Wivu ni nini hasa?

Wivu ni nini hasa?

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,295
Reaction score
5,458
Habari za wakati huu wanajukwaa.

Kwa yaliyonitokea week end hii yamenipa maswali sana.

Hivi wivu wa mapenzi hua unasababishwa na nini?

Ukiwa na mume au mke akichepuka wewe roho inakuuma kwa sababu gani hasa?

Je unafikiria jinsi unavyomuhudumia au ? Na kwa mwanamke kwa nini unahisi wivu kwa mwenzi wako?

Naomba msaada hapa wa mawazo yenu wana jukwaa la MMU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kama unafuga ng'ombe, unamhudumia vizuri kuliko hata wewe mwenyewe unavyojihudumia.
Mwisho wa siku anakuja jamaa anamkamua ng'ombe wako maziwa na kuyanywa.
Na wivu katika mapenzi ni sawa na mfano huo!
Yaani wewe una mke mzuri kabisa, unampatia huduma zote, mwisho wa siku bwege fulani anamnyonya, inauma, na ndiyo wivu huo.
 
Huo mafano wako umelenga upande wa mwanamme je kwa wanawake wao how does this situations happen?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mafano wako umelenga upande wa mwanamme je kwa wanawake wao how does this situations happen?
Siku hizi sina wivu kabisa..... Sijui nimepatwa na nini mie....??????
 
Nafikiria vile anavyonifanya ndio anamfanya,zile raha ndio anazipata mwingine huko

Inauma
 
Huo mafano wako umelenga upande wa mwanamme je kwa wanawake wao how does this situations happen?

Sent using Jamii Forums mobile app
ameolewa, na anajitajidi kumhudumia mumewe vile awezavyo halaf ghafla asikie tu mumewe anamtu mwengine lazima ajiulize anakosa nn na huduma zote anapewa?🙈🙈
 
Sina la kuchangia ila matokeo ya wivu huwa ni mazuri kidogo ila mabaaaya sana.

Kuchapiwa demu tu inavyouma, je mke?
Ndiyo maana sina na siwezi kumsamehe mwanamke kwa kosa la usaliti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliishi na wamasai na wamang'ati aise yale maisha yao mazuri sana hawana wivu wakijinga kwa mwenza wao kikubwa atiwe au apate papuchi ila kwenye Mali ndyo atakuuwa ila sisi wivu wakijinga jingaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni mambo yenu huko mikoani, wivu mwisho Chalinze huku mjini hakunaga
 
Ni kama unafuga ng'ombe, unamhudumia vizuri kuliko hata wewe mwenyewe unavyojihudumia.
Mwisho wa siku anakuja jamaa anamkamua ng'ombe wako maziwa na kuyanywa.
Na wivu katika mapenzi ni sawa na mfano huo!
Yaani wewe una mke mzuri kabisa, unampatia huduma zote, mwisho wa siku bwege fulani anamnyonya, inauma, na ndiyo wivu huo.
Mkuu, hiyo analogy ya ng'ombe haifanani kabisa na uhalisia.

Maziwa ni product.
Ila yeye anagawa service. Service isiyohitaji maintenance yoyote. Ukiigharamia au la, ile service ipo tu, hawajimilikishi.
Ni service ya muda mfupi, na ni mali ya mhusika. Ni service ambayo utaipata tu hata na mwingine akipewa. Na itakuwa na sifa zile zile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muuliza swali yaonyesha huja oa,lkn pia yaonyesha hujawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi...ushauri wangu OA au uwe na mpenzi usikie anatoka na mwanaume mwingine,then turejeshee mrejesho wa swali lako....pia ningeweza kukujibu kiimani hasa kwa wanandoa kua mkisha oana mnakuwa mwili mmoja....sasa chukua wembe jikate mwilini mwako.
 
Mkuu Nina miaka nane sasa kwenye ndoa ambayo imebarikiwa watoto wawili.

Ila kuna situation imetokea ndio maana nikajiuliza hili swali. Ili nipate mawazo tofauti ya wadau humu JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mungu mwenyewe anajinasibu kuwa ni Mungu mwenye wivu, yaAni ukimwabudu yeye umwabudu yeye peke yake. Hataki kushindanishwa, hataki kulinganishwa na chochote kwa hiyo tabia hiyo tumerithi kutoka kwake, mtu akiwa na wewe unataka awe na wewe tu ukiona kuna mwingine anapewa umuhimu sawa na wewe roho inauma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom