m-3m Tsh......ndugu yangu Athumani ntakuja kuchukua mwili sitoi hata senti tano siandiki barua kama ulivyonishauri siku hiyo utaniona na utanifahamu....

Wasaal
 
Mkuu jukumu lao la kwanza wanapo pokea mgonjwa wanapaswa kumpa huduma kisha mambo mengine yaendelee

Love and peace
 
Sasa unataka ndugu yako aifadhiwe bure ? Ukimsusa atazikwa na serikali.
 
Back
Top Bottom