Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kuna suala ambalo limenitatoza sana Hapo Muhimbili Hospital nalo ni suala la WAGONJWA WA AKILI.
Ktk kipindi kifupi nilipokuwa hapo Muhimbili nikiwa kitengo cha wagonjwa wa Akili nimeshuhudia Namna wagonjwa hao wanavyodhalilika kutokana na madaktari kutokujali kabisa wagonjwa hao.
Nimegundua kuwa kuna sababu nyingi zinazochangia madaktari kutokuonyesha utu kwa Wagonjwa hao na napenda kuziorodhesha hapa.

1. UCHACHE WA MADAKTARI upande wa Psychiatric department.
2 . Udogo wa Ward pamoja na mazingira ya wagonjwa wa akili ( Psychiatric ward facilities).
3. Kukithiri kwa Rushwa kwa wahudumu wote wa department hio ya wagonjwa wa akili.

Nimeshuhudia kwa macho yangu kuwa mgonjwa akiletwa na familia yenye uwezo anatazamwa vizuri kuliko yule aliye na familia isio na uwezo wa kutoa pesa.

Nimeshuhudia wagonjwa wa akili kulazwa VYOONI sababu hakuna Nurses wa kutosha kutazama na kudhibiti wagonjwa hao.

As you all aware madaktari wote WAMEKULA KIAPO.
na moja ya kipengele cha hicho kiapo ni
" To practise medicine with integrity, humility, honesty, and compassion—working with fellow doctors and other colleagues to meet the needs of all patients."

Napenda kuuliza je !
Where integrity, humility, honesty, and compassion here?
Kwanini Doctors wawekwe kwenye mazingira ya kuwawezesha kuvunja ahadi ya kiapo Chao kabla ya kuruhusiwa kumgusa mgonjwa? Km Daktari amefikia kukosa utu hata kwa mgonjwa asie jitambua kiakili huyo hafai kuhudumia mgonjwa yyt.

Mimi nimepita tu hapo na sitegemei kuja kufanya kazi ktk mazingira hayo ila naomba sana sana wizara yako ichungulie idara hio.
Sote tunafahamu changamoto zilizopo Nchini hasa ktk Idara hii ya Afya lkn this is too much.

Tumeni mpelelezi mmoja akapeleke hapo mgonjwa kisha asitoe pesa aone Kipi kinafanyika. Ni udhalilishaji wa kupita kiasi.
Nikipata jibu la hili ombi langu ntakuja kujadili nilio yaona kwenye Ward ya Kina mama na Watoto.
Natamani ningekuwa na uwezo kifedha ngebadili hii situation leo leo lkn Uwezo anatoa Mungu . Na yeye ndio mwenye Hekma za Nguvu zote.

Mungu tunakuomba Itazame Nchi yetu kwa jicho la huruma. Na uwape ujasiri wahudumu wa afya kufanya kazi kwa moyo mzuri ktk mazingira haya magumu .

Amin.
 
wizara tunaomba mtengeneza mfumo wa ufadhili E-Sponsorship,mana haufanyi kazi vizuri kwa wanao hitaji kujisajiri.
 
Wizara tulitangaziwa Leo kutakuwa na uzinduzi wa utaratibu wa kuwapata wahudumu ngazi ya jamii je ni Leo kweli t
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Naomba kujua juu ya taarifa hii
Screenshot_20240206_072755.jpg

Hii barua Ina ukweli wowote au ni feki
 
Wizara ya Afya, Toeni bhas Ajira,
Maana tumejitolea sana kwenye Hospital za Rufaa na still hamjatuona, tukaamua turud tyuu kupiga madili vijiwen.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Ila jamani mmezingua sana mlivyofanya mabadiliko kwenye Bima za afya kua kama mtu sio mama yako aubaba yako au mwanao et hawezi kutumia Bima yako.
Aisee haijakaa poa,kuna watu hawana wazazi kabisa basi fanyeni utaratibu wasiwe wanakatwa Bina km wenye wazazi na watoto.Na hapo mtu hospitali anaweza asiende miaka miwili.
Kwanini msiache mtu aingize ata mdogo wake au mkubw wake mwngn km Bibi/Babu zao kaka/Dada na watoto wa ndugu zao ambao saa hiyo unakuta ni Yatima na Ana jukumu la kuwalea…Yan inakuaje mnawakata hao watu Bima na unakuta hawana familia.
Fanyeni kitu mtengenez haki jamani,wengine tunaishi na mayatima na babu na bibi zetu wagonjwa kwann msitusaidie hao watu wakaingia kwny Bima zetu ili tuone nafuu yetu.Sio ulipie huku na huku wakati unajua kbs unakatwa na hiyo Bima ipo tu haitumik mara kwa mara.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Hawa nguchiro wakipewa maoni wanayafanyia kazi kweli?
 
Mgonjwa wa morogoro mmefikia wapi??? Jamaa ni kama anaumwa sana selikali mmekosa kumsaidia
 
Wizara naomba kama ikiwezekana, kwanini kusiwepo askari kwenye hospitali kubwa kama za mkoa au Rufaa hata za wilaya kwa ajili ya watu wanao pata ajali kuweza kupata PF3 kwa uharaka zaidi ili kuwahi kufanyiwa matibabu.

Hii itasaidia kuepuka mzunguko mrefu wa kutoka eneo la ajali hadi kituo cha polisi then hospitali. Sometimes majeruhi wanapoteza maisha au kupata implications zaidi kutokana na mzunguko uliopo. Kwa hospitali binafsi wanaweza kupata huduma ya kuwepo askari kwenye maeneo yao kwa kufuata utaratibu ambao wizara itaweka.
 
Back
Top Bottom