KERO Wizara ya Afya inawahujumu wanafunzi walioko masomoni nje ya nchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Pamoja na kwamba ni jambo jema kuutangazia umma kua wanafunzi kadhaa wamepata ufadhili kupitia wizara ya afya(siku hizi wamebadili jina wanaita Dr Samia super-specialized scholarship program), lakini nyuma ya pazia wanafunzi hao wanateseka haswa.

Mimi nafanya kazi moja ya nchi huku ughaibuni, Nina uthibitisho hasa kwa wale waliopata ufadhili mwaka jana kuja vyuo hivi vya nje ya nchi hawajalipwa pesa yoyote siyo ya kujikimu wala ada toka mwaka jana mpaka hapa ninapoandika sasa hivi, baadhi ya wanafunzi wamekua wakishindwa kuingia madarasani ama kushindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kwa wakati hivyo kuishia kufanya shughuli ambazo sizo zilizowaleta huku, hali ya maisha kwa wanafunzi hao walio wengi ambao ni wageni katika nchi hizi ni mbaya, wamekua wakijaribu kuomba usaidizi wa pesa za kujikimu kwa ndugu na marafiki huko Tanzania hali inayopelekea kuchokwa na kutosaidika tena kwa kua watu hao huamini mwanafunzi huyo amelipiwa kila kitu. baadhi ya balozi zetu tumekua tukijitahidi kuwasaidia pale tunapoweza lakin hali si nzuri. Imagine mtu alikuja huku mwezi wa nane mwaka jana, mpaka sasa ni miezi tisa hajawahi kulipwa hata senti mia kwa kisingizio kua siku wakiwalipa watawalipa kwa mkupuo, yaani watawekea pesa ya kujikimu(stipend) ya mwaka huo mzima pamoja na ada, nauli ya kuja na wengine wale wa miaka ya mbele zaidi pamoja na pesa ya research.

Sasa cha ajabu na cha kushangaza wanafunzi hao wameleta uthibitisho wa meseji za wahusika(coordinator na mhasibu) kutoka wizara ya afya wakiwajulisha kua kuna shida kidogo hivyo hawatolipwa pesa ya mwaka mzima badala yake watalipwa pesa ya miezi nane na hiyo ya miezi minne inayobaki haijulikani italipwa lini. Ni karibia mwezi sasa toka waambiwe hivyo lakini mpaka sasa hawajalipwa hata senti.

Kama tujuavyo maisha nje ya nchi ni ghali sana tofauti na nyumbani, masomo haya hasa ya afya yanahitaji utulivu wa akili na mwili, vipi hawa wataalamu watarudi na ujuzi waliotumwa kwenda kusomea kweli, mtu analala njaa, hela ya kodi hana darasani wengine hawaingii, wana stress tu mpaka huruma, vipi watamaliza vyuo kwa wakati kweli, kuna baadhi ya vyuo hutoza mpaka dollars 300 kwa aliyechelewa kulipa ada, nani atawalipia pesa hizi, lakini kwenye majukwaa utasikia "tunasomesha wataalamu nje ya nchi" ni aibu sana.

Ombi langu kwenu Jamiiforums, fuatilieni suala hili tuwasaidie hawa wataalamu, ni aibu na kukosa utu, kama ulisema utamsomesha mtu na ukautangazia umma basi fanya hivyo, hiyo siyo hisani tena ni lazima maana hao watu walisaini mikataba ya makubaliano ya kulipiwa gharama hizo kwa muda wote watakaokua masomoni,
leo nimesoma kwenye mitandao ya jamii kwamba waziri wa afya anasema wanatarajia kusomesha wataalamu zaidi ya elfu moja na wengine nje ya nchi nikabaki nawasikitikia hao watakaoomba nje ya nchi, ni aibu.

Kuhusu wale waliopo vyuo vya ndani sina uhakika kama wao wamelipwa ama na wao ni dana dana. kama kuna watu wanazitumia pesa hizo vibaya badala ya kuwapa wanafunzi kwa wakati ninaomba serikali yetu iwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe funzo kwa wengine.

Mwisho kabisa niwashukuru Jamiiforum kwa kuanzisha jukwaa hili, mnasaidia wengi na Mwenyezi Mungu awabariki.
 
kunae m1 huyo, alivyokua anatamba kwenda ughaibuni, cku hizi kila mda huko tsup kulia lia tyuuh.

Ila afadhar ulaya anakujua, ajichanganye huko huko. Woiiiih
 
Kila jukwaa upo. Heshima yako mkuu
 
Kibarua chako umekiweka rehani! Futa hiyo sentensi
 
Hili jambo zito na ni aibu Kwa Taifa letu wabunge wanalijua hili au kazi Yao kugonga meza tu na kumsifia raisi
 
WATASHUGHULIKIWA ILA LAZIMA WAJITOE SANA MANA KUNA WATU HAWAJALI MATATIZO YA WENZAO
 
Mkuu ni nchi hio kama hutajali kuitaja maana hata mimi nina jamaa yangu UK na ni mkimya sana inaweza kuwa anateseka lakini anashindwahata kuniambia,
 
Back
Top Bottom